Chagua njia shirikishi ya majaribio na utekelezaji
- Shule ya wakulima
- Majaribio
- Shamba darasa
- Kutembeleana
- Siku ya mkulima
- Chagua mbinu za makabiliano zilizojaribiwa katika eneo lako
- Mbinu inayofaa baada ya kujaribiwa ndiyo inayotekelezwa

Hatua ya 4 inasisitizia masahihisho na utekelezaji wa mbinu za makabiliano shambani (angalia Umbo Na 18). Kulingania na mahitaji ya mbinu zako, utekelezaji unweza kuanzia mafunzo (k.m. kwa kupitia Shamba Darasa) hadi kufikisha utaalaumu juu ya mbinu maalum za makabiliano, na hata kuanzisha vwanja vya majaribio
Kulingana na aina ya mbinu la makabiliano, muda unaohitajika unaweza kuanzia miezi michache hadi miaka michache. Kwa mfano, ujenzi na majaribia ya kifaa cha kukaushia kwa kutmia minzi ya jua ili kuboresha ukaushaji wakati wa majira ya mvua inaweza kuchukua miezi 6 hadi 12; kuotesha miche ya kahawa kwa kutumia viroba vikubwa zaidi na/au Micorrhizas inaweza kuchukua miezi 4 hadi 6; kuanzisha kivuli na kusahihisha upandaji wa miti inayofaa kwa kivuli na vipimo kutoka mti mmoja hadi mwingine inaweza kuchukua miaka kadhaa.
Masahihisho maana yake kujaribu na kutathmini mbinu ya makabiliano ili kuhakikisha kuwa ni fanisi, inawezekana, na inakubalika na jamii ya wakulima. Masahihisho kwaida yanafanyika kwanza kwa kiwango kidogo (k.m. kwa mashamba machache au kwa sehemu maalum) kabla ya kuanza utekelezaji kwa kiwango kikubwa zaidi. Inashauriwa kuwa masahihisho yafanyike kama mbinu la makabiliano ni jipya na bado haijulikani matokeo shambani yatakuwaje, au kama wakulima wanaonyesha mashaka juu ya mafanikio yanayowezekana. Utekelezaji utendeke kwa kiwang kikubwa (k.m. kwa kikundi kikubwa cha wakulima au eneo kubwa la uzalishaji) pale panapofahamika kuwa matokeo yatakuwa mazuri na tathmini inaonyesha kuwa mbinu linafaa mfumo maalum wa uzalishaji. Lakini bado inawezekana kuanza utekelezaji kwa kiasi kikubwa bila masahihisho kama mbinu la makabiliano linafahamika vizuru na matokeo mazuri yameshawahi kuonekana kipindi cha nyuma. Kuna baadhi ya mbinu shirikishi za mchakato wa kusahihisha na kutekeleza mbinu za makabiliano (angalia Jedwali 14).
M&E ni muhimu kwa kipindi kizima cha mchakato wa masahihisho na utekelezaji. M&E nzuri inawezesha shirika la utekelezaji na jamii ya kienyeji kujifunza na kurekebisha shughuli kuitikia matokeo. Pia ni muhimu kwa wengine wanaoangalizia kutekeleza shughuli kama hizi za makabiliano. Hatua ya 5 intoa taarifa zaidi juu ya mchakato wa M&E na mafunzo ya pamoja.

Hatua ya 4 inahusu shughuli za shambani. Baada ya masahihisho kwa kiwango kidigo (kana inahitajika), na kuna amani kuwa matokeo ya mbinu la makabiliano zitakuwa ni nzuri, utekelezaji kwa kiwango kikubwa zaidi unaweza kuanza.
Ifikapo mwisho wa hatua hii, utakuwa umechagua mbinu bora zaidi za kuwafundisha wakulima juu ya utekelezaji na watajua ni nini wafanye ashambani.
Utakuwa umeweka kumbukumbu juu za athari ya mbinu la makabiliano kwenye mmea, udongo na mazingira, na utaweza kuzitumia kutathmini ufanisi wa mbinu kwa ujumla. Lakini, takwimu za ufwatiliaji inayohusikana na utendaji wa mbinu (k.m. mabadiliko ya hali ya udongo) ni sehemu moja tu ya mchakato mpana zaidi wa M&E, ambao umeelezwa kwenye hatua ya 5.