Tathmini ya changamoto za mabadiliko ya tabia nchi
Utangulizi
Hatua ya 2 ni hatua ya msingi kwenye mchakato wa c&c. Ni kwenye hatua hii utakapojifunza juu ya mabadiliko ya tabia nchi na kutathmini vihatarishi vya sasa vya hali ya hewa na athari zake shambani. Inakuhitaji uunganishe dalili za kisayansi na uzoefu na utaalamu wa ndani ili kujenga uelewa wa kina juu ya athari za mabadiliko ya tabia nchi na mahitaji ya makabiliano. Kwenye hatua hii wakulima wa kahawa na wadau wanaanza mchakato husushi wa kugundua na kujifunza juu ya makabiliano dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi na uhusiano wake na tabia za kilimo. Hii inategemea uelewa wa mwanzo uliojengeka kwenye Hatua ya 1.
Malengo
Kutathmini vihatarishi vinavyosababishwa na mabadiliko ya tabia nchi na athari za sehemu husika kwa uzalishaji wa kahawa na kwa maisha ya wakulima wa kahawa.
Kutambua mbinu za makabiliano zinazowezekana
Maswali ya Mwongozo
Mabadiliko ya tabia nchi yanaathiri vipi uzalishaji wa kahawa?
Nitapata wapi taarifa husika kutoka vyanzo mbalimbali?
Ni wadau gani niwatafute kwa ajili ya kukusanya taarifa
Nitatathmini vipi taarifa nitakazopata kutoka vyanzo tofauti?
Zipi ni mbinu za makabiliano zinazowezekana? Wapi nitaweza kupata taarifa juu ya mbinu hizi?
Muda Unaohitajika
Miezi miwili hadi mitatu
Nini kinafanyika kwenye hatua ya 2?
Tathmini hii ya vihatarishi inajibu maswali makuu mawili:
Ni jinsi gani mabadiliko ya tabia nchi yanaathiri uzalishaji wa kahawa, wakulima wa kahawa na familia zao kwenye maeneo yao maalumu?
Nini tunaweza kufanya mashambani ili kufanya mifumo ya uzalishaji wa kahawa kuwa tengamafu zaidi?
Kumbuka kuwa mkazo hapa uko kwenye ngazi ya shamba. Hii haimaanishi kuwa maswala ya mazingira yote kwa ujumla si muhimu (taarifa juu ya hayo zikusanywe popote panapowezekana), bali ni kwamba, athari za hali ya hewa kwenye mashamba ni kipaumbele cha kwanza.
Hatua ya 2 ina tathmini ya vihatarishi vya muda mfupi na muda mrefu vya mabadiliko ya tabia nchi, ambayo inafanywa kwa uchunguzi wa mezani (yaani, siyo shambani) na majadiliano na wahusika. Kwenye uchunguzi wa mezani , angalia taarifa za kisayansi na takwimu zinazopatikana, pamoja na taarifa husika kuhusu makabiliano dhidi ya tabia nchi kwenye sekta ya kahawa. Hii inahitaji kulinganishwa na dhana, matazamo na ujuzi utakaopatikana kutokana na mahojiano na mikutano na wakulima wa kahawa na wataalamu wa ndani, au 'wadau' (watafiti, waajiriwa wa makampuni binafsi, maafisa ugani kutoka taasisi za kahawa za kitaifa, na mashirika yasiyo ya kiserikali, n.k.).
Ili kukusanya taarifa kutoka vyanzo vyote, unaweza kutumia mbinu ya pandetatu (triangulation methodology) (Umbo Na 6 na Jedwali Na 6). Hii inamaanisha kukusanya taarifa kutoka kwa vyanzo tofauti, zikiwemo takwimu za vipimo na za maelezo kutoka kwa wakulima, vikundi maalum na sayansi, na kutambua zinapofanana na zinapotofautiana.
Wakulima ni chanzo muhimu cha taarifa kwani wanafahamu zaidi kushinda wote hali ya kilimo ya pale na changamoto zilizopo. Watakuwa na ufahamu mzuri juu ya jinsi hali ya hewa inavyobadilika na athari za mabadiliko haya kwa uzalishaji. Juu ya hayo, inawezekana kuwa wameshaanza kubadilisha mifumo yao ya uzalishaji ili kuitikia athari hizi. Hata kama ufundi wa makabiliano hauleti ufanisi, unaonyesha kuwa kuna tatizo ambalo wakulima wanajaribu kutatua.
Wataalamu wa ndani – mara nyingi hawa ni maafisa ugani, lakini pia wanunzi na madau wengine – wana ujuzi mpana na uzoefu wa hali ya sehemu fulani na matatizo yanayotokea kwa kilimo cha kahawa, na wanaweza kutoa taarifa muhimu juu ya mbinu za makabiliano. Inawezekana pia kuwa wameona mbinu za makabiliano zilizofanikiwa sehemu nyingine.
Kupitia utafiti wa kisayansi uliopo na taarifa zilizopo ili kuongezea juu ya vyanzo vilivyotajwa katika Hatua ya 1. Hii inaweza ikawa maoni ya hali ya hewa (mwelekeo wa takwimu za vipindi vya nyuma, k.m. joto ya juu kwa siku kipindi cha maua kuchana) na makadirio (mabadiliko ya hali ya hewa kwa miaka ijayo). Angalia pia historia ya hatari kutokana na hali ya hewa na athari zake (k.m. nini kilitokea shambani wakati wa kipindi cha ukame uliopita?). Tathmini takwimu hizi za kisayansi sambamba na majibu toka kwa mahojiano na wakulima na wadau. Mabadilishano ya mawazo na waajiriwa wa taasisi za utafiti nazo pia zitasaidia.
Kuifanyia kazi maada ya mabadiliko ya tabia nchi inamaanisha kufanya kazi kwenye mazingira yasiyokuwa na uhakika. Kuna upungufu wa dalili zilizopimwa na umbo zima la muundo wa hali ya hewa kwa miaka ijayo haufahamiki. Hivyo, taarifa zozote zinazofanana kati ya vyanzo vyake tofauti utatoa mtazamo unaowezekana zaidi juu ya athari za hali ya hewa na kuzalisha baadhi ya mbinu za awali za makabiliano.
Panga maoni yote utakayopata kupitia mchakato wa pembetatu ili kutayarisha ripoti itakayotoa maelezo juu ya hatari za hali ya hewa, ahari na orodha ya awali ya mbinu za makabiliano yanayowezekana.
Umbo la 7: Mbinu ya pembetatu
Matokeo ya Hatua ya 2
Baada ya kupitia hatua hii, utapata yafuatayo:
Tathmini ya vihatarishi kutokana na hali ya hewa kwa uzalishaji wa kahawa na maisha ya wakulima wa kahawa
Mpangilio wa kiupaumbele wa mahitaji ya makabiliano
Orodha ya mbinu za makabiliano yanayowezekana
Kulingana na rasilimali fedha zinazopatikana na mahitaji ya ndani, hii inaweza kuonyeshwa kwenye jedwali kamili au ripoti ya ukina.
Juu yake, machakato mzima wa ukusanyaji wa takwimu, wadau na wakulima wa ukandani wanahitaji kuelemishwa juu ya maswala ya mabadiliko ya tabia nchi ili waweze kuwa sehemu mojawapo ya kazi za makabiliano tangu mwanzo. Hii inajenga umilikaji na kuongeza uwezo wa matumizi na uhusiano wa hatua za makabiliano zitakazotolewa.
Majukumu ya hatua 2
A
Tambua wadau husika
Mbinu
ramani ya wadau (utambuzi, udadisi, michoro na upangaji wa kipaumbele way wadau wote muhimu)
Matokeo
Orodha ya wadau muhimu kwa ajili ya mikutano ya kwanza na mahojiano;
ramani ya wadau pamoja na taarifa juu ya ushirikiano wao kwenye shughui za c&c (hatua 2 hadi 5)