Kwenye kutathmini mahitaji ya makabiliano dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi kwenye ukanda husika wa uzalishaji wa kahawa, hatua ya kwanza kabisa ni kujenga ujuzi na uelewa wa msingi juu ya mabadiliko ya tabia nchi. Ukusanyaji wa taarifa juu ya jinsi tabia nchi inavyobadilika kwenye ukanda wako na jinsi gani inaweza kubadilika miaka ya mbele itakusaidia kugundua jinsi gani mabadiliko haya yanaweza kuathiri kilimo na uzalishaji wa kahawa.
Ni muhimu kutambua kuwa ujuzi juu ya mabadiliko ya tabia nchi na utofauti wa hali ya hewa zinaweza kuwepo kwenye jamii zinazozalisha kahawa. Kwa mfano, mazungumzo na wakulima na wadau wa ndani kuhusu ya maoni yao juu ya mabadiliko ya sasa ya tabia nchi yanaweza kuongezea ujuzi wa kisayansi. Hii ni muhimu, kwani ingawa takwimu za kisayansi hazipatikani kiurahisi, wakulima bado wanahitaji kuelewa vihatarishi vya hali ya hewa kwenye maeneo yao. Kwa kuzungumza na wakulima na wataalamu wa ndani, unajifunza pia juu ya dharura na hivyo hamasa ya kujihususha na makabiliano dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi.
Lakini kukusanya taarifa tu haitoshi. Hatua ya 1 ni pahala pa kufanya uchunguzi ili kujua ni nini haswa kitakachohitajika kwenye makabiliano kwenye mazingira yako. Baadhi ya maamuzi muhimu sana yanafanyika katika hatua hii, na inaweza kuathiri kwa kiwango kikubwa undani wa tathmini na umbo la kazi zinazojili. Kama hatua hii haijaangaliwa kwa makini, dhana mbovu zinaweza kufikiwa au njia zisizo sahihi zinaweza kuchukuliwa ambazo hapo baadaye zitabana uwezo wa kupanga utekelezaji.