Zana mpya: Viuawadudu vyakibaiolojia kwa wadudu wakuu wa kahawa

Kidomozi (Coffee Berry Borer), Ruhuka (Coffee Leaf Miner), au Utitiri (Red Spider Mite) - wadudu hawa na wengine hustawi katika hali ya joto linalopanda ambalo huletwa na mabadiliko ya hali ya hewa katika kilimo cha kahawa.
Dawa zitokanazo na mimea fulani ya kienyeji, zinazojulikana kama viuawadudu vya kibaiolojia, zinaweza kutumika kama vidhibiti na kupunguza kwa kiasi kikubwa idadi ya wadudu. Hii inasababisha mimea ya kahawa kuwa na afya na kukuza uzalishaji wa mazao na ubora.
Faida zake? Ikilinganishwa na viuawadudu vya kikemikali, viuawadudu vya kibaiolojia ni vya gharama nafuu na vinapatikana kwa urahisi. Vinaweza kuoza, ambapo husaidia kuhifadhi mazingira, na kukuza afya ya wakulima na watumiaji.
Angalia aina mbalimbali za viuawadudu vya kibaiolojia ambavyo tunapendekeza katika kipengele cha kisanduku cha zana cha "Utunzaji na ukuzaji wa mimea" -> "Udhibiti jumuishi wa wadudu na magonjwa"!