Eleza mipaka na weka malengo
Muhtasari
Mashirika mengi yanatumia muda mfupi mno kwenye kufafanua kiupana/ kiundani. Wanaona makabiliano kama swala la kiufundi ambalo linaweza kutatuliwa kwa ngazi ya mradi kama shughuli maalum itakayofanywa na shirika au washauri wa nje.
mikutano na wahusika maalum, wafanya biashara na vikundi na vyama husika
Uelewa juu ya majukumu na michango ya wadau toka jumuiya kuhusu shughuli dhidi ya tabili hewa
Nadharia
Mashirika mengi yanatumia muda mfupi mno kwenye kufafanua kiupana/ kiundani. Wanaona makabiliano kama swala la kiufundi ambalo linaweza kutatuliwa kwa ngazi ya mradi kama shughuli maalum itakayofanywa na shirika au washauri wa nje.
Bahati mbaya, mtazamo huu mara nyingi hautoshelezi. Ingawa tathmini ya athari ni mchakato halisi/mbaki kwa kiasi fulani, uamuzi juu ya makabiliano yanahitaji kuegemea kupangwa kwa sera ili kupata 'matokeo yanayotarajiwa' (tunakabiliana kwa ajili gani?) pamoja na vihatarishi na fursa 'halisi' (makabiliano yetu ni yapi?). Sehemu nyingi za mchakato ni za kifikra. Utahitajika kufikiria nini ni muhimu kwako na kwa wakulima unaofanya nao kazi, na hivyo kuipanga vitendo kwa kipaumbele.
Hatua zote kuanzia ya 1 hadi ya 3 ni muhimu kwa kupanga na kufafanua malengo yako. Wadau (hasa wakulima wadogowadogo) watakuwa na jukumu kubwa kufanikisha mchakato huu.Uamuzi juu ya makabiliano ni mchakato unaotegemea maadili, na hii inaifanya kutambuliwa, kueleweka na kuweka kumbukumbu ya dhana zote kuwa muhimu sana.Hatua Na 3 inatoa mwongozo wa jinsi ya kufanya hili.
Utakapoanza kupanga malengo yako ya makabiliano, zingatia yafuatayo:
- Kwa nini mabadiliko ya tabia nchi ni muhimu kwa mazingira yako?
- Nini ungeenda kufaidika nalo kutokana na makabiliano?
- Nani atafaidika na mchakato huu?
- Kuna yeyote atakayeathirika vibaya na malengo yako ya makabiliano
Kupanga utaratibu na wadau wengine (mamlaka, wafanyabiashara, vikundi maalumu na jumuiya, n.k.) kwenye ukanda wako ni muhimu. Wataarifu juu ya mchakato na malengo yake, na tathmini uwezekano wao wa kushiriki.
Angalia “Mwongozo: Kanuni za makabiliano mazuri” kwa uchunguzi wenye manufaa juu ya kufafanua kiupana na kupanga malengo yake, pamoja na vitendo vingine.
Mwongozo
- Fanya kazi kwa ushirikiano. Tambua na husisha jamii yako na hakikisha wanapata taarifa vizuri.
- Tatua hatari zinazohusika na mabadiliko ya tabia nchi ya leo kama sehemu ya kuanzia vitendo, ukiwa unazingatia hizi kutatulia hatari na fursa zinazosababishwa na mabadiliko ya tabia nchi ya muda mrefu zaidi.
- Tumia usimamizi wa makabiliano ili kukabiliana na hali ya kutokuwa na uhakika na tambua thamani ya makabiliano ya hatua kwa hatua.
- Tambua thamani ya kuishi bila ya kujutia au kuwa majuto kidogo, pamoja na makabiliano ya yenye manufaa kwa pande zote (mbinu zinazowezesha mafanikio ya ziada, au kuleta faida hata pasipokuwa na athari za mabadiliko ya tabinachi) kwa kuzingatia ufanisi wa matumizi ya fedha na mafanikio mengimengi.
- Epuka vitendo vitakavyobana wengine kufanya makabiliano au vitendo vya mwitikio.
- Pitia mara kwa mara maboresho ya mchakato ikiwemo pia kufuatilia na kutathmini vihatarishi.