Dadisi na fupisha taarifa
Muhtasari
Pune ukimaliza kuzipanga taarifa kutoka kwa wakulima, wadau na sayanzi, unahitaji kuzitathmini na kutambua wapi zinapofanana na zinapotofautiana. Kama vyanzo vyote vitatu vinafanana na matokeo, basi inaweza kutambuika kuwa ya kuaminika, na hivyo kuwa msingi mzuri wa kutafutia mbinu za makabiliano. Kama kuna utofauti miongoni mwa vyanzo vitatu, tathmini na uchunguzi zaidi zitahitajika. Tayarisha taarifa hizo kama nakala ya awali ambayo inakupa muhtasari mzuri wa matokeo kutoka vyanzo vyote vitatu, ambayo inaweza kujadiliw na wahusika wote.
mkutano kati ya waajiriwa na wadau: kuhakiki
- udadisi wa matokeo toka vyanzo vitatu vya taarifa
- udadisi wa vitishio kwa kilimo cha kahawa na wakulima
- orodha ya mbinu mbali mbali ya makabiliano
Nadharia
Pia ni vizuri kufupisha na kuorodhesha matatizo ya hali ya hewa (ikiwemo athari, madhara na sababu za kudhuriwa), pamoja na ufumbuzi unaowezekana, kwenye jedwali 14, angalia hapo chini. Utegemeana na lahitaji yako, inaweza kukusaidia kuandika ripoti ya muhtasari kwa kina. Mifano ya ripoti za muhtasari ya kina za uchunguzi wa changamoto za wakulima zinawezekana kupatikana katika sanduku la Vitendeakazi vya c&c (c&c toolbox).


Pia ni muhimu kufupisha na kuorodhesha matatizo ya hali ya hewa (ikiwemo hatari, athari na sababu za udhaifu), pamoja na suluhisho zinazowezekana katika jedwali lililopangwa kwa muundo maalum14, tazama hapa chini. Kulingana na mahitaji yako, inaweza kuwa muhimu kuandika ripoti ya muhtasari iliyo ya kina.
Jedwali 8: Mfano wa orodha ya madhara na utambulizi wa makabiliano
Kitishio | Mvua kali | Joto kuongezeka |
Athari (Tatizo) |
|
|
Sababu | Udongo kwenye milima haujalindwa (madawa ya magugu, hakuna kivuli) | kutokuwa na ujuzi juu ya Mbinu mbadala wa kinga dhidi ya CBB |
Chanzo cha taarifa |
|
|
Orodha ya athari na/ au Athari | Wakulima: Juu (3) Wadau: Wastani (2) Sayansi: Chini (1) | Wakulima: Wastani (2) Wadau: Wastani (2) Sayansi: Juu (3) |
Kipaumbele ya tatizo | Juu (3) | Wastani (2) |
Baadhi ya Chagu za Makabiliano |
|
|
Mwongozo wa vitendo
Lengo
- Kufananisha taarifa juu ya mabadiliko ya sasa ya tabia nchi kutokana na vyanzo vya kitaalam na taarifa toka kwa wadau ili kutambua kama athari za vihatarishi vya tabia nchi zinafanana.
- Kutambua na kuwekea kipaumbele vihatarishi vya tabia nchi na athari kwa uzalishaji wa kahawa kwa sehemu husika.
- Kutambua mbinu zinazowezekana za makabiliano.
Mwongozo wa maswali kwa kutathmini athari za mabadiliko ya tabia nchi na kutambua mbinu za makabiliano
- Ni pande gani za tabia nchi zinaathiri wakulima zaidi (k.m. athari za moja kwa moja kama vile jootoridi za juu au ukame, au athari za embeni lama vile magonjwa mengi yanayosababishwa na hali ya hewa isiyo kawaida)?
- Je, taarifa juu ya utofauti wa tabia nchi kwa miaka iliyopita au hali ya hewa iliyokidhiri zinaonyesha udhaifu dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi? uu Je, kuna uwiano kati ya kile wanachosema wakulima, maafisa ugani na sayansi juu ya maswala yanayohuska na tabia nchi?
- Nani anaathirika zaidi na utofauti wa tabia nchi (fikiria majukumu tofauti kati ya wanaume na wanawake)? uu Je, ni matatizo gani mengine yanawakumba wakulima (k.m. kupunguza usimamizi wa uzalishaji wa kahawa ili kuwekea nguvu kwenye kutatua matatizo yanayoathiri mazao ya chakula)?
- Ni kwa njia gani mabadiliko mbele ya tabia nchi yataathiri maamuzi na umuhimu wa kuyafanya (k.m. je ukanda wako umekaribia kwa kiasi gani viwango vya juu kabisa vya jotoridi, ambavyo ni hatari)?
- Kw kufwatilia mchakato wa pembetatu, je mradi huu utazingatia zaidi mwitikio wa hivi sasa dhidi ya tatizo maalum, au unaona mwitikio wa ujumla dhidi ya mabadiliko ya muda mrefu?
- Kama wakulima wameshaanza kujaribu mbinu za makabiliano, je inawezekana kwa hatua hii hutathmini ufanisi wa mbinu hizo?
I. Vihatarishi vya tabia nchi na kuwekea athari orodha ya ushindi
Lengo
Kutathmini mabadiliko ya tabia nchi na kutambua vihatarishi vya tabia nchi na vifaa vya kukabiliana na athari ili kupunguza athari zinazowezekana.
Matokeo tarajiwa
Tathmini ya vihatarishi vya tabia nchi na athari zinazoendana nazo kwa uzalishaji wa kahawa.
Utaratibu
- unganisha na panga taarifa ulizozikusanya kutoka kwa wakulima, wadau na sayansi. uu Tayarisha muhtasari. Itakusaidia ukizipanga taarifa zote kwenye Jedwali. Hakikisha unazingatia kama na jinsi gani athari zinawakabili wanaume na wanawake.
- Upangaji wa vihatarishi kwa orodha ya ushindi itakusaidia kuwekea kiaumbele maswala yanayohitaji kuchukuliwa hatua za makabiliano. (Angalia Jedwali la 26).
- Upangaji wa vihatarishi kwa orodha ya ushindi unaweza kutokana na kutamkwa kwa uwingi na wakulima au mfumo wa maafisa ugani kupiga kura kwenye semina. Ikiwezekana, taarifa za kisayansi zipatikane kutoka takwimu za tabia nchi za sehemu maalum, lakini kawaida hii ni vigumu kupata. Kwa mfano wa hpo juu, hi haitahitajika kwani kuna makubaiano kwa ujumla kuwa mvua inaanza kuwa nzito zaidi. Pale ambapo taarifa na takwimu juu ya jambo hili hazipatikani, pata ushauri kutoka kwa mtaalamu wa hali ya hewa au mtaalam mwingine anayehusika.
- Wekea kipaumbele matatizo makuu kwa kuhesabu maksi kutoka kwa wakulima na aafisa ungani waliotoa maksi za juu. Kipaumbele kabisa itaamuliwa na kikundi cha shambani, mara nyingi ni wazi kabisa toka mwanzoni matatizo makuu ni yapi. Kama kuna mgongamano wowote kati ya vyanzo vya taarifa, itawezekana kuwa wakulima na maafisa ugani watahitaji kujadili zaidi. Pakiwa na mashaka, kawaida wakulima ndio watakaokuwa na uamuzi wa mwisho.
II. Utambulizi wa sululisho za makabiliano yanayowezekana
Lengo
- Kutambua mbinu za makabiliano kwa kupunguza athari zilizopo za tabia nchi
- Kuwahusisha na kuwashirikisha wadau wa sehemu maalum
- Kuhamasisha wakulima na kufikiria matokeo ya tathmini.
Matokeo tarajiwa
Orodha fupi ya mbinu zilizopo za makabiliano zitakazotumika kutayarisha mpango wa utekelezaji (Hatua ya 3) na kwa ajili ya masahihisho na/au utekelezaji (Hatua ya 4).
Utaratibu
- Ni wazo zuri kutambua kwanza mbinu nyingi iwezekanavyo (angalia “Kupata chagu ya makabiliano” hapo chini). Mara nyingine, vifaa vilivyopo vinaweza visisaidie sana lakini hatimaye vinakuwa ni mbinu inayopendwa zaidi baada ya kuvifikiria na kuvirekebisha.
- Ukifika hatua hii, inakusaidia kutayarisha tathmini na Jedwali ya matatizo na sululisho zilizopo (angalia Jedwali la 27)
- Tayarisha Jedwali la vihatarishi na mbinu zilizopo za makabiliano kwa kuziwekea mpangilio wa kipaumbele kwa ajili ya matumizi ya baadaye (anglia Jedwali la 28). Epukana na kufanya uamuzi juu ya ubora or ufanisi wa mbinu kwa hatua hii. Utathmini wa mbinu ni zoezi tofauti (hatua ya 3) na unatakiwa ufanyike kwa kuzingatia vigezo vitakavyotokana na malengo ya makabiliano.
- Panua hatua za makabiliano zilizopo kulingana na ujuzi na uzoefum na tayarisha orodha. Pamoja na kuorodhesha mbinu za makabiliano, fikiria pia matokeao kwa nawaume na wanawake.
- Kwa nyongeza, katika ile orodha ya mbinu za makabiliano pia fikria madhara kwa wanaume na wanawake.
Jedwali 26: Mfano wa upangaji safu wa athari za hali ya hewa
Hatari | Mvua kali | Pimajoto kuongezeka |
Athari |
|
|
Sababu ya hatari | udongo kwenye mteremko haujalindwa | Kukosa ujuzi wa udhibiti husishi wa wadudu na magonjwa |
Chanzo cha taarifa |
|
|
Cheo cha athari | Wakulima: Juu (3) Wadau: Wastani (2) Sayansi. Juu (3) | Wakulima: Wastani (2) Wadau: Wastani (2) Sayansi. Juu (3) |
Kipaumbele ya tatizo | Juu (3) | Wastani (2) |
Jedwali la 27: Mfano wa uainishaji wa vitisho vya hali ya hewa, athari na utambuzi wa chaguo zinazowezekana za kukabiliana
Hatari | Mvua kali | Pimajoto kuongezeka | Joto kali sana |
Athari |
|
|
|
Sababu ya hatari | udongo kwenye mteremko haujalindwa | Kutofahamu usimamizi wa mbinu mbadala dhidi ya CBB | Kupanda kahawa bila kivuli |
Chanzo cha taarifa |
|
|
|
Cheo cha athari | Wakulima: Juu (3) Wadau: Wastani (2) Sayansi: Juu (3) | Wakulima: Wastani (2) Wadau: Wastani (2) Sayansi: Juu (3) | Wakulima: Wastani (2) Wadau: Wastani (2) Sayansi: Juu (3) |
Kipaumbele ya tatizo | Juu (3) | Wastani (2) | Juu (3) |
Baadhi ya mbinu za makabiliano |
|
|
|
III. Kutafuta mbinu za makabiliano
c&c toolbox ilitambua mbinu za jumla za makabiliao (angalia “zana” kwenye c&c toolbox ). Neno 'jumla' limetumika kwa sababu ingawa zinaweza kufanya kazi kwa mazingira fulani, zana hizi haziwezi kutumika sehemu zote na zinaweza hata zikahitaji marekebisho ili ziendane na mazingira mengine. Pia zinahitaji zirekebishwe ili kuendana na mfumo wa uzalishaji wa kahawa, badala ya kurekebisha mfumo wa uzalishaji ili uendane na zana.
- Kwa mfano: Ongezeko la kivuli inaweza kukinga dhidi ya joto la juu, lakini kwa mazingira yenye unyevunyevu kivuli kinaweza kuongeza uwezekano wa ugonjwa kama vile American Leaf Spot.
Mbinu zinazotokea sehemu husika: Daima, wakulima wamekuwa wabunifu.Katika historia nzima ya kilimo, wamekuwa chanzo kikuu cha mawazo na majaribio. Hivyo, inawezekana kuwa baadhi ya wakulima kwenye eneo maalum wameunda zana au mbinu mpya au aina mpya ya zana zilizopo ambazo zinaweza kutumika.
- Kwa mfano: Nchini Brazil, c&c wamekuwa wakirabisha aina ya majani yaitwayo Bracharia kwa matumizi ya matandazo pamoja na matibabu ya jasi kwa udongo, na mbinu zote mbili zimegunduliwa na wakulima wenyeji.
Hivyo, inasaidia kuangalia kile kinachofanywa na wakuliwa kama mbinu za kienyeji za makabiliano dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi, na kuwekea mkazo zaidi kwenye uchunguzi wa ukanda wa chini wa kahawa, ambayo inawezekana itaathirika zaidi na mabadiliko ya tabia nchi.
Mafunzo kwa wafanyakazi wa mashambani yatahitajika ili waweze kuangalia shughuli zinazotendeka na wakulima kwa macho yaliyo wazi zaidi. Maelezo juu ya kunukuru mbinu mpya wanaoziona, kuzipiga picha na kunukuru mahali ilipo kwa kutumia GPS.
- Mfano: Miti ya kivuli inaweza kuwa na manufaa kwa kahawa, lakini pia kuna hasara.
Ingewezekana, majaribio makubwa na ya miaka mingi ingetakiwa ifanyike kwa baahi ya aina ya miti ili kuchinguza kufaa kwao kwa mazingira maalum, lakini hii inaweza kuchukua miaka mingi kuleta matokeo. Badala yake, tafuta mifano ya shambani ya kahawa inayoendelea vizuri ikiwa chini ya kivuli kwenye mazingira iliyokidhiri na ichinguze kama mfano wa majaribio ya muda mrefu.
Matokeo tarajiwa
- Jedwali la 28 linatoa muhtasari wa matokeo ya awamu ya tathmini kwa njia ya ukina na ni hatua nzuri ya kutayarisha mwanro wa upangaji wa makabiliano (Hatua ya 3)
- Kulingana na mahitaji maalum pamoja na hali halisi ilivyo hapo, pengine ingefaa kuandika ripoti yanye maelezo zaidi.
Muda unaohitajika
Wiki moja kwa kiongozi wa waajiriwa kupanga taarifa zilizokusanywa na siku moja kwa maafisa ugani.
Utaratibu
Kiongozi wa waajiriwa pamija na maafsa ungani wanapanga taarifa zilizokusanywa kwenye kipindi cha kazi.
Mbinu za makabiliano zinaweza kutambuliwa kwa kuitia mbinu zifwatazo:
- Kipindi cha kuchangia mawazo: Waalike wadau na wataalam kufikiria juu ya kila athari na kuzifikiria kwa mtazamo tofauti. Vikundi tofauti kama ilivyowekwa kwa muhtasari kwenye Jedwali la 27 inaweza kusaidia kuweka mbinu za aina mbalimbali. Kuwa mwangalifu juu ya salwa la jinsia ukiwa unatayarisha orodha ya utakaowaalika ili kuhakikish kuwa maoni ya wanaume na wanawake yanakusanywa. Wataalamu pia watoke fani mbali mbali, wakiwemo pia wanaohusiana na masomo ya jinsia.
- Mazoea ya kipindi kilichopita kuhusu jinsi gani watu walikabiliana na matukio ya hali ya hewa au uharibifu wowote mwingine.
- Mbinu ambazo zilishazingatiwa na kukataliwa au kutochunguzwa kwa undani zaidi.
- Walio kando: Wakulima wa ukandani waliokabiliana vizuri na matukio yaliyopita au walioathirika vibaya zaidi na mabadiliko ya tabia nchi.