Rudi
C

Kusanya taarifa toka kwa wakulima na wataalamu wa kahawa

Muhtasari

Wakulima na wataalamu wa ndani wa kahawa, au “wadau”, wanaweza kukupatia taarifa muhimu juu ya hali ya mabadiliko ya tabia nchi na athari zake kwa uzalishaji wa kahawa. Kubadilishana mawazo nao ili kujifunza juu ya hali ya wakulima ni mwanzo mzuri wa kuelewa jinsi gani athari za hali ya hewa zinavyosikika na watu wa ndani. Inaweza pia kukusaidia kuelewa umuhimu wa mabadiliko ya tabia nchi kwa ukanda wako maalum wa kahawa.

Mbinu

Mahojiano ya mtu mmoja mmoja na vikundi maalumu vya wakulima na wataalamu wa kahawa

Matokeo

Upembuzi wa awali wa mawazo na uzoefu juu ya madhara ya tabili za hali ya hewa katika eneo maalumu lakilimo cha kahawa

Nadharia

Mikutano ya vikundi maalum ni njia nzuri ya kuongezea majadiliano ya wakulima na wataalamu wa kahwa. Vikundi hivi vinaweza kutoa takwimu za maoni (yasiyo na yaliyo rasmi), dhana za mabadiliko ya tabia nchi, na taarifa juu ya shughuli zinazofanyika mashambani. Zingatia ni makundi gani ya watu yatakayohojiwa. Kwa mfano, wale walio na zaidi ya miaka 20 ya uzoefu wa hali ya hewa na kilimo cha maeneo husika wanaweza kutoa maoni tofauti na wale ambao hawajafanya kazi maeneo hayo kwa muda mrefu. Ni muhimu kukumbuka kuwa hii isiwe mwingiliano pekee kati yako na wakulima wakati wa mfumo wa c&c, na kuwa itawezekana kuiangalia mada hizi kwa ukina zaidi kwenye hatua nyingine.

Kazania mahojiano au majadiliano na makundi kwa kufuata si zaidi ya maswali matano, kama hivyo yafwatayo:

Umbo la 5: Tazama majedwali tofauti tofauti
kundi la wanaume linasimama katika shamba la mimea .

Mwasali ya Mwongozo:

Je, kumekuwa na utofauti wowote wa misimu ya joto au mvua ndani ya miaka 20 hadi 30 iliyopita?

Nini ni ushahidi wa hii (masimulizi ya watu yanatosheleza)?

Je, kwa miaka ya nyuma imetokea hali ya hewa iliyokithiri?

Ni matukio yapi na kwa muda gani?

Kumekuwa na mabadiliko ya hali ya hewa ya sehemu maalum (microclimate)? Kama ndiyo, hii imeathiri vipi uzalishaji wa kahawa hapo?

Je, kumekuwa na mabadiliko wa tabia za kilimo, isitoshe kulingana na mabadiliko ya hali ya hewa?

Je, ungependa kufahamu zaidi juu ya changamoto za mabailiko na utofauti wa tabia nchi, na pia njia zilizopo za mwitikio?

Elekeza majadiliano kuelekea dhana na uchunguzi wa hali ya hewa, lakini ruhusu pia uvumbuzi wa mada nyingine kama ikihitajika. Huu ni utangulizi tu wa dhana zilizopo, unyeti na uelewa wa mabadiliko ya tabia nchi. Kumbuka kuwa si mabadiliko yote watakayoyahisi yanatokana na mabadiliko ya tabia nchi. Ni muhimu kutathmini vizuri taarifa yoyote inayokusanywa ili kuandaa tathmini kiuhakika ya umuhimu wa swala hili kwa jamii ya wazalishaji wa kahawa.