Sehemu ya Mwalimu
Mabadiliko ya Tabia nchi kwenye sekta ya kahawa
Mabadiliko ya hali ya hewa yanatambulika kuwa tatizo la dunia. Madhara yake yametanabaishwa kwa ngazi za kimataifa, na katika sekta mbali mbali, ikiwepo pia sekta ya kilimo. Madhara yake katika uzalishaji wa kilimo yanatarajiwa kuongezeka kwa viwango tofauti, upungufu wa uzalishaji kwenye baadhi ya maeneo na mabadiliko ya kijiografia.
Sababu na athari za mabadiliko ya hali ya hewa kidunia zimeanza kufahamika sana na zitajadiliwa hapa kwa ufupi.
Jifunze zaidi
Mpango wa c&c wa Makabiliano dhidi ya Mabadiliko ya Tabia nchi kwa Sekta ya Kahawa
Jilio la c&c ni mpango wa hatua tano ambazo zinawawezesha wakulima wa kahawa kuitikia mabadiliko ya tabia nchi kwa ufanisi kwa kufuata mpangilio wa kutathmini vihatarishi, pamoja na kutambua na kutekeleza mbinu za kukabiliana zitakazowafaa.
Jifunze zaidiUtangulizi wa mabadiliko ya tabia nchi na utofauti wa hali ya hewa
Kama ilivyofafanuliwa na IPCC kuwa ni mabadiliko ya muda mrefu katika joto na mvua, mabadiliko ya tabianchi yanasukumwa zaidi na shughuli za kibinadamu na ongezeko la gesi chafu. Matokeo yake? Hali ya hewa kali na isiyotabirika zaidi, mifumo ya mvua inayobadilika, na ongezeko la joto duniani. Kilimo, kinachotegemea sana hali thabiti ya mazingira, kiko hatarini mno. Mabadiliko ya tabianchi yanafanya kazi kama kizidisho cha hatari – yakiunda changamoto mpya na kuongeza zile zilizopo kwa wakulima kote ulimwenguni.
Jifunze zaidi