Tambua wadau husika
Muhtasari
Utambulizi na ushirikishi wa wahusika maalumu kutoka kwenye jamii, au 'wadau', ni ufunguo wa mchakato mzima wa makailiano.
ramani ya wadau (utambuzi, udadisi, michoro na upangaji wa kipaumbele way wadau wote muhimu)
- Orodha ya wadau muhimu kwa ajili ya mikutano ya kwanza na mahojiano;
- ramani ya wadau pamoja na taarifa juu ya ushirikiano wao kwenye shughui za c&c (hatua 2 hadi 5)
Nadharia
Maswali muhimu kwa ramani ya wadau:
- Ni mashirika yapi (ya serikali au zisizo za serikali) zinahusika na kutatua maswala ya mabadiliko ya ya hali ya hewa na kahawa?
- Zipi ni sera au mikakati itakayoongoza kazi zao?
- Ni shughuli zipi wanazozitekeleza kwa sasa zinazogusia makabiliano?
- Ni mashirika yapi na taasisi zipi zilizo na mamlaka ya kutatua maswala ya mabadiliko ya tabia nchi? Wana uwezo gani wa kushawishi makabiliano?
- Wana uhusiano gani na mashirika mengine?
- Zipi ni nguvu zao na upungufu wao, k.m. je kuna ukosefu wa uwazi juu ya wajibu? Wapi kuna upungufu wa ujuzi?
Majibu ya maswali haya yataamua shughuli zozote za mashauriano na wadau.
Utata wa makabiliano dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi inamaanisha kuwa mara nyingi, kuna baadhi ya michakato mbalimbali inayoweza kufanyika. Wadau wanaweza kuwa na jukumu muhimu la kusaidia kutambua na kusaidia hatua za makabiliano kwa sehemu fulani na kutoa taarifa juu ya jinsi kuwasaidia wakulima kusimimia hatari za hali ya hewa. Wanaweza pia kutoa taarifa juu ya mazingira ya kiuchumi na kijamii ili kuepukana na mbinu mbovu za makabiliano. Kwa kuzingatia maoni mengi tofauti kunaweza kuongezea uwezekano wa kukubalika kwa hatua zinazoshauriwa, na kuhakikisha ufanisi unakuwepo.
Jedwali 6: Ramani ya Wadau – Mfano wa orodha ya makundi husika, taasisi na watu wanaoweza kushirikishwa kwenye Mkakati wa Kahawa na Tabia Nchi
Wadau | Malengo | Uhusiano unaoweza kujitokeza |
Watoa huduma: msaada wa kitaalamu (taasisi za umma/ binafsi) | Kutoa mafunzo/ kupata taarifa | taarifaza kisayansi, ujuzi na utalamu |
Taasisi za zilizozibitishwa: msaada wa kitaalamu | Kutoa mafunzo/ kupata taarifa | Shughuli za majaribio na usambazaji |
Taasisi za wazalishaji | msaada wa kitaalamu shambani | Pilot activities and scaling up |
Bodi ya Kahawa | Kutoa na kuboresha utafiti, mafunzo, mipango | taarifa za kisayansi, mafunzo, kujenga uwezo |
Wizara ya Kilimo na/ au ya Mazingira | Kuhakiki ubora wa utafiti, mafunzo, mipango | taarifa za kisayansi, mafunzo, kujenga uwezo |
Wanunuzi wakubwa wa kahawa | Kutoa mikopo | Fedha, mafunzo (hasa udadisi wa vihatarishi) |
Benki za Mikopo vijijini | Kutoa mikopo | Fedha, mafunzo (hasa udadisi wa vihatarishi) |
Taasisi za Maendeleo | nyingi | nyingi |
Nini maana ya utambuzi wa wadau?
ni mchakato shirikishi wa utafiti na majadiliano ambayo yanaazimia kupata maoni tofauti ili kubaini orodha ya msingi ya wadau kutoka nyanja tofauti tofauti.
Utambuzi unaweza kugawanywa kwenye awamu nne:
- Kubainisha: kuorodhesha makundi, mashirika na watu husika
- Tathmini: kuelewa maoni na maslahi ya wadau
- Utambuzi: tambua uhusiano kati ya malengo na wadau wengine
- Kuweka kipaumbele: kuorodhesha wadau kulingana na umuhimu wao na kutambua maswala
Mchakato wa kuwatambua wadau ni muhimu kulingana na matokeo yatakayopatikana, na ubora wa mchakato unategemea sana ujuzi wa wanaoshiriki. Hatua za kwanza kwenye utayarisahji wa ramani ni kuelewa kuwa hakuna orodha iliyokwisha kaa tayari na kwa kipekee. Orodha ya mwisho itagemea mazingira maalumu ya sehemu ya kazi pamoja na malengo ya sasa ya shughuli. Hivyo, orodha itakuwa inayopitiliwa mara kwa mara kulingana hali halisi.
Punde orodha ya wadau ikitambuliwa, tathimini ya nyongeza itakusaidia kuelewa zaidi umuhimu wao, mtazamo wao na uhusiano wao na maswala husika. Wapange kwa kuzingatia kipaumbele kwa kufuata mwongozo huu:
Orodha ya vigezo vya kutathmini wadau
- Mchango: Je, mdau ana taarifa, ushauri, au utaalamu juu ya maswala ambayo yatakuwa muhimu kwa kufikia malengo?
- Uhalali: Je, madai ya mdau kujishughulisha yana uhalali wa kiasi gani?
- Utayari wa kujushughulisha: Je, utayari wa mdau kujishughulisha ni wa kiasi gani?
- Ushawishi: Je, mdau ana kiwango gani cha ushawishi?
- Haja ya kuhusishwa: Je, huyu ni mtu anayeweza kupotosha au kukatisha mchakato kama hajahusishwa?
Haisaidii, na mara nyingi si lazima kuwahusisha wadau wote kwa kiwango kinachofanana, kwa wakati wote. Kufanya uamuzi juu ya nani kumhusisha na kwa sababu gani kabla ya kuanza machakato itakuokolea muda na hela. Pia ni muhimu kusimamia mategemeo ya wadau; kuhuska kwao si dhamana kuwa maoni yao yatapendwa zaidi ya maoni ya wengine.
Mbinu za tathmini ya wadau
Lengo: Kuelewa uhusiano na tofauti ya madaraka kati ya wadau mbalimbali.
Matokeo tarajiwa: ramani inayoonesha wadau tofauti na uhusiano kati yao (angalia mfano hapo chini)
Muda unaohitajika: Saa moja hadi tatu.
Utaraibu
- Mchoro wa Venn ni dhana iliyo rahisi kutumia inayosaidia wahudhurua kupeleleza na kukosoa hali halisi ya sasa, na wakati huo huo kushauri mbinu za kuboresha kwa kujenga uhusiano na kuunganisha watu.
- Inaweza kutumika kwenye vikundi ili kuanzisha majadiliano.
- Waombe wahudhuria wachague madwara ya ukubwa mbali mbali (k.m.ndogo, ya wastani na kubwa) ili kuwasilisha wadau wa mazingira yao. Ukubwa wa dwara unawakilisha umuhimu wao kwa mradi; duara likiwa kubwa zaidi, nao umuhimu wa mdau ni mkubwa.
- Kisha, madwara haya yanapangwa kulingana na duara la katikati ambalo linawakilisha mradi (au programu) unaotekelezwa. Kiwango cha nguvu ya mdau juu ya mradi kinawakilishwa na umbali kati ya dwara lake na dwara la katikati. Nguvu inahusiana na madaraka na mamlaka juu ya maamuzi, ikiwemo pia jinsi yanavyofanyika na jinsi gani yanayo (au yatakavyo) tekelezwa. Umbali kati ya madwara yanoyowakilisha wadau inamaanisha kiwngo cha mgusano na ushirikiano kati yao.Palipo na mgusano mdogo kati ya wadau, madwara yanatakiwa yawekwe mbali mbali, na pale palipo na mgusano wa karibu na ushirikiano, madwara yawekwe kandokando.
- Tbaada ya kikundi kutayarisha ramani, itumike kwenye kuanzisha majadiliano juu ya mdau yupi anaonekana kuwa anahusika na anapaswa ashirikishwe kwa hatua mbali mbali. Pia itumike kunukuru wapi kunaweza kuwa na mgogoro na jinsi gani kutatua.

II. Matriki ya taathiri na umuhimu
Lengo: Matriki ni njia nyingine ya kuwasaidia washiriki kufikiria juu ya nani anayeweza kuwa na mtazamo au uzoefu wa kuchangia, na nani ataathirika na, au kuiathiri, mchakato wa makabiliano. Inaweza pia kuweka wazi ni nani akikosekana basi itamaanisha kuwa taarifa za muhimu zitakosekana, na njia ya kuwavutia kushiri.
Matokeo tarajiwa: Ramani inayoonyesha madaraka ya wadau tofauti
Muda unaohitajika: Ushirikishi wa wadau unafanyika sambamba na hatua zingine, inayomaanisha kuwa hakuna muda maalum unaowekwa kando kwa shughuli hii.
Utaraibu:
Tambua wadau walio muhimu:
- Hawa ni watu walio muhimu sana kwa mafanikio ya mradi au programu ya makabiliano ya tabia nchi; watu ambao matatizo, mahitaji, matakwa na uwezo wao yanahusiana moja kwa moja na mradi. Usipowahusishawatu hawa, mradi hautaweza kufikiriwa kuwa umefanikiwa.
- Maswali yafwatayo yatahitajika ili kutambua wadau muhimu:
- Je, wana mahitaji au matatizo yanayohusiana na pradi? Wataathirika na matokeo yake?
- Je, wana taarifa unazohitaji?
- Je, wanajali mahitaji ya watu watakaoathirika na matokeo?
- Je, wana mahitaji yanayoweza kupingana na mradi?
Tambua wadau walio na nguvu::
- Hawa ni watu walio na nguvu ya kuathiri mradi au programu. Kwa mfano, wanaweza kuwa watu wanaofanya maamuzi muhimu, walio na madaraka juu ya maamuzi yatakayofanyika au wa madaraka mengine yatakayoathiri uamuzi unaofanyika, k.m. kwa kuwalazimisha au kuwashawishi wengine.
- Mwongoo wa maswali kwa kutambua wadau walio na taathiri:
- Je, wanasimamia maamuzi juu ya mradi?
- Je, wana madaraka juu ya mradi?
- Je, wana uhusiano na watu muhimu (k.m.na wanasiasa au wanaoshika fedha)?
- Je, wana madaraka juu ya maamuzi ya matumizi ya fedha au uwezo wa kupata ufadhili zaidi?
- Je, wanaheshimika katika jamii (k.m. madaraka ya kisiasa au kidini)?
- Je, wanaweza kuathiri jina la mradi?
- Je, wana madaraka, ama rasmi au kienyeji (k.m. ya tabia njema, ya kisiasa, au kijamii)?
- Wakilisha madaraka haya kwa kutumia mchoro wa ramani ya wadau mbali mbali.

