Rudi
A

Chagua njia shirikishi ya majaribio na utekelezaji

Muhtasari

Hizi ni mbinu shirikishi za masahihisho ya mbinu za makabiliano ambazo ni mpya na zisizofahamika sana na zinazoshirikisha wakulima moja kwa moja tangu mwanzo (k.m. mashamba ya majaribio na shamba darasa). Juu yake, kuna mbinu shirikishi za kufundisha wakulima ambaz zinawahusisha zaidi kwenye mchakato wa mafunzo na inawahamasisha kutekeleza ujuzi mpya (k.m. SD, viwanja vya majaribio, siku za shambani, mafunzo na matembezi).

Mbinu
  • Shule ya wakulima
  • Majaribio
  • Shamba darasa
  • Kutembeleana
  • Siku ya mkulima
Matokeo
  • Chagua mbinu za makabiliano zilizojaribiwa katika eneo lako
  • Mbinu inayofaa baada ya kujaribiwa ndiyo inayotekelezwa

Nadharia

Mbinu za ungani zinazotumika kwa uwingi zaidi ni zifwatazo:

  • Viwanja vya majaribio (utafiti) vinawezesha kujaribu mbinu la makabiliano ambalo halijasahihishwa kwa mazingira ya kienyeji kwenye mashamba halisi.
  • Shamba Darasa zinaruhusu fursa ya kujaribisha mbinu mpya ya kilimo, ufundishaji wa wakulima na kubadilishana ujuzi.
  • Mashamba ya mfano vinaonyesha mbinu bora za utekelezaji wa mbinu la makabiliano na matokeoyake mazuri.
  • Wakulima kutembeleana inasaidia kuchangiana mazoea na kubadilishana ujuzi kati ya wakulima
  • Siku za shambani zinasaidia kutoa fursa ya kujifunza kutoka kwa 'wakulima bingwa' ambao wamefanikiwa kutekeleza mbinu za makabiliano. Kwa kukutana shambani kwake, wakulima wengine wanaweza kujifunza kutokana na kuona mfano hai wa vitendo vizuri shambani.
  • Mafunzo na matembezi vinata fursa kwa maafisa ungani kuwafundisha wakulima vitendo maalum vya kilimo. Baada ya hapo, wakufunzi wanafwatilia kuhakikisha kuwa vitendo hivi vinatekelezwa shambani na kwa usahihi na wakulima mashambani kwao, na zinamsaidia mzalishaji kupata ushauri mwingine wa kiufundi atakayohitaji. Maafisa ungani wanakusanya maoni na mazoea ya wazalishaji, na wanaripoti juu ya mafanikio au changamoto.

I. Shamba Darasa

Shamba darasa (SD) ni kikundi cha wakulima (15 hadi 25) walio ya nia ya kutatua changamoto fulani ya uzalishaji. Hii inaendeshwa kwa njia shirikishi inayoboresha uwezo wa washirikiia kutambua matatizo na kutafuta ufumbuzi kwa kupitia majaribio. Kwa kufanya kazi kwa mapoja na maafisa ungani, wakulima wanatayarisha majaribio ya shambani yanayolinganisha mbinu ya makabiliano zinazowezekana na desturi zao za shambani. Lengo ni kuwasaidia kuelewa mchakato wa kilimo na ekolojia na kuwafanya wasimamie mifumo yao ya uzalishaji ili kufanikisha matokeo bora zaidi (angalia mfano kwenye Mafunzo Hai hapo chini).

  • Maangalizi, tathmini na uamuzi ni mchakato muhimu kwenye SD. Wakulima wanakusanya na kutathmini takwimu ili kufananisha utekelezaji wa mimea chini ya mifumo tofauti wa usimamizi, k.m. urefu wa mmea, idadi ya matunda, afya ya mmea, aina na uzito wa magugu, magonjwa na wadudu, unyevunyevu wa udongo, mavuno na nguvukazi. SD ni zaidi ya mafunzo, inatoa pia nafasi kwa wakulima kubadilishana matazamia na mazoea, pamoja na kuwasilisha taarifa mpya kutoka nje ya jamii.
  • Mtu aliye na utaalamu wa ufundi anatakiwa kuongoza kikundi kwa kuppitia mazoezi ya vitendo, na kujiweka kando punde kikundi kinapohisi kuwa kinaweza kufanya kazi peke yake. Mtu huyu anaweza kuwa afisa ungani au Aliyekamilisha mafunzo rasmi ya SD. Wahudhuria wa SD wanakutana katika mazingira yao ya kila siku, kwa mfano mashuleni, ukumbi wa jamii au shambani kwa mmojawao.

II. Mashamba ya majaribio

Kabla ya kuhamasisha matumizi ya mbinu mpya au mbinu ambalo halijajaribiwa kwa kupitia mashamba mifano na SD, inahitaji kutathminiwa kwa mazingira ambayo itatekelezwa. Kwa kupitia majaribio ya kiwango kidogo, maafisa ungani shambani na wakulima wanaweza kupata matokeo juu ya uwezekano na ufanisi wa mbinu lililopendekezwa.

Jaribio kawaida kufanywa kwa kuwango kidigo, k.m. idadi ndogo tu ya miti na eneo lililozuguka, kitalu kidogo cha miche ya kahawa, au ujenzi mdogo wa miundombinu (k.m. kikaushio cha kutumia mionzi ya jua). Kwa kila jaribio, mpango kazi na vigezo vya vipimo vinahitaji kupangwa. Ni muhimu kuzingatia uwezo wa maafisa ungani pamoja na rasilimali iliyopo ili kufafanua vigezo vinavyoweza kupimwa. Kuweka kumbukumbu za maangaizi, takwimu maalum juu ya shughuli mbalimbali, gharama na mavuno, na viashiria vya ufanisi (k.m. uhifadhi wa unyevunyevu wa udongo, uoto wa mizizi, upatikanaji wa virutubiso n.k.) ni shughuli muhimu sana ya jaribio kwa uzima. Rasilimali ya kutosha inahitajika kwa kuanzisha na kutunza kiwanja cha majaribio, na msaada wa muda wa maafisa ungani inahitajika pia.

Baada ya taarifa kukusanywa wakati wa majaribio, itahitaji kutathminiwa na matokeo kuwakilishwa kama kesi ya utafiti. Ongezea ushauri muhimu kwa majaribio mengine yatakayofanyika au kwa utekelezaji kwa kiwangokikubwa, pamoja na mafunzo muhimu yaliyotokea (angalia mfano wa Mafunzo Hai).

Baada ya kukamilisha awamu ya majaribio na mbinu za makabilaino yanaonyesha mafanikio, kiwanja bora zaidi kinaweza kutumika kama mfano wa utekelezaji unaostahili na athari kwa mmea, udongo na mavuno.

III. Mashamba ya mfano

Maafisa ungani watataka wakulima kurekebisha tabia zao za kilimo ili kuongeza ustahimilivu dhidi ya athari maalum za hali ya hewa (mf. Kutumia mazao ya matandazo ili kuitikia ukame). Mashamba mfano yanaweza kutumika kwenye baadhi ya viwanja ili kuruhusu wakulima wote kuangalia mbinu maalum za makabiliano wakati wa awamu tofauti za uoto na kujifunza mbinu bora.

Shamba mfano ni sehemu iliyokusudiwa kwa mbinu la makabiliano au ambapo mfano wowote mwingine wa kilimo unatekelezwa. Inaonyesha utekelezaji unaotakiwa wa mbinu la makabiliano na athari yake kwa mmea, udongo na mavuno. Shamba mfano linaweza kuwa dogo, k.m. miti michache na eneo la karibu, au linaweza kuwa shamba zima la kahawa. Mashamba mfano hutumika kama sehemu za mafunzo au kutembelea. Uzoefu umenyesha kuwa mashamba mfano yana ufanisi mkubwa kwani inawaruhusu wakulima kuona kwa macho yao wenewe matokeo mazuri ya mbinu bora kwenye mazingira yao. Ukianzisha shamba mfano ni muhimu kuzingatia kuwa baadhi ya vitendo vya kilimo vitazalisha matokeo baada ya muda fulani (k.m. miti ya kivuli, mazao ya kufunika udongo na matandazo).

Hakikisha umeweka kumbukumbu za shughuli, gharama, maoni ya wakulima na viashiria maalum vya ufanisi (k.m. usimamizi wa Churubuni, uhifadhi wa udongo au uhifadhi wa unyevunyevu kwenye udongo) na kuwasilisha taarifa hizi wakati wa matembezi na wazalishaji wengine.

Juu ya hayo, fedha za kutosha zinahitajika muhifadhi shamba mfano ili kutoa mfano bora- Kwa kawaida, hii ni uwezeshaji wa muda wa maafisa ungani. Kufadhili shamba mfano kwa kutumia fedha za nje ni uamuzi utakaohitaji kuatathminiwa kwa uangalifu kwaza, kwani hii inaweza kutilia mashaka swala la marudio ya mifano au kufaa kwa mbinu la makabiliano.

IV. Matembezi

Njia nyingine kwa wakulima na maafisa ungani kupata nafasi ya kuona mbinu za makabiliano zilizofanikiwa ni kwa wao kutembelea vituo vya utafiti, vinwanja vya majaribio vya wazalishaji waliofanikiwa ili waone kwa macho yao wenyewe. Kwa njia hii, wakulima wanajifunza kwa macho: Aina hii ya mafunzo kati ya mzalishaji mmoja na mwingine inaweza kuhamasishwa kwa kutumia mbinu za kubadilishana ujuzi kama kifaa cha muhimu kwenye kazi za ungani. tool.

Matembezi pia inajulikana kama “kutembelea mashamba' yanahitaji kupangwa kwa uangalifu na ni muhimu kwanza afisa ungani atembelee. Mashamba mfano yatakayochaguliwa lazima yawe yametekeleza mifano ya makabiliano ambayo yanaonekana wazi. Hakikisha umewakilisha mazoea, matazamizi, na athari nzuri na maunzo kwa wanaotembelea kwa njia inayoeleweka (angalia Umbo la 19).

Ni muhimu kuweka mkazo wa matembezi kwenye vipengele maalum na kutoa maelekezo kamili kwa kikundi kabla ya kuanza safari ya kwenda shambani. Hii inaweza kufanyika kwa kutoa orodha ya maswali kwa wanaohudhuria ya kujibu wakati wa matembezi (angalia mwongozo wa maswali hapo chini). Mwezeshaji awahamasishe wahudhuria kuchunguza shamba kwa kina, ama kwa kupitia majadiliano na wakulima wengine au kwa kuliangalia shamba kwa makini. Baada ya matembezi shambani, waulize wahudhuria kutoa maoni yao kwa kupitia majadiliano ya vikundi na kukubaliana jinsi ya kuwakilisha walichojifunza wenye mifumo yao ya kilimo.

Mwisho kabisa, wazalishaji wachochelewe kuiga mbinu zozote za makabiliano walizoona wakato wa matembezi shambani kwa kiwango kidogo, k.m. kwenye mashamba yao.

Mwongozo wa maswali wakati wa kutembelea shambani:

  • Aina gani ya ufundi wa kilimo alianzishwa kama mbinu la makabiliano dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi?
  • Nini zi hatua za utekelezaji? Nini imetekelezwa?
  • Ni mabadiliko gani uliyoyaona (k.m. mabadiliko ya udongo, miti ya kahawa, au mabadiliko mengineyo)?
  • Je, mbinu hii inafaa kwa mazingira yako?
  • Je, mbinu hii ni rahisi na inapatikana kwa wakulima wa eneo lako?
  • Nini imepungua na ingehtajika kwa wakulima ili waweze kutekeleza mbinu hii mashambai kwao?

Nini tofauti kati a mbinu za makabiliano na kanuni bora za kilimo?

Mbinu nyingi za makabiliano zinafahamika tayari kama kanuni za kilimo bora. Lakini kanuni za kilimo bora, kama vile kuweka matandazo, kinaweza kuwa mbinu lamakabiliano hapo itakapotumika dhidi ya athari fulani ya hali ya hewa kwa ukanda maalum, au dhidi ya udhaifu unaosababishwa na hali ya hewa. Ni pale tu panapokuwa na hatari ya kuathirika na mabadiliko ya tabia nchi, k.m. kama kuna athari au udhaifu kutokana na hali ya hewa ndipo mbinu ya utekelezaji inakuwa mbinu ya makabiliano, Hivyo, matandazo inaweza kufikiriwa kuwa mbinu la makabiliano na pia ni kanuni za kilimo boraa.

Mwongozo wa vitendo

Shamba Darasa

Shamba Darasa (SD) inahusisha makundi ya wakulima ambao wanatathmini matokeo, gharama na faida za teknlojia mbadala kwa kufanya majaribio shambani. Ni njia shirikishi ya huduma za ungani ambapo wakulima wanatumia ufumbuzi wao kufanya uamuzi juu ya mbinu za uzalishaji.

Lengo

  • Kujenga uwezo wa wakulima kwa kutumia mifano hai juu ya mifumo ya kilimo-msitu na kanuni za ikolojia, kama vile uhusiano kati ya maji na udongo, rutba na virutubisho, viumbe hai na uhifadhi wa unyevunyevu, n.k. Mkazanio unatakiwa uwekwe kwenye uzalishaji wa kahawa usioharibu mifumo ya kilimo-msitu.
  • Kuwasaidi wakulima kujifunza juu ya gharama na faida za teknolojia mbadala kwa kuendeleza na kuboresha uzalishaji wa shambani wa kukabiliana na mabadiliko na utofauti wa tabia nchi.
  • Kuwafundisha waklima juu ya mchakato wa mzunguko wa vitendo, tathmini na uamuzi (mbinu ya tathmini ya mfumo kilimo-msitu, AESA). Hii inawafundisha jinsi ya kutambua matatizo kwa kuangalia,kutathmini matatizo hay na kutambua sababu zake, na hapo fani hizi zikiwepo, kwa wao kufanya uamuzi wenyewe na hivyo kuwa na usimamizi bora wa mazao.
  • Kuongezea wakulima uwezo wa kufanya maamuzi kuhusu mbinu zinazowanufaisha – yaliyo na msingi wa maoni yao toka shambani – na kueleza sababu za mbinu zao. Ushauri unatakiwa ufae hai halisi ya sehemu maalum na uhusishe utaalam na mazoea ya sehemu hiyo, vitu ambavyo wakulimatu wanaweza kuchangia.
  • Kuongeza uwezo wa maafisa ugani wanaofanya kazi kwa ushirikiano na watafiti na kutoa huduma ya kuwezesha mafunzo kwa vitendo kwa wakulima. Wanawezesha mafunzo badala ya kuagiza ushauri wa ujumla ambao unatolewa kwa ukanda mzima, lakini haufai mazingira maalum.
  • Kuwafundisha maafisa ugani na watafiti jinsi ya kufanya kazi na wakulima kwenye kujaribu, kutathmini na kurekebisha aina tofauti za mbinu ili zifae maeneo yao maalum.
  • Kutoa mafunzo yenye msingi wa kujifunza kwa vitendo, ufumbuzi, malinganisho na uhusiano usiokuwa na mfumo wa msonge wa madaraka kati ya viongozi na wakufunzi, masomo yanayofanyika mashambani kwa kiasi kikubwa. uu Kufwata kanuni kuu tatu zifwatazo:
    • Zalisha zao lililo na afya nzuri
    • Kuangalia hali ya shamba mara kwa mara
    • Kuhifadhi adui wa wadudu waharibifu wa mazao uu Wakulima waelewe ikolojia na mabadiliko ya tabia nchi, na wawe wataalam kwenye mashamba yao

Utaratibu

  • Hatua ya I – Kuunda kikundi: uchaguzi wa jamii na motisha kwa wakulima kujiweka tayari uchaguliwa. Mahudhurio ni kwa kujitolea tu!
  • Hatua ya II -Ufafanuzi wa ufundi uliomo: Eleza sifa za mfumo wa kilimo hai. Tumia mtihani wa boksi33 pamoja na wahudhuria ili kutambua kiwango chao cha ujuzi juu ya mfumo wa kilimo-ikolojia wa kahawa, pmoja na udongo, virutubisho, waduu na usimamizi wa magonjwa, n.k.(yaani, tathmini ya hali halisi ya sasa). Fafanua kwa undani masomo ya mbinu la makabiliano kw kutumia mchakato wa c&c.
  • Hatua ya III - Kuanzisha uwanja wa mafunzo: Chagua mkulima atakayekaribish SD kwake. Panga na tekeleza viwanja maalum vya masomo kwa mbinu moja au mbii za makabiliano. Eleza malengo ya viwanja vya majaribio.
  • Hatua ya IV – Utayarishaji wa ufundi uliomo: Tayarisha mchakato wa mafunzo hatua kwa hatua, kwa kupitia madarasa ya mara kwa mara. Chunguza viwanja vya majaribio (mbinu za makabiliano) na kiwanja kitakachobaki bila kuchukuliwa hatua za makabiliano kwa vipimo na kuangalia. Tathmini matokeo. Hatimaye, rudia mtihani wa boksi ili kutambua ongezeko la ujuzi kwa wahudhuria.
  • Hatua ya V: Mahafali na ufwatiliaji wa wahudhuria.
Umbo la 38: Hatua za kuanzisha na kuendesha Shamba Darasa (SD)
mchoro unaoonyesha hatua za mradi.

Mbinu ya ugani ya Shamba darasa

  • Kikundi cha wakulima 25 hadi 30 wanaoathirika na walio na nia ya kutatua matatizo ya uzalishaji wa kahawa unaosababishwa na mabadiliko ya tabia nchi au udhaifu kutokana na vihatarishi vya tabia nchi, wanaunda SD.
  • Kwa kushiriakiana na maafisa ugani, wakulima wanapanga majaribio ya shambani (viwanja vya majaribio) ili ulinganisha mbinu na mashamba yao ya sasa (viwanja).
  • Wakulima wanamchagua mkulima atakayekuwa mwenyeji wao, pamoja na sehemu ya mafunzo. uu Wakulimwa wanakutana kwa mpangilio watakaokubaliana kulingana na mahitaji yao, k.m. umri wa zao na hatua za kukua (mikutano 8 hadi 12 kwa msimu).
  • Kwa vikundi vidogo vidogo,wakulima wanaangalia na kutathmini uhusiano kati ya mmea na mazingira yake. uu Wanapima na kunukuru vigezo vitakavyoleta mabadiliko kwenye maendeleo ya matibabu.
  • Kwenye vikundi vyao vidogo, wakulima wanatathmini takwimu, wananukuru tofauti kati ya maendeleo na sababu za tofauti hizi.
  • Wakulima wanafanya uamuzi wa usimamizi. Wanajiuliza, “Je, kama kitu hiki kinatokea kwa mimea yangu, nahitaji kufanya nini ili kukisimamia vizuri?”
  • Vikundi vinawasilisha matkeo ya uchunguzi wao kwa SD. uu SD linafikia makubaliano ya pamoja juu ya uamuzi upi wa usimamizi utekelezwe.
  • Takwimu za kukusanya na kutathminiwa na wakulima ili kulinganisha maendleo ya mazao yaliyo chini ya usimamizi tofauti, k.m.
    • Asilimia ya kuibuka, rangi ya majani, urefu wa mmea, idadi ya chipukizi, idadi ya matawi yanayotoa matunda, urefu wa jani, upana wa pinacle, aina tofauti za magugu na uzito, magonjwa na wadudu,au tija.
    • Faida kwa fesa iliyotumika kwenye teknolojia mbali mbali (tathmini ya ghanama na faida)
  • Hatimaye, tathmini ya matokeao wanafanyika kwa kufwata sifa za upimaji na ubora na matokeo yanapangwa na kusambazwa kwa wajumbe wengine wa jamii, na jamii nyingine na SD nyingine.

Msingi wa SD ni mtaala uliojaribiwa, ambao kwa kawaida unafwata mzunguko wa ukuaji wa mmea. Mwongozo wa shambani, mashamba ya majaribio, na mkusanyiko wa mazoezi ya elimumwendo inatoa msingi wa mtaala, ambao unakuwa ukijumuisha shughuli zote kwa kipindi cha mafunzo.

Ufundishaji wa SD inapitia matendo na ufumbuzi kwa kila mhudhuria. Shughuli zinapangwa kuhakikisha wahudhuria wanajifunza kwa kupitia vitendo hai, na kipindi kikubwa cha masomo kinafanyika shambani. Kubadilishana maoni, kuchangia mawazo na majadiliano kwa urefu yanawezesha mabadilishano ya taarifa na kuzalisha ujuzi.

Jiwe lamsingi la mbinu ya SD ni tathmini ya mfumo wa kilimo-misitu (AESA), ambao unawaruhusu wakulima kuangalia jinsi mmea unavyoingiliana na mifumo mingine iliyo hai na isiyo hai inayokuwepo sambamba shambani. Hii inamaanisha kuwa zao linafwatiliwa mara kwa mara shambani (kwa kahawa ni kawaida kupitia shambani kila siku 15 au mara moja kwa mwezi). Wahudhuria wanafanya kazi kwa vikundi vidogo vya watu wanne hadi watano, na wanajifunza jins ya kufanya uchunguzi wa kina, ikiwemo:

  • Hatua ya kukuwa kwa mmea
  • Wadudu, wadudu waharibifu na idadi itakayo leta manufaa
  • Magugu na kiwango cha magonjwa
  • Hali ya hewa
  • Hali ya udongo
  • Afya ya mmea kwa ujumla
Figure 39: An FFS produce compost for use on their farms, c&c pilot Vietnam
kikundi cha watu kimesimama kuzunguka rundo la udongo.

Wakulimma wanafanya maamuzi ya usimamizi kutokana na maoni yao na tathmini zao. Sehemu muhimu ya SD ni kuwasaidia na kuwahamasisha wakulima kufanya utafiti wao wenyewe na kujaribu mbinu mbali mbali za usimamizi wa mimea.

Hakuna ushauri wa ujumla au mbinu za kitekinolojia kwa ujumla, badala yake wakulima wanaamua pamoja mbinu gani au dhana zipi ya usimamizi wa mimea unafaa kufanyiwa utafiti, na wanafanya kila uamuzi kwa kutathmini matokeo yao wenyewe. Kwa kupitia mafunzo hai, wakulima wanachangia elimu yao na kuwa wafanya maamuzi walio huru.

Umbo la 40: Wakulima wanapima na kunukuru vigezo vinavyoleta mabadiliko kwa maendelea ya matibabu mbali mbali mradi wa c&c c ukanda wa Trifinio
kikundi cha watu kimesimama shambani wakitazama mimea.

Matokeo tarajiwa

  • Wakulima wanaweza kufanya uamuzi ulio na msingi wa ujuzi kamili juu ya makabiliano, ambayo inatokana na tathmini ya tekinolojia mbali mbali, kwa kila hatua ya mmea maalaum, kwa mfano huu ikiwa ni kahawa.
  • Wakulima walio ya utaalam wa mahitaji ya usimamizi kwa kila hatua ya ustawi wa mmea.
  • Ufanisi mashambani na uzalishaji mkubwa iwezekanavyo wa faida kupatikana kwa muda mfupi. Hii ni kutokana na juhudi za jumla na majaribio na wakulima, watafiti na maafisa ugani.