Rudi

Mpango wa hatua tano

logo1
Kuyafafanua mazingira
4
Masahihisho na utekelezaji wa mbinu za makabiliano
3
Kupanga makabiliano
2
Tathmini ya changamoto za mabadiliko ya tabia nchi
5
Somo la kujifunza na maendeleo ya hali uelewa
Tatizo
Suluhisho

Jilio la c&c ni mpango wa hatua tano ambazo zinawawezesha wakulima wa kahawa kuitikia mabadiliko ya tabia nchi kwa ufanisi kwa kufuata mpangilio wa kutathmini vihatarishi, pamoja na kutambua na kutekeleza mbinu za kukabiliana zitakazowafaa.

Kuyafafanua mazingira inaruhusu kuangalia kwa haraka umuhimu wa mabadiliko ya tabia nchi kwenye eneo maalumu la kazi.

Tathmini ya changamoto za mabadiliko ya tabia nchi inajenga uelewa juu ya athari za mabadiliko ya tabia nchi kwa uzalishaji wa kahawa na maisha ya wazalishaji, na inatambua mbinu zinazofaa kwa mwitikio wa ufanisi.

Kupanga makabiliano kuchagua mbinu kwa kuzingatia kipaumbele kwa mazingira husika na kupanga mchakato wa utekelezaji.

Masahihisho na utekelezaji wa mbinu za makabiliano inarihusu mbinu tofauti za kuwezesha kazi za utekelezaji na inasisitiza umuhimu wa kusahihisha au kujaribisha mbinu za makabiliano kwa vitendo kwa kiwango kidogo kabla ya kusambazwa.

Somo la kujifunza na maendeleo ya hali uelewa inaangalia mchakato wa utekelezaji kwenye hatua za ufuatiliaji, uthibiti na mafunzo. Hii ni muhimu sana kwa mchakato kukamilisha mzunguko mzima, kwani unatoa mafunzo na ushahidi unajenga msingi kwa maamuzi ya baadaye ya makabiliano. Pamoja na hii, hali ya hewa inaendelea kubadilika wakato wote, hivyo nguvu za makabiliano zinahitaji kutathiminiwa muda wote.

Sifa kuu za Mkakati wa c&c kwa muhtasari

  • Ujio wa mzunguko na wa hatua kwa hatua: Ujio wa c&c una hatua tano ambazo zimejipanga moja kufuata nyingine na hivyo kuruhusu utaratibu wa mpango wa utekelezaji.
  • Ni mahsusi kwa sehemu moja: hakuna sululisho la kuwafaa wote kwenye makabiliano dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi kwenye sekta ya kahawa. Hivyo, mkakati wa c&c unasaidia utambulisho wa sululisho zinazofaa hali za ndani (kijamii, kimazingira na kuchumi) na eneo mahsusi la kuzalisha kahawa.
  • Shirikishi: Mkakati wa c&c unashirikisha wadau na kaya za wakulima kwa kutambua matatizo ya eneo na utatuzi unaowezekana, na inasaidia kuanzisha vikundi vya wadau vya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.
  • Vitendo: Zana na nyenzo za mafunzo zimetayarishwa kwenye sanduku la Vitendeakazi vya c&c (c&c Toolbox).
  • Nyongeza: Mkakati wa c&c unafaa kutilia juu ya mafunzo mengine au kuongezea kwenye makabiliano mengine yaliyopo, na programu za kujenga uwezo.
  • Msingi wa kisayansi na mwelekeo wa shambani: Mkakati wa c&c unajumuisha sayansi ya mabadiliko ya tabia nchi na mbinu hakiki za kilimo pamoja na utaalamu wa ndani ili kufikia sululisho bora litakalowezekana. Inahimiza ushirikiano kati ya watafiti na wakulima shambani ili kupata matokeo yanayoweza kutekelezwa.
  • Mtandao wa Mafunzo: Mkakati wa c&c unajitahidi kuweka mtandao (wa ndani, wa ukanda na hata wa kimataifa) ambao utaruhusu kubadilishana kwa taarifa, mafunzo kwa vitendo na uzoefu wa jinsi ya kukabiliana dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi ili kuinua ujuzi wa hii sekta.

Maada

Uhamasishaji na ushikishwaji wa wadau: Mpango wa c&c unatekelezwa kwa kupitia nguvu moja ya wadau wa kahawa toka ngazi ya ndani hadi ngazi ya ukanda. Ushikisho wao ni muhimu sana hasa kwa hatua ya 2 hadi 5, wakati athari za mabadiliko ya tabia nchi inapotambuliwa, mbinu za makabiliano zinapofafanuliwa na maendelezo yanatathminiwa. Kuwashirikisha wadau wa ndani hausaidii tu kwenye utekelezaji wa mbinu za makabiliano, bali unasaidia pia uhamasishaji wa wahusika wa mada ya mabadiliko ya tabia nchi, na hivyo kuhamasisha hitaji la vitendo.

Mchakato na ufuatiliaji wa matokeo: ufuatiliaji kwa vitendo ni sehemu muhimu ya Hatua ya 3 hadi 5, na ni muhimu kwa kuelewa matokeo ya vitendo vilivyoamuliwa kwenye uzalishaji wa kahawa na maisha ya wazalishaji kwa muda mrefu. Pamoja na hili, ufuatiliaji unasaidia kutayarisha mafunzo ya makabiliano dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi.

Sanduku la Vitendeakazi vya c&c (c&c toolbox) inachukua nafasi ya kati ya Mkakati wa c&c. Ni mkusanyiko mpana wa nyenzo, ujuzi na uzoefu uliyopo kutoka kwa washiriki kwenye sekta ya kahawa ulimwengu mzima. Unatoa mwongozo juu ya utekelezaji wa hatua tano za Mkakti wa c&c , na ni malighaf kwa maafisa ugani na wengine wanaowasaidia wakulima kwa kutumia Mkakti wa c&c kwa kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

Sanduku la Vitendeakazi vya c&c

Sanduku la Vitendeakazi vya c&c umetengenezwa kuongezea mkakati wa c&c na kuwapatia watumizi taarifa na masomo ya kitaaamu juu ya ,mabadiliko ya tabia nchi, mifano ya mbinu maalumu za makabiliano inayoweza kutekelezwa, mifano hai, zana ya kupima faida, pamoja na nyenzo za kutolea mafundisho na zana nyingine za kuruhusu utekelezaji wa hatua tano za Mkakati wa c&c.

Sanduku la Vitendeakazi vya c&c ni jukwaa hai inayopitiliwa na kuongezewa mbinu mpya za makabiliano mara kwa mara. Inapatikana kwenye mtandao lakini taarifa zinapatikana pia kwenye ofisi maalumu katika nchi zinazotayarisha kahawa kama vile Brazil, Guatemala, Tanzania na Vietnam9. Wote wanohudhuria kwenye mtandao wa c&c wanahamasishwa wachangie mazoeao yao kwenye sanduku la vitendeakazi wakati wakufaidika pia kutokana na michango ya wenzao kupitia mkusanyiko wa ujuzi wa

c&c.Sanduku la Vitendeakazi vya c&c unatoa:

  • Maelezo ya msingi juu ya mabadiliko ya tabia nchi, k.m. athari za mabadiliko ya tabia nchi kwa uzalishaji wa kahawa au maandishi ya kisayansi juu ya kanda zitakazofaa kwa uzalishaji wa kahawa kwa miaka ya mbeleni (ramani za hali ya hewa).
  • Maelezo mafupi juu ya baadhi ya mbinu za makabiliano yanapatikana kwenye vitendeakazi vya c&c kwa kutumia toolbox wizard, ambayo ni mbinu ya kutafuta taarifa mtandaoni inayoonesha makundi ya madharajinsi ya hali ya hewa inanavyohatarisha uzalishaji wa kahawa, nchini na aina ya kahawa iliyolengwa na makabiliano maalum, na dhumuni kuu na aina ya mbinu inayofaa katika kukabiliana. Mifano kutokana na utekelezaji wa mbinu maalum za makabiliano pia zinaweza kupatikana kwenye sanduku la vitendeakazi.
  • Nyenzo kwa kila hatua tano za mkakati wa c&c, k.m. mwongozo wa mbinu ya pembetatu, au nyenzo za kutolea mafunzo ya kuhamasisha kaya za wakulima juu ya hiaja za mabadiliko ya tabia nchi na mipangilio ya semina za kuwahusisha wadau.

Sanduku la vitendeakazi pia liko nazana za aina mbalimbali za kusaidia utekelezaji wa hatua tano (angalia pia Umbo Na 4).

Sanduku la Vitendeakazi vya c&c linapatikana kwa wote na unaweza kupatikana pia kwenye jukwaa lake mtandaoni.

toolbox.coffeeandclimate.org