
Kusanya taarifa juu ya uelewa wa tabili za hali ya hewa
Muhtasari
Ni muhimu kufahamiana na dhana za msingi za mabadiliko ya tabia nchi na istilahi zinazotumika (mabadiliko ya tabia nchi, utofauti wa tabia nchi, hatari za hali ya hewa, uathirikaji, uwezo wa makabiliano, utengamafu, n.k.) toka mwanzoni kabisa. Hii itakusaidia kuzitumia kwa ufanisi zaidi taarifa utakazozikusanya baadaye.
Sehemu ya 1 “Mabadiliko ya tabia nchi kwenye sekta ya kahawa” na sehemu ya 2 zinatoa taarifa za wali kwa kujibu masawali yafuatayo:
- Mabadiliko na utofauti wa tabia nchi ni nini?
- Nini kinasababisha dunia kupata joto na baadhi ya athari za mabadiliko ya tabia nchi ni zipi?
- athari zipi zinazoweza kutokea kwa zao la kahawa?
- Nini maana ya maneno makuu kama uathirikaji, utengamafu na uwezo wa makabiliano?
utafiti wa mezani na kwenye mtandao
Mapitio ya vipengele na tafsiri maalum za tabili za hali ya hewa
uwelewa juu ya matokeo ya kipindi cha nyuma, hivi sasa na kutabili mabadiliko ya hali ya hewa kwa mipaka mbali mbali, na madhara yanayoweza kutokea
Mwongozo wa vitendo
Lengo
Kupata dhana, mazoea na matazamio ya mabadiliko ya tabia nchi kwa sehemu maalum na athari zake kwa uzalishaji wa kahawa.
Matokeo tarajiwa
Tathmini juu ya umuhimu wa mabadiliko ya tabia nchi kwa jamii za ya kienyeji ya wazaishaji wa kahawa..
Muda unaohitajika
Wiki moja au mbili, inategemea upatikanaji wa maafisa ugani na idadi ya makundi maalum kwa majadiliano.
Mwongozo wa maswali
- Je, kumekuwa na mabadiliko ya jotoridi au mikondo ya mvua kwa miaka iliyopita (miaka 20 hadi 30)? Kama kumekuwa na mabadiliko ya tabia nchi ya kienyeji, hii imeathari vipi uzalishaji wa kahawa?
- Zipi ni changamoto kuu za uzalishaji? Je, yanahusiana na mabadiliko ya hali ya tabia nchi?
- Je, kumeuwa na mabadiliko ya tabia za kilimo ambayo pengine yanatokana na mabadiliko ya hali ya tabia nchi
- Je, umeshuhudia mabadiliko ya mazao kwenye miongo iliyopita?
- Unaonaje miaka ya mbele ya uzalishaji wa kahawa?
Utaratibu
- Hoji wakulima na wadau walio na miaka mingi ya mazoea ya hali ya tabia ya nchi na kilimo (zaidi ya miaka 20)
- Kazania mahojiano haya kwenye maswali makuu matatu hadi matano na nukuru majibu
- Kwa kupitia mahojiano na makundi maalum ya wakulima, chagua makundi madogo ya wakulima tano hadi kumi, hasa wenye historia ndefu ya uzalishaji kwenye eneo husika (k.m. zaidi ya miaka kumi). Ingekuwa bora zaidi kama wanakikundi watokee ukanda mmoja (ili wawe na uzoefu unaofanana wa hali ya hewa).
- Lengea mahojiano kwenye dhana na matazamio ya tabia nchi, lakini ruhusu muda pia kwa kufikiria maswala mengine yanayohusiana na mada ya mabadiliko ya tabia nchi. Kuwa mwangalifu kuwa si madhara yote waliyokumbana nayo yanahusika na mabadiliko ya tabia nchi.
- Unapozungumza na wakulima, ni muhimu kuzungumzia mabadiliko ya tabia nchi kwa uhumla badala ya kuzungumzia mabadiliko ya tabia nchi kwa mfululizo. Kwa mfano, jaribu kujadili jinsi gani misimu ya uzalishaji yamebadilika kulingana na shighuli za kilimo. Jarbu pia kuepuka maswali yanayobana majibu,k.m. “Mabadiliko ya tabia nchi ni tatizo kwa maeneo haya, au siyo?”. Utaratibu huu utakusaidia kuepuka wakulima kukuambia kile wanachofikiri ungependa kusikia, na itavutia majadiliano ya kufikiria zaidi juu ya mabadiliko ya mazingira kwa ujumla.
- Tathmini taarifa unazopata kutoka kwa wakulima na wadau (angalia Jedwali Na 21), lakini kumbuka kuwa si matatizo yote ya uzalishaji yanahusiana na mabadiliko ya tabia nchi.
- Kumbuka kuwa inawezekana kuwa wakulima wameshabuni njia zao za makabiliano wenyewe kama mwitikio wa hali ya kubadilika kwa tabia nchi. Tafuta dalili ya mbinu hizi za kilimo, kwani yanaweza kufaa kwa wengine kwenye ukanda huo.
Jedwali 20: Mfano wa matatizo yanayotokana na mabadiliko ya tabia nchi, Mradi wa c&c Tanzania
Zipi ni changamoto kuu kwenye uzalishaji | Mabadiliko gani yametokea ndani ya miaka 20 iliyopita? | Unaonaje kilimo cha kahawa kwa miaka ya mbele |
|
|
|
Tafhadhali zingatia kuwa ni changamoto zilizoandikwa kwa wino mzito ndizo zilitajwa na wakulima | ||