
Mabadiliko ya Tabia nchi kwenye sekta ya kahawa
Mabadiliko ya hali ya hewa yanatambulika kuwa tatizo la dunia. Madhara yake yametanabaishwa kwa ngazi za kimataifa, na katika sekta mbali mbali, ikiwepo pia sekta ya kilimo. Madhara yake katika uzalishaji wa kilimo yanatarajiwa kuongezeka kwa viwango tofauti, upungufu wa uzalishaji kwenye baadhi ya maeneo na mabadiliko ya kijiografia.
Sababu na athari za mabadiliko ya hali ya hewa kidunia zimeanza kufahamika sana na zitajadiliwa hapa kwa ufupi.
Ukweli wa jumla kuhusu mabadiliko ya tabianchi duniani
Ongezeko zaidi la joto duniani: Joto la wastani la dunia linaongezeka, hasusani jotoridi la chini. Kwa sababu kasi ya mabadiliko ni taratibu, mabadiliko yoyote hayatakuwa rahisi kubaini, hata kwa wakulima. Lakini wadudu waharibifu na magonjwa yanaweza kuenea zaidi pale kiwango fulani cha joto (hii ni vigumu kujua au kupima) kikivukwa.
Kasi ya kuongezeka kwa joto duniani si sawa kutokana na tabia ya bahari kunyonya 92% ya joto la jua, na kulisambaza kwa kupitia mikondo ya wima na usawa wa baharini. Bado kunaweza kuwepo miaka mingi ambapo joto za wastani halitaongezeka sana. Baadhi ya sehemu za dunia zinaweza kupata misimu ya baridi zaidi hapo upepo wa msimu utakapobadilika na kusababisha joto sehemu nyingine za dunia.
Kiwango cha mvua duniani kinaongezeka kwa sababu hewa iliyo na joto inabeba unyevu zaidi. Lakini, hii haimaanishi kuwa kanda zote zitapata mvua zaidi, bali kuwa itakaponyesha mvua, inaweza kunyesha zaidi. Hii inamaanisha kuwa mmomonyoko na maporomoko ya ardhi yaweza kuongezeka.
Dunia inajionea mabadiliko ya hali ya hewa yakizidi kukithiri, baadhi ya maeneo yakipata joto au baridi zaidi, au yakipata unyevu au kuwa kavu zaidi. Hii ni vigumu kuhakikisha kwa kutumia takwimu, lakini takwimu toka taaluma za kisayansi na sekta ya bima ya majanga zinaonyesha kuwa kuna ongezeko la hali ya hewa iliyokithiri. Hii inamaanisha kuwa wakulima wa kahawa wanaweza kujionea mabadiliko ya hali ya hewa yakikithiri, ikiwemo joto na baridi.
Athari za hali ya hewa na tabia nchi kwa zao la kahawa (angalia ufafanuzi hapo chini) zinajitokeza kwa ngazi mbalimbali za nyakati.
- Matukio ya muda mfupi kama vile dhoruba au tufani ya kitropiki.
- Matukio ya muda wa kati, kama vile El Nino na mizunguko mengine inayochukua miezi au miaka kutokea.
- Hali ya hewa ya muda mrefu au mwenendo wa hali ya ukame unaoweza kuchukua miaka au miongo kadhaa kukamilika.
- Hali ya joto la muda mrefu kama vile joto la wastani la dunia linavyotarajiwa kuongezeka kwa miaka 100.
Athari za tabia nchi: ingawa kuna uelevu imara wa kisayansi juu ya sababu za Mabadiliko ya Tabia nchi, bado kuna upungufu wa ujuzi juu ya athari zake kwa mazingira maalum, ambapo kiwango na mtandao wa madhara ya mabadiliko ya tabia nchi ni tofauti sana na kukosekana kwa uhakika. Mara nyingi, kutopatikana kwa takwimu bora kutoka vituo vya hali ya hewa inasababisha kutoelewa kikamilifu jinsi gani tabi nchi inavyobadilika. Kipengele muhimu cha Mfumo wa c&c ni kuwezesha uamuzi wa kitaalamu juu ya hatari za mabadiliko ya tabia nchi kwa mazingira tofauti tofauti
Hii ina maana gani kwa wakulima?
Wakulima wananashuhudia kukithiri na kutotabirika kwa hali ya hewa. Hawawezi tena kutegemea kupata hali yenye kufaa kwa uzalishaji wa mimea ya kudumu kama vile kahawa kwa mavuno mengi. Hii inaathiri sana maisha na mikakati yao: je, wawekeze zaidi kwenye makabiliano au kwenye mazao mengine?
Kuna vidokezo vinavyoshabihiana juu ya muundo wa kuwasaidia wakulima. Kushindwa kutabiri inafanya iwe vigumu sana kutoa ushauri ulio sahihi na jinsi ya kuweka kipaumbele kwenye matumizi ya rasilimali ili kupunguza hatari. Madhumuni ya Mfumo wa c&c ni kusaidia kutoa huduma hizi, kupanga na kujaribu mbinu na zana ili kutathmini vihatarishi muhimu zaidi vya Mabadiliko ya tabia nchi na kurahisisha kupunguza athari.
Hali ya hewa: hii inaeleza hali ya anga sehemu maalum kwa kuzingatia joto la hewa, shindikizo, unyevu, kasi ya upepo, mawingu na mvua.
Tabia nchi: mara nyingi hii inafafanuliwa kama hali ya anga kwa wastani wa muda mrefu (kawaida miaka 30)
Uoto wa Dunia: ni kuongezeka kwa joto la wastani duniani.
MabadiliKo ya tabia nchi: badiliko lolote adhimu la hali ya hewa, kama vile joto au mvua, linayodumu kwa muda mrefu, kwa kawaida kwa miongo, ambapo chanzo chake ni matukio ya kawaida au shughuli za binadamu.
Utofauti wa hali Tabia nchi: hii inamaanisha utofauti kwenye hali ya sasa ya hewa, k.m. kiwango cha mvua iliyonyesha mwaka hadi mwaka; pamoja na ukame wa muda mrefu, mafuriko, na hali inayosababishwa na matukio ya mara kwa mara ya El Niño and La Niña (ENSO).
Ongezeko la joto la ukanda au ndani: hii inaweza kusababishwa na mabadiliko ya matumizi ya ardhi na inaweza kuharibu kabisa hali ya hewa ya huo ukanda na kukithiri kwa joto.
Hatari za Hali ya Hewa: Matukio hatari maji ya mvua ama mafuriko au matukio kama vile kuongezeka kwa joto au mabadiliko ya msimu wa mvua pamoja na ukubwa na kasi ya kukithiri kwa matukio kama vile dhoruba, mafuriko au ukame.
Athari za Tabia nchi: Madhara yatokanayo na Mabadiliko ya tabia nchi kwenye mifumo ya mazingira au binadamu.
Hali ya hewa inaathirije uzalishaji wa kahawa?
Uzalishaji wa kahawa unategemea sana mpangilio wa kawaida wa hali ya hewa. Hali ya hewa inayofaa kwa uzalishaji wa zao la kahawa ya Arabika ni:
- Kipindi kikavu/ jua cha miezi mitatu ambapo mkazo unawekwa kwenye miti ili maua yachanue vizuri; lakini kipindi kikavu hakitakiwi kiwe kirefu sana la sivyo miti inakuwa dhaifu.
- Kipindi cha mvua za wastani ili kuchanua lakini isiwe mvua ya kudumu kwani hii itaathiri matunda kushika.
- Joto lisiwe la juu sana (la wastani) inaweza kusababisha shida mbali mbali kwenye umbile la mti, pamoja na kuungua kwa maua.
- Mvua ya kawaida kwa msimu/ kipindi kizima cha kukuwa kwa matunda.
- Kipindi kikavu (jua) sana kuendelea hadi mavuno.
- Kipindi kikavu wakati wa mavuno ili kurahisisha uvunaji na ukaushaji wa kahawa (hii ndiyo hali ya ubora wa kahawa lakini si hali halisi katika nchi zote zinazozalisha kahawa).
Mabadiliko katika mifumo ya hali ya hewa joto, dhoruba, upepo mkali na hali ya hewa kukithiri zinaathiri obora wa kahawa moja kwa moja, na viwango vya tija. Matukio haya yanayoweza kuwa yenye u haribifu yanaitwa .
Madhara ya Mabadiliko ya tabia nchi katika mifumo ya mazingira au binadamu huitwa athari za tabia nchi. Hizi zinaweza kuwa athari za moja kwa moja (kwa mti wa kahawa) au siyo za moja kwa moja. Baadhi ya athari mbaya ya Mabadiliko ya Tabia nchi (CC) kwa kahawa ya aina ya Arabika, ambazo ni rahisi zaidi kubaini zimeorodheshwa kwenye Jedwali Na. 1 hapo chini.
Robusta pia inaathiriwa na kukithiri kwa tabia nchi, ingawa inaweza kuvumilia joto kalizaidi na ni inahimili zaidi dhidi ya baadhi ya wadudu na magonjwa. Hii inaweza kuwa mojawapo ya sababu ya ongezeko la uzalishaji wa Robusta duniani, toka 20% hadi 40% kuanzia mwaka 1980. Lakini Robusta inahitaji mvua zaidi, ambayo (kutokana na uwezekano wa matukio ya ukame ya muda mrefu) itamaanisha kuwa umwagiliaji utahitajika zaidi.
Hali ya hewa kukithiri kwa kipindi cha miaka michache iliyopita (k.m. mvua nyingi iliyonyesha kati ya mwaka 2009 hadi 2011 nchini Kolombia, au ukame wa mwaka 2014 Minas Gerais nchini Brazil) inaonyesha kuwa kunaweza kuwa na madhara makubwa kwa kipato na kwa hiyo, uchumi wa wakulima. Inawezekana kuwa matukio kama haya yangeweza kutokea bila kuwepo kwa mabadiliko ya hali ha hewa, lakini pia inawezekana kuwa yamekuwa yakikithiri zaidi kwa sababu yake.
Matokeo ya ujumla ya athari za hali ya hewa kukithiri ni upungufu wa ubora na tija ya kahawa, pamoja na ongezeko la gharama za uzalishaji na mahitaji zaidi ya pembejeo na nguvukazi.
Jedwali 1: Madhara mbalimbali ya Mabadiliko ya Tabia Nchi kwa miti ya Kahawa aina ya Arabika
Kihatarishi | Athari ya moja ka moja kwa mti wa kahawa | Athari nyingine |
Joto kali |
|
|
Mvua kali, mvua ya mawe, upepo mkali |
|
|
Mvua fupi na zisizo za msimu |
|
|
Mvua za muda mrefu |
|
|
Ukame wa muda mrefu |
|
|
Kuratibu Mwitikio wa Mabadiliko ya Tabia nchi
Ili kupata picha kamili ya makabiliano dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi (CC), Mwitikio unahitajika kupangwa na kuratibiwa kulingana na uzito na ukubwa wa matukio ya hali ya hewa (Jedwali Na. 1). Wakulima wanajionea matukio haya kama matukio ya kushitua na siyo mabadiliko ya taratibu. Mwongozo huu unashughulika zaidi na mraba wa juu upande wa kushoto kwenye jedwali Na 1 “makabiliano kwa kupitia tabia mpya za kilimo” ambayo inajumuisha tabia, mkakati au hatua zozote zinazochukuliwa kuitikia Mabadiliko ya tabia nchi. Lakini, c&c inalenga kutayarisha zana kwa upande wa kulia wa jedwali, yaani “zao mbadala au vitega uchumi vingine” kwa miaka ya mbele.

Kuangalia umuhimu wa kukabiliana na Mabadiliko ya Tabia nchi (CC) kimkakati
Mabadiliko ya hali ya hewa ni swala lenye utata sana na bado hakuna uhakika juu ya jinsi itakavyoathiri mifumo ya uzalishaji kwa miaka ya mbele. Pia, uzalishaji wa kahawa si kitu rahisi na hutofautiana sana nchi mmoja hadi nyingine. Lakini, mara nyingi mifumo ya uzalishaji inayotumiwa kwa kila ukanda huwa haibadiliki na hubadilika kwa kiasi kidogo sana kwa muda mrefu. Hii inamaanisha wakulima wa kahawa wanahitaji kuwekeza muda wa kutosha na rasilimali fedha za kutosha ili kuwawezesha kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabia nchi.
Hali ya sasa ya ujuzi wa kahawa na Mabadiliko ya Tabia nchi (CC) inaonyesha kuwa wadau watahitaji kufikiria mabadiliko makubwa sana kwa miaka ya mbele. Inaelekea pasipo epukika kwamba:
- Baadhi ya kanda zilizokuwa na utamaduni wa kuzalisha kahawa hazitafaa tena kwa kilimo cha kahawa, hali ambayo italazimisha kutafuta mazao mbadala. Hii hali imeshaanza kuonekana katika nyanda za chini katika nchi nyingi zinazozalisha kahawa, lakini utafiti na ufadhili wake ni hafifu sana.
- Maeneo mengineyo ya kiutamaduni yataendelea kufaa kwa kilimo cha kahawa kwa miaka mingi, lakini mbinu mpya za kilimo zitahitajika ili kukabiliana na Mabadiliko ya Tabia nchi (CC), na hasa dhidi ya matokeo ya hali ya hewa iliyokithiri.
- Baadhi ya kanda/ maeneo yataanza kufaa kwa kilomo cha kahawa.
Mwongozo huu unajihusisha na kipengele cha 2) tu; vipengele 1) na 3) vinahitaji vinzingatiwe na kuwekewa mipango pia iwapo itatokea kwa njia ya kuongeza uendelevu na kupunguza uharibifu kwa jamii na mazingira. Hivyo, mpango wa kimkakati wa makabiliano unaoelezwa hapa unahitaji kuonekana kama sehemu moja tu ya mkakati mzima, ambao unavuka mipaka ya uzalishaji wa kahawa peke yake.
Ufafanuzi
Makabiliano na Mabadiliko ya Tabia nchi
Mabadiliko ya mifumo ya kiasili na ya kibinadamu kama mwitikio wa hatari (stimuli) zinazotarajiwa au zinazotokea (athari za mabadiliko ya tabia nchi) au athari zake, ambayo itapunguza athari au kufaidika na fursa zinazojitokeza
Kuchua hatua zitakazo lenga kupunguza athari mbaya za mabadiliko ya tabia nchi au kutumia fursa.
Tunawezaje kuitikia Mabadiliko ya tabia nchi (CC)?
Nini maana ya vihatarishi vya tabia nchi na uwezo wa kukabili?
Athari za mabadiliko ya hali ya hewa yanaonekana dhahiri katika nchi, hii inamaanisha kuwa mwitikio pia unahitaji kufafanuliwa kwa ngazi ya sehemu au ukanda husika. Makabiliano halisi dhidi ya Mabadiliko ya tabia nchi yanahitaji uelewa mzuri juu ya hali ya vihatarishi kwa mfumo husika wa kilimo cha kahawa na jamii za wakulima.
Athari za Mabadiliko ya Tabia nchi (CC) kwa uzalishaji wa kahawa inategemea sana ustahimilivu (angalia kamusi ya maneno yanayohusika na hali ya hewa ukurasa wa 15) au nguvu ya mfumo husika. Si lazima kuwa neno “mfumo” limaanishe uzalishaji wa shambani tu, bali inamaanisha pia jamii za wakulima, na mazingira yote ya ugavi, pamoja na miundo mbinu kama bara bara, maghala ya kuhifadhi mavuno, n.k.
Kwa hiyo, mkakati wa makabiliano inawezekana ukawa umedhamiria kuongeza ustahimilivu wa makundi ya watu pamoja na ustahimilivu wa mifumo yao ya uchumi wanayoitegemea. Kwa sababu hii, vihatarishi kwa mifumo ya kahawa pamoja na jamii ni muhimu kwenye kuzingatia athari za Mabadiliko ya Tabia nchi (CC).
Kihatarishi kinaweza kufafanuliwa kama hali ya. Mara nyingi inaelezwa kama matokeo ya sababu kadhaa (Jedwali Na 2) na hivyo dhana hii inaweza kuwa vigumu kuitumia au kuileza. Istilahi tofauti zinazotumika hapa zinaelezwa kwa urahisi zaidi, kwa mfano:
Mkulima anaweza kuona kuwa shamba lake linashambuliwa zaidi na kutu ya majani (Hemileia vastatrix) kutokana na Mabadiliko ya Tabia nchi (CC) (joto kupanda na unyevunyevu kuongezeka). Aina ya kawaha (Coffea Arabica) inahatarishwa na ugonjwa huu na hivyo ni yenye mguso sana. Mkulima hataweza kuepukana na tatizo hili bali anaweza kuamua kupunguza unyeti kwa kuweka dawa ya fangas mara kwa mara au kwa kupanda aina nyingine ya kahawa iliyo na ukinzani dhidi ya kutu ya majani,kupata mbinu sahihi si jambo rahisi na itabadilika kulingana na hali halisi ilivyo. Kama mkulima atapata ushauri wa kitaalam, au akiongeza ujuzi na akiwa na rasilimali fedha za kutosha kumwezesha kufanya uamuzi, basi anatambulika kuwa na uwezo wa makabiliano mzuri. Hivyo, hata kama uwezekano wa mashambulizi ya ugonjwa utaendelea kuongezeka, mkulima anaweza kusawazisha hii kwa kupunguza hatari.
Kama inavyoonekana kwenye Jedwali Na 2, Kihatarishi cha hali ya hewa kwa mfumo wa uzalishaji inaunganisha athari kutokana na kutoweza kuepukana na tatizo na unyeti dhidi ya Mabadiliko ya tabia nchi, pamoja na uwezo wa makabiliano au uwezo wa kupunguza hatari za kimfumo au mkulima. Sababu hizi pamoja zinamaanisha kuwa athari za Mabadiliko ya Tabia nchi (CC) shambani ni matokeo ya uhusiano kati ya idadi na uzito wa tukio, kama inavyoonekana kwenye jedwali Na 1. Ni muhimu kurejea jedwali Na 2 ni marahisisho ya mfumo wenye utata usio wa mstari wa kunyooka, na ambao kwa sababu tofauti (ikiwemo kutu ya majani) unaeleweka kwa kiasi tu.
Hivyo, madhumuni ya mwongozo huu ni kusaidia wakulima na wale wanaowasaidia kuongeza uwezo wa makabiliano. Mbinu za makabiliano ni hatua hai zinazodhamiria kupunguza vihatarishi na athari za hali ya hewa. Jedwali Na 2 linaonyesha baadhi ya mifano jinsi gani wazalishaji wa kahawa wanavyoweza kuitikia athari ya hali ya hewa zilizoorodheshwa kwenye Jedwali Na 1., na hivyo kupunguza madhara ya hali ya hewa kwa kutekeleza na kuchagua mbinu za makabiliano.
Mbinu za makabiliano zinaweza pia kuwa hatua zinazoitikia vihatarishi maalum vya hali ya hewa kwa njia isiyo ya kawaida. Kwa mfano, njia zinaweza kuwa kutoa mafunzo kwa jamii juu ya jinsi ya kuanzisha shughuli za kiuchumi zisizo za shambani.
Ni muhimu pia kutambua kuwa utayarishaji wa jinsi ya kukabiliana si tu suala la kuweza kusalimika kutokana na matukio ya hali ya hewa kwa muda mfupi. Inazingtia pia kuwajengea watu binafsi na jamii uwezo wa kukabiliana na mabadiliko katika mazingira yao na kuleta matokeo ya muda mrefu yanayowezekana kijamii na kiuchumi.

Mwongozo
Uwezo wa makabiliano
- Uwezo wa makabiliano unaweza kuongezwa kwa kuongeza rasilimali fedha na utaalamu wa wakulima, na kwa kuwezesha watu binafsi na mashirika kuitikia ipaswavyo vihatarishi vya Mabadiliko ya Tabia nchi (CC).
- Uwezo wa makabiliano unaweza kuongezwa kwa kutumia mbinu pendekezwa za makabiliano, k.mf. Kuwafundisha wakulima jinsi ya kutengeneza mifumo ya umwagiliaji yenye ufanisi zaidi, na jinsi ya kujenga mifumo ya kuhifadhi maji, au pia kwa kuboresha upatikanaji wa fedha kwa kupitia mikopo ya riba ndogo.
Jedwali 2: Madhara ya Mabadiliko ya Tabia Nchi, Vihatarishi, na Mbinu za Makabiliano kupunguza madhara
Kihatarishi | Adhari za moja kwa moja | Kinga |
Joto kali |
|
|
Mvua kali, mvua ya mawe, upepo mkali |
|
|
Mvua kipindi ki fupi na zisizo za msimu |
|
|
Mvua za muda mrefu |
|
|
Ukame wa muda mrefu |
|
|
Ustahimilivu
Miaka ya karibuni, neno ustahimilivu limeanza kutumika mno, sawa na neno “endelevu” linavyotumika kwa namna na mazingira tofauti tofauti. Kwa madhumuni ya mwongozo huu, maana ya ustahimilivu ni uwezo wa kuitikia kwa ufasaha athari za Mabadiliko ya Tabia nchi, na wakati huo huo tukiendelea kufanya kazi kwa kiasi kinachoridhisha. Ufafanuzi mzuri wa ustahimilivu kwa mfumo wa uzalishaji wa :
- Kiwango cha uharibifu ambacho wazalishaji wa kahawa wanaweza kumudu wakiendelea bila mabadiliko yoyote (uwezo wa kuyaishi mabadiliko);
- Kiwango cha marekebisho ambacho wazalishaji wanaweza kufanya kama mwitikio wao dhidi ya Mabadiliko ya Tabia nchi (uwezo wa kujirekebisha ili kuendana na mabadiliko)
- Uwezo wa wazalishaji wa kahawa kujifunza juu ya nini inahitaji kubadilishwa na jinsi ya kutekeleza mabadiliko hayo (uwezo wa kujifunza kutokana na uzoefu na kutumia ujuzi mpya kwa kuboresha mipango ya mbele).
Ustahimilivu unahitaji ushirikiano mzuri (k.m. kati ya jamii, serikali na wafanyabiashara), pamoja na mfumo nyumbufu unaoweza kusaidia mafunzo kutokana na uzoefu, na inayoweza kutumika kwa mipango ya miaka ya mbele (angalia Hatua ya 5 ya Mkakati wa c&c)
Jinsi ya kufikria makabiliano
Mara nyingi makabiliano dhidi ya hali ya hewa yanaongelewa kama njia ya kupunguza hali ya hatari. Ingawa hii ina faida yake, mpango wa c&c unafaa zaidi kuifikiria kuhusiana na njia za kuongeza ustahimilivu na kujenga uwezo wa makabiliano. Jilio hili ni bora zaidi na unaweza kurahisisha ushirikiano wa wadau kwa kujadili fursa za kuongeza ustahimilivu wa asili badala ya kuwatazama kama wahanga wa Mabadiliko ya tabia nchi. Ujumbe unatakiwa uwe kuwa makabiliano yanamsaidia mkulima kuwa mzalishaji aliyestawi zaidi.
Istilahi na ufafanuzi kwenye suala la Makabiliano na Mabadiliko ya Tabia nchi
Hatari (Kihatarishi): Uwezekano wa matokeo yaliyo na madhara au hasara (k.m. vifo, majeruhi, vifo, kupoteza makazi, kupunguzwa kwa uzalishaji wa kiuchumi na/au uharibifu wa mazingira) unaosababishwa na mwingiliano kati ya hatari za tabia nchi, . Hatari inaweza kufikiriwa kama mwingiliano kati ya majanga na hali ya kuathiriwa kama vile ilivyoonyeshwa kenye Jedwali Na 2. Mara nyingine inaonyeshwa kama: Hatari= MajangaX hali ya kuathiriwa. Lakini kwenye vitendo hai ni vigumu kuyapa vifungu hivi kipimo na kutumia hesabu hii shambani.
Kuwa wazi: Kiwango cha mfumo (k.m. shamba, mfumo wa uzalishaji au mti wa kahawa) katika sehemu husika imetanzuka na hali ya mabadiliko (k.m. mti wa kahawa unapata unyevunyevu mwingi). Hii ni vigumu zaidi kudhibiti, lakini inaweza kubadilishwa kwa kupunguza kivuli kwenye baadhi ya mazingira, ingawa hii italifanya shamba liwe wazi kwa mabadiliko mengine ya hali ya hewa.
Usitahimilivu: Kiwango cha uvumilivu wa mfumo k.m. shamba, mfumo wa uzalishaji au mti wa kahawa) dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi. Kwa mfano, mti wa kahawa unaopata kutu ya majani ni unastahimili ongezeko la joto la chini na uwingi wa mvua katika hatua muhimu za mzunguko wa maisha yake. Upandaji wa miche inayostamili zaidi kutu inaweza kupunguza unyeti.
Kuathirika: Kiwango cha mfumo kuhatarishwa au kushindwa kukabiliana na athari mbaya za Mabadiliko ya tabia nchi, ikiwemo pia hali ya hewa inyotofautiana au inayokithiri. Kwenye uzalishaji wa kahawa, vihatarishi vinaweza kuongezeka kupitia mashina ya zamani ya mti wa kahawa, ardhi dhaifu, ujuzi dhaifu n.k.
Uwezo wa Makabiliano: Uwezo wa mfumo kujirekebisha kulingana na hali ya hewa inyotofautiana au inayokithiri, kutumia fursa au kukabiliana na matokeo. Kwa mfano, wakulima walio na uwezo mkubwa wa makabiliano wanaweza kurekebisha tabia zao za kilimo kulingana na hali ya ukame kushinda wale walio na uwezo mdogo wa makabiliano. Uwezo wa makabiliano ni pamoja na ujuzi wa vitendo hai, uzoefu, rasilimali fedha na mtandao wa kijamii wa wakulima na maafisa ungani.
Utengamafu: Uwezo wa mfumo kupinga, kuduta au kurejea hali yake baada ya madhara ya tabia nchi. Jamii ya wakulima wa kahawa iliyo tengamaa watakuwa na uwezo wakudhibiti majanga, kupunguza madhara yake na/au kupona haraka baada ya madhara kutokea, na kuibuka wakiwa sawa au bora kushinda walivyokuwa kabla ya adhari kutokea. Kuna kiungo cha karibu sana kati ya utengamafu na Uwezo wa makabiliano, na hivyo utengamafu unatofautiana sana kwa vikundi mbalimbali ndani ya jamii.
Makabiliano hafifu: Ni vitendo ambavyo vinaonekana kama vile vya makabiliano, lakini vinavyoweza kutokuwa na faida/ manufaa. Kwa mfano, wakulima wa kahawa kwenye maeneopembezoni (mf. Joto sana au ukame mara kwa mara) wanaweza kujitahidi kurekebisha mfumo wao wa uzalishaji wa kahawa, lakini badala yake wangesaidiwa zaidi kwa chagua mbinu tofauti kwani joto litazidi kuongezekwa kwa vyovyote vile.
Ni jinsi gani wazalishaji wa kahawa wanaweza kukabiliana na Mabadiliko ya Tabi anchi?
Makabiliano yanamruhusu mkulima kupunguza athari mbaya za mabadiliko ya Tabia nchi, na kufaidika kutokana na fursa mpya zinazosababishwa nayo.
Makabiliano kwa uzalishaji wa kahawa yanaweza kuzingatiwa kwa njia mbalimbali, ambazo zinaweza kupangwa kwa kufuata vipimo vilivyooneyeshwa kwenye Jedwali Na 3.
Hadi leo, c&c imejizatitia zaidi majaribio mashambani kwa vitendo na kwenye jamii. Mpango unatambua kuwa masuala ya mandhari ni muhimu sana, lakini haya yanahitaji kutatuliwa kwa kupitia kwa kuwa na mwongozo bora kuliko ilivyokuwa hadi sasa. Walakini, hatua tano za Mpango wa c&c zitaruhusu kuzifanyia kazi kwa ngazi hizi mbalimbali za makabiliano. Lengo ni kuwasaidi wadau kutambua na kutekeleza mbinu za mbinu zinazofaa ili kuifanya mifumo ya uzalishaji, wakulima wa kahawa na jamii kutengamaa zaidi na kupungua kwa hatari ya kuathiriwa maisha yao
Jedwali 3: Ngazi mbali mbali na mbinu za makabiliano
Ngazi ya kinga | Maelezo | Mifano ya mbinu za kinga |
Mmea | Hatua za kuongeza kinga ya mmea dhidi ya tabia nchi |
|
Shambani | Hatua za kuongeza kinga ya shamba zima, hasa kwa kubadilisha mbinu za kilimo |
|
Nyumbani na mfumo wa kilimo | Hatua za kutayarisha kaya kujikinga dhidi ya tabili za hali ya hewa zinazotolewa |
|
Eneo kuzunguka shamba | Hatua za kuongeza ustahimilivu wa shamba la kahawa kwa ujumla |
|
Sera na mipango | Hatua za kisera za kuwezesha wakulima katika shughuli zao za kilimo kwa ujumla |
|
Je, Wadau wana wajibu gani kwenye mchakato wa makabiliano?
Utambuaji na uhusishaji wa jamii husika (yaani, “Wadau”) ni ufunguo wa mafanikio ya mchakato wa makabiliano. Wadau wanachangia kupitia ujuzi na maarifa waliyonayo.
Ukamilifu wa ujuzi na maarifa haya, ndio yatawaongezea wadau taarifa zaidi juu yamchakato na sababu za kimsingi, na itasaidia zaidi kuchagua maamuzi yatakayoleta mafanikio. Hii inajumuisha pia utambuzi wa thamani ya ujuzi wa kienyeji na wa kiasili.
Lengo la kwanza la kuwahusisha wadau ni kujenga uelewa wa pamoja juu ya hali na kiwango cha vihatarishi vya hali ya hewa, na pia kupanga mikakati ya makabiliano kwenda sambamba na uwezo wa kuiuchumi, mahitaji yao na mila za jamii husika.
Ufanafuzi
Mdau ni nani?
Kuna mawazo mengi tofauti juu ya ufafanuzi wa mdau, na ni muhimu kuamua ufafanuzi upi utumike.
Kwa Mpango wa c&c, wadau wanajumuisha kaya za wakulima, wataalamu wa wa kahawa wa ndani na wa ukanda, maafisa ugani, bodi za kahawa za taifa, wawakilishi wa mashirika ya serikali na yasiyo ya serikali, watafiti wa ndani, ukanda na wa kimataifa, na hata vito vya utafiti vya kimataifa, Wizara za Kilimo, an/au Mazingira, mashirika ya wazalishaji, na wahusika wengine sekta binafsi kama vile taasisi za usajili na vyeti, wafanyabiashara, wakaangaji wa kahawa, mashirika ya ufadhili, benki, na wakala wa maendeleo, n.k.