Kusanya taarifa za kisayansi
Muhtasari
Kuzitafuta, kuzitafakari na kuzitumia taarifa za kisayansi zilizopo juu ya mabadiliko ya tabia nchi si kitu rahisi, hasa kama unashughulika na zao kama la kahawa.
utafiti wa mezani: udadisi wa utafiti juu ya hali ya hewa na
Fupisha taarifa juu ya mabadiliko ya Tabia Nchi za sasa na za mbele, vihatarishi na madhara.
Nadharia
Hali ya hewa ya sasa na ya miaka ya nyuma
Hatua muhimu kwenye ukusanyaji wa taarifa ni kujaribu kuzipata takwimu za kiutaalamu za hali ya hewa, na ikiwezekana kuwasiliana moja kwa moja na taasisi za hali ya hewa. Taasisi za utafiti za ndani au mashirika ya kahawa ya kitaifa pia wanazo takwimu hizi.
Takwimu za hali ya hewa mara nyingi kuonyeshwa kama viwango vya wastani, lakini kwa madhumuni ya kilimo, ni muhimu zaidi kuwa na viwango vinavyovuka mipaka ya kawaida (k.m. joto za juu na za chini kabisa). Kinyume na hii, zipo nchi zilizo na takwimu za kila siku, zinazoruhusu uthathmini wa takwimu ghafi na wale walio na utaalamu na uzoefu. Kwa mfano, kwa kutafsiri takwimu za hali ya hewa na kuziweka katika mpangilio maalum, kama vile ramani au model za hali ya hewa, taarifa hizi zinaweza kuwasilishwa kwa watu walio nje ya fani hiyo (angalia “Kujifunza kutokana na uzoefu: Ramani za Hali ya Hewa kwa matumizi ya wadau ukurasa wa 44).
Ni muhimu kutafuta vipimo vya joto linalokithiri na kubaini kama linakithiri zaidi au kutokea mara nyingi zaidi. Pia, hakikisha unaangalia muda na uzito wa mvua. Ingawa kunaweza kutokuwa na tofauti za mvua kwa mwaka, kunaweza kuwa na ishara za mvua zisizofululiza au mabadiliko kwenye mwanzo au mwisho wa msimu wa mvua. Itakapowezekana, tafuta msaada wa wataalamu wa hali ya hewa. Kumbuka kuwa mashirika mengine yanaweza kuwa wamefanya utafiti huo huo. Hivyo, itakusaidia pia ukishauriana na wawakilishi wa serikali na mashirika ya utafiti au taasisi zisizo za serikali kwenye mkoa wako.
Utabili wa hali ya hewa ya miaka ijayo: Makabiliano na kutokuwa na uhakika
Kuna mwongezeko wa idadi za model za hali ya hewa zinazotabili ongezeko wa joto na mvua kwa miaka ijayo, hadi kufukia mwaka 2100. Model hizi zinaweza kukupa picha ya mabadiliko ya tabia nchi kwa miaka ya mbele, lakini bado hazina uhakika wa kutabili viwango vya hewa ukaa hewani (ambazo zitaathiri kiasi na kasi ya mabadiliko yanayotabiliwa), tafsiri ya mifumo ya hewa na dunia (ambazo zitazalisha utabili tofauti), na tafsiri ya hatari na majanga
Ikibidi kuchagua miongoni mwa baadhi ya utabili kwa madhumuni ya kazi yako, ni muhimu kuelewa jinsi gani ilifanyika na kama inaonyesha anuwai ya model au picha. Itakapowezekana, tafuta ushauri wa kitaalam kukusaidia kutambua utabili utakautumia, kwa mfano, kutoka kwenye ofisi ya hali ya hewa.
Model tofautia huwa na maoni yanayofanana juu yaa mabadiliko kushinda nyingine. Kwa mfano, karibu model zote zinatabili kuwa kutakuwa na ongezeko la joto, lakini mara nyingi inapingamana juu ya kiwango cha ongezeko hili. Pia, kawaida kuna utofauti mkubwa juu ya utabili wa mvua. Ili kuonyesha tofauti kutokuwepo kwa uhakika, mara nyingi model zinatoa upana mkubwa wa utabili unauwezekana. Kwa mfano, utabili wa ongezeko la joto la nyuzi 3 za sentigred ifikapo mwaka 2015 inaweza kuwa na mashaka ya nyuzi 1.5 hadi nyuzi 5; utabili wa wastani wa mvua kwa ukanda maalum unaweza kuwa hasi, lakini mashaka yanaweza kuwa kati ya asilimia 20 hadi 50. utabili wa hali ya .
Utabili wa hali ya hewa kawaida unapatikana kwa ngazi ya mkoa au taifa, na isitoshe hautoi taarifa za kina kwa mahitaji ya ngazi ya ndani. Lakini ikitimika kwa usahihi inaweza kuwa chanzo muhimu cha taarifa kwa mwelekeo wa miaka ya mbele kwa sehemu maalum. Hata hivyo, inaweza kutumika ili kujenga picha ya mabadiliko ya tabia nchi na hivyo kusaidia kujenga mwanko miongoni mwa wadau.
Ukosefu wa takwimu za kisayansi
Bahati mbaya, katika nchi nyingi zinazozalisha kahawa, takwimu nzuri za hali ya hewa ni pungfu na vituo vya hali ya hewa ni vichache; takwimu za kihistoria hazijakamilika, hasa kwa ngazi za kienyeji. Kama hii ndiyo hali, shauriana na wanahistoria wa kienyeji pamoja na wataalam wengine, ama wa kitaalamu au wa kienyeji, pamoja na kutafuta kwenye mtandao wa ulimwengu.
- Kumbukumbu za kihistoria: uzalishaji wa kahawa una historia ndefu na ka kina. Kumbukumbu kutoka vituo vya utafiti na bodi za bidhaa zinaweza kutoa taarifa nzuri, na tathmini ya makini ya taarifa hizi inaweza kuangaza uthibiti wa matukio ya zamani ya hali ya hewa, pamoja na mabadiliko ya matumizi ya ardhi na viwango vya uzalishaji. Bodi nyingine rasmi zikiwemo vitengo vya serikali vya mambo vijijini au shughuli za ujenzi, pia zinaweza kuwa hifadhi muhimu.
- Takwimu binafsi: Baadhi ya mashamba makubwa ya kahawa zinaweza kuwa na takwimu zinazorejea miongo mingi, na isitoshe ina takwimu za hali ya hewa.
- Takwimu za umma: Hifadhi za magazeti zinaweza kuwa chanzo nzuri juu ya matukio ya hali ya hewa athiri na hata kuwa na taarifa maalum za hali ya hewa.
Vyanzo vyote hapo juu vinaweza kutoa takwimu muhimu, ambazo kwa pamoja zinaweza kutoa tathmini kamili ya hali ya hewa kwa miaka ya nyuma. Lakini, takwimu itachukuwa muda na gharama kuzikusanya. Kama taarifa za kisayansi hazipatikani na utafiti wa ziada hauwezi kufanyika, hakikisha unatathmini taarifa zinazopatikana toka kwa wakulima na wadau kwa makini.
Mwongozo wa vitendo
Lengo
- Kufahamu na kuelewa jinsi gani tabia nchi kwenye ukanda maalum itabadilika na jinsi gani hii itaathiri wakazi na uzalishaji wa kilimo.
- Kukusanya taarifa juu ja mabadiliko ya tabia nchi ya sasa na yaliyotabiwa, pamoja na mabadiliko ya jotoridi, mvua, matukio ya hali ya hewa iliyokidhiri, na matukio mengine muhimu kutika vyanzo vya kitaalam kwenye mtandao.
- Kuweka muhtasari, kutathmini na kutafsiri taarifa hizi za kitaalam.
Matokeo tarajiwa
- Orodha ya nyaraka, utafiti na ripoti
- Muhtasari wa taarifa zinazopatikana kuhusu mabadiliko ya tabia nchi kwenye nchi maalum na ukanda wa uzalishaji kahawa, na matokeo yanayoweza kutokana kwa uzalishaji wa kahawa.
Muda unaohitajika
Wiki moja hidi mbili, kulingana na upatikanaji wa takwimu na ujuzi uliopo kwa anayefanya utafiti huu.

Utaratibu
- Pitia na tathmini utafiti na utabili uliofanyika na IPCC kwa mikanda tofauti (angalia tarifa za kwenye muhtasari hapo chini)
- Angalia kama kuna utabili ambao umefanyika juu ya mabadiliko ya tabia nchi ukandani kutoka vyanzo kama Wizara ya Mazingira, Taasisi ya hali ya hewa, taasisi za utafiti wa kisayansi au mashirika ya kimataifa ya maendeleo.
- Pitia UNFCCC kwa ajili ya nchi yako maalum. Mawasiliano ya Kitaifa (National Communications) ni ripoti rasmi juu ya kila nchi iliyojiunga na UNFCCC na ina taarifa za kina juu ya athari zinazotarajiwa za mabadiliko ya tabia nchi kwa kila nchi.
- Panga taarifa hizi za kitaalamu kwa kufwatilia vihatarishi vya sasa na vya baadaye, athari za sasa na zinazotarajiwa baadaye (k.m. ziainishe kama 'Jotoridi', 'Mvua' na 'Matukio Iliyokidhiri ya hali ya hewa na matukio mengine'), pamoja na njia au mbinu mbali mbali za makabiliano.
- Kama ikiwezekana, fanya hitimisho juu ya maana ya taarifa hizi kwa ukanda wako maalum (angalia umbo la 37).
- Inashauriwa kuwa unatafuta ushauri wa mtaalam wa mambo ya mabadiliko ya tabia nchi ukutathmini taarifa hizi (k.m. kwa ajili ya kutayarisha amani za hali ya hewa).
Vyanzo vya taarifa
Ripoti za IPCC: ripoti hizi zinatoa muhtasari wa ujuzi uliopo sasa juu ya mabadiliko ya tabia nchi na athari zake kwa kila ukanda kijiografia na kiekolojia. www.ipcc.ch/publications_and_data/ar4/wg2/en/contents.html
UNFCCC Mawasiliano ya Kitaifa (National Communications) Nyaraka hizi zinawasilisha matokeo ya tathmini za kiataifa juu ya uzalishaji wa gesijoto, pamoja na taaraifa juu ya udhaifu, athari na makabiliano. unfccc.int/national_reports/non-annex_i_natcom/ submitted_ natcom/items/653.php na unfccc.int/ national_reports/annex_i_natcom/ submitted_ natcom/items/4903.php
Tovuti ya Taarifa za Mabadiliko ya tabia nchi ya benki ya Dunia ( The World Bank Climate Change Knowledge Portal). Jukwaa hili ni kifaa cha mtandaoni kinachoruhusu upatikanaji wa takwimu za kina za athari na udhaifu wa tabia nchi za sasa, za miaka iliyopita na utabili wa miaka ijayo kutoka ulimwengu mzima. sdwebx.worldbank.org/climateportal/index.cfm
Climate Wizard ina taarifa juu ya mabadiliko ya tabia nchi na inabainisha athari zilizoonekana sehemu yoyote duaniani. www.climatewizard.org
Adaptation Learning Mechanism inatoa muhtasari za nchi mbali mbali juu ya athari za mabadiliko ya tabia nchi ambazo zimeonekana na zinazotabiliwa. www.adaptationlearning.net
Taarifa za Umma: Kumbu kumbu za magazeti zinaweza pia kuwa chanzo kizuri cha taarifa juu ya matukio kidhiri yaliyotokea na inaweza pia kuwa na taarifa maalum za hali ya hewa.
Kuna vyanzo vingi vingine vya taarifa, mara nyingi zinapatikana kwa ukanda, mikoa au nchi maalum, amabazo hazijaorodheshwa hapa. Hakikisha kuwa unatafuta kwenye kwa kinaganaga kwenye mtandao na kushauriana na wataalam wenyeji. Vyanzo vilivyotajwa hapo juu vinaweza kukupatia takwimu za kufaa pamoja na tathmini ya kina ya mabadiliko ya tabia nchi kwa miaka iliyopita. Kama taarifa za kisayansi hazipatikani na utafiti wa ziada hautaweza kufanyika, inashauriwa kuzitathmini kwa uangalifu taarifa zitakazotoka kwa wakulima na wadau na kutumia hizi kama taarifa za msingi kwa kazi yako.