Rudi
B

Kusanya taarifa kutoka kwa wakulima

Muhtasari

Wakulima wa kahawa ni chanzo cha msingi cha taarifa, kwani wao wanafahamu kwa ukaribu hali ya kilimo, na mara nyingi hutambua mabadiliko ya uzalishaji wakati yakitokea.

Mbinu
  • uchunguzi wa mkulima mmoja mmoja
  • mahojiano na vikundi vya wakulima
  • warsha za wakulima, k.m.
Matokeo
  • Utambuzi wa hatua zinazotumika dhidi ya madhara kwa maeneo mbali mbali
  • Kuelewa wanaoathirika zaidi, na nini na kwa sabubu gani.

Nadharia

Taarifa kutoka kwa wakulima na jamii zao ni muhimu kwa kutambua vihatarishi kutokana na hali ya hewa, na kuwekea kipaumbele hatua za makabiliano. Ili kutathmini athari za mabadiliko ya tabia nchi kwenye uzalishaji wa kahawa, unganisha mbinu tatu zifuatazo:

  • Mahojiano ya mkulima ya ana kwa ana: (kumpima mkulima mmoja mmoja)
  • Mahojiano na vikundi maalum ya wazalishaji wa kahawa
  • Semina za wakulima, k.m. semina za kuhamasisha juu ya athari za mabadiliko ya tabia nchi kwenye uzalishaji wa kahawa au Semina ya Ushaidi wa Hali ya hewa.

I. Mahojiano ya mkulima ana kwa ana

Ubainishaji wa mkulima unatumia mahojiano ya mkulima pamoja na matembezi shambani. Itakusaidia kufanya yafuatayo: a) kutambua athari za mabadilko ya tabia nchi kwa uzalishaji wa kahawa, na b) kupata mtazamo, mazoea na maoni ya mkulima mmoja mmoja kulingana na matatizo ya sasa ya uzalishaji na changamoto kwenye mashamba yao.

Mtembelee mkulima, mhoji, na tembelea shamba lake. Wakati wa mahojiano, tambua matatizo makuu matatu, na wakati wa kutembelea shamba, angalia hali ya maeneo ya uzalishaji kwa ujumla. Wakati wa mahojiano haya kwanza, ni vema zaidi kutotaja hali ya hewa au mabadiiko ya tabia nchi, ili mkulima asitoe maoni yake juu la hilo. Kama matatizo ya hali ya hewa hayajitokezi kwenye majibu yao, hii inaweza kuwa dalili ya kuwa matatizo ya mabadiliko ya tabia nchi si muhimu au kuna matatizo mengine yaliyopewa kipaumbele, kama vile bei za kahawa. Pia, inawezekana kuwa baadhi ya matatizo yaliyotambuliwa yanatokana na mabadiliko ya tabia nchi, lakini wakulima hawatambui hivyo (k.m. kuongezeka kwa idadi ya wadudu au magonjwa).

Ni muhimu kufafanua idadi ya wakulima utakao wahoji ili kupata sampo kamili. Hii itategemea ukubwa wa eneo la mradi wako ua mtandao wa maafisa ugani, pamoja na utofauti wa hali ya hewa, mazingira, uchumi na utamaduni katika eneo la kazi. Jaribu pia kuwahusisha wakulima walio kwenye ukanda wa kando/chini za uzalishaji wa kahawa, kwani nao wanaweza kutoa taarifa muhimu , si tu juu ya athari za sasa za hali ya hewa, bali pia vihatarishi vya miaka ya mbele kwa eneo zima la kazi.

Maswali muhimu kwa mahojiano na mkulima ni::

  • Nini ni changamoto kuu unazokabiliana nazo kwenye uzalishaji wa kahawa?
  • Nini ni changamoto nyingine unazokabiliana nazo kwenye uzalishaji kwa ujumla?
  • Kama hali ya hewa(tabia nchi haikutajwa na mkulima, mwulize yafuatayo: Je, umegundua mabadiliko yoyote ya hali ya hewa kwa kipindi kizima cha shughuli zako za kilimo? Kwa marejeo, itasaidi kuuliza kama kumetokea mabadiliko ndani ya miaka 20 hadi 30 iliyopita.

Baada ya kukusanya taarifa hizi toka shambani, takwimu zinapaswa zipangwe na kutathminiwa. Kwa mfano, unaweza kuyaorodhesha matatizo yaliyotajwa na mkulima kulingana na idadi ya kutajwa (angalia: “Kujifunza kutokana na uzoefu: Kuorodhesha matatizo yaliyotajwa na wakulima”). Zoezi hili litakusaidia kuweka kipaumbele vihatarishi vilivyo muhimu zaidi na athari zake kwenye uzalishaji wa kahawa, ambayo itakuwezesha kukazania zaidi kila mbinu maalum la makabiliano.

Kielelezo 9: Majadiliano ya kikundi maalum nchini Brazil
kundi la watu wamekaa kwenye madawati darasani wakizungumza kesha.

II. Mahojiano na vikundi maalum vya wakulima

Mahojiano na kikundi maalum cha wakulima walio na historia ndefu (miaka 20 hadi 30) kwenye sehemu fulani inaweza kusaidia sana kukusanya mtizamo wa ndani na maoni juu ya vihatarishi na athari za hali ya hewa.

Waombe wakulima wajibu maswali matatu ya msingi:

  • Hali ya hewa imebadilika vipi ndani ya miaka 20 iliyopita? Umeona mabadiliko yoyote ya mvua au joto kwenye miezi maalum?
  • Kumekuwa na mabadiliko yoyote ya misimu ya uzalishaji wa mashamba yako?
  • Vihatarishi vikuu inavyosababishwa na hali ya hewa ni vipi? Je, vihatarishi hivi vina athari yoyote nyingine? Kwa mfano, mvua nzito zinaweza kusababisha mporomoko wa ardhi zinazoweza kuziba barabara na kufanya kufika masokoni kuwa vigimu.
  • Wanawake na wanaume (wazee na vijana) wanaathriika vipi kutokana na vihatarishi vya hali ya hewa?
  • Unaonaje miaka ya mbele ya uzalishaji wa kahawa a) kwenye eneo lako na b) kwenye ukanda/mkoa wako?

Baada ya kunukuru maoni na dhana za wakuliima juu ya mabadiliko ya tabia nchi, utofauti wa hali ya hewa, na kithiri, inakubidi kutathmini takwimu. Fafanua kwa ukalimifu wakati ukipanga sifa kwa kuzingatia viwango na ugumu wa hatari za mazingira, na ikiwezekana tofautisha kati ya sababu za athari ziinazotokea. Ni muhimu kukumbuka kuwa athari za hali ya hewa hazitokei peke yake mbali na mabadiliko ya kijamii, kiuchumi na kimazingira. Hivyo, si rahisi au njia nzuri kuyatenga matatizo haya na kudai kuwa “yanasababishwa na hali ya hewa tu”. Kwa mfano, mabadiliko ya hali ya hewa yanaweza kusababisha hali nzuri kwa magonjwa, lakini magonjwa yanaweze kusambazwa kutokana na msukosuko kati ya mashamba.

III. Semina ya uhamasishajii wa wazalishaji juu ya hali ya hewa

Semina shirikishi, kama vile Semina za Ushahidi wa Hali ya hewa12 au semina ya uhamasishaji juu ya mabadiliko ya tabia nchi na athari kwa uzalishaji wa kahawa, zinaweza kusaidia kutathmini jinsi gani wakulima wanavyofikiria juu ya mabadiliko ya tabia nchi, na kufafanua mbinu bora. Semina zinaweza kuongezea taarifa utakazokusanya kutokana na uchunguzi wa wakuima. Mbinu mojawapo ni kutekeleza Semina ya Ushahidi wa Hali ya hewa kwa siku mbili pamoja na jamii maalum au na kikundi maalum cha wakulima, kwa mfano wajumbe wa shirika . Matokeo yawe mpango wa vitendo kwa ajili ya kutatua changamoto walizozitambua wao wenyewe.

Umbo Na 10: Semina za Ushahidi wa Hali ya hewa kwenye Mradi wa c&c, Trifiio
kundi la watu wamekaa kuzunguka meza wakizungumza kesha.

Ratiba ya muda inamsaidia mkulima kuelewa zaidi shughuli za kibinadamu na kimazingira zilizoathiri maisha na mazingira yao kwa kipindi kilichopita (kawaida miaka 20).

Kalenda ya misimu: inanukuu matukio na shughuli za mizunguko, na jinsi gani hizi zimebadilika kwa miongo iliyopita.

Orodha ya wanyama na mimea inasaidia taarifa juu ya viumbehai vilivyopo na jinsi gani hivi vimebadilika muda unavyoenda.

Kurejesha maswala kwa kuzingatia shughuli zilizofanyika awali inasaidia kutambua mabadiliko ya mazingira na maisha ya wakulima yanayosababishwa na mabadiliko ya tabia nchi.

Maoni ya pande mbili inaongezea kwenye majadiliano juu ya jinsi gani wakulima wanavyotambua mabadiliko ya tabia nchi, na jinsi gani mabadiliko haya yataathiri maisha yao, na wangependa maisha yao yaweje kwa miaka ya mbele.

Zoezi la kipaumbele cha rasilimali inasaidia wakulima kuamua ni rasilimali zipi zina umuhimu kwao na hivyo yahifadhiwe kwa miaka ijayo. Katika zoezi hili, 'rasilimali' yanafafanuliwa kuwa mali za mazingira, kama vile ardhi, maji, mimea maalum, mazao maalum, n.k.

Orodha ya matatizo inasaidia kutathmini maswala ya mabadiliko ya tabia nchi na mbinu za kukumbana nazo.

Kwenye zoezi la mti wa matatizo, wakulima wanaamua ni changamoto zipi zinahusian na mabadiliko ya tabia nchi (angalia Umbo Na 11)

Zoezi la mionzi ya jua inaweza kutumika kugawa matatizo katika sehemu ndogo ndogo, na kutafutia ufumbuzi.

Tathmini ya mbinu za makabiliano inasaidia wakulima kuamua ni shughuli zipi wazipe kipaumbele ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

Hatimaye, muhtasari wa matokeo inafupisha hatari zote za hali ya hewa na mbinu za makabiliano kama zilizoshauriwa na wakulima.

Matokeo ya Semina ya ushahidi wa Hali ya hewa ni ya muhimu sana kwa mchakato wa pembe tatu.

Mpangilio na shughuli zitakazotekelezwa kenye Semina ya ushahidi wa Hali ya hewa yanahitaji kurekebishwa kulingana na mahitaji na uwezekano. Kama hutakuwa na muda wa kutayarisha Semina nzima ya ushahidi wa Hali ya hewa, badala yake unaweza kufanya semina ndogo zaidi ya kuhamasisha juu ya hali ya hewa kwa kutumia mbinu kama vile:

  • Maoni ya pande mbili na Orodha ya matatizo
  • Zoezi la mti wa matatizo
  • Zoezi la mionzi ya jua
Jedwali 7: Semina ya Mashuhudio ya Mabadiliko ya Tabia Nchi

Siku ya Kwanza

Siku ya Pili

  • Mpango muda
  • Kalenda ya misimu
  • Orodha ya wanyama na mimea
  • Maonyesho na marejeo ya matokeo, kulinganisha na Mabadiliko ya Tabia Nchi
  • Kutafakari: maoni ya pande mbili
  • Kipao mbele cha thamani
  • Orodha ya matatizo
  • Mti wa matatizo
  • Zoezi la mionzo ya jua
  • Umadadi wa mbinu za Makabiliano
  • Matokeo kwa ufupi

Mwongozo wa Vitendo

I. Uchunguzi wa mkulima binafsi

Lengo:

  • Kutambua vihatarishi vya tabia nchi na athari zake kwa uzalishaji wa kahawa, na kupata dhana, mazoea na maangalizi ya mkulima mmoja mmoja kuhusu changamoto anazozipata kwenye kuzalisha kahawa shambani kwake sasa.
  • Kuchanganua taarifa juu ya mabadiliko ya tabia nchi kwa sehemu maalum, vihatarishi vya tabainchi na athari, pamoja na kutambua mahitaji ya makabiliano.

Matokeo tarajiwa: Muhtasari wa hatari tofauti zinazohusiana na tabia nchi, na athari kuu kwenye uzalishaji wa kahawa, pamoja na rodha ya mbinu mbalimbali za makabiliano yanayofaa.

Muda unaohitajika: Wiki moja hadi tatu, kutegemeana na upatikanaji wa maafisa ugani na idadi ya wakulima watakaohojiwa

Umbo la 28: Mzalishaji anaweza kufafanua athari za tabia nchi kwa eneo maalum na kutambua mbinu za haraka za makabiliano
mwanaume na mwanamke wamesimama bustanini wakiangalia ubao wa kunakili .

Utaraibu:

  • Tambua idadi ya wakulma watakahojiwa kulingana na upana wa eneo na utofauti wa hali ya hewa kwenye eneo la kazi yako (k.m. wazalishaji 14 hadi 30). Wahusishe wazalishaji kutoka sehemu mbai mbali za uzalishaji, hasa wakulima walio kwenye ukanda wa pembeni (k.m. walio kwenye sehemu za chini au juu sana za milima), na walio na historia ndefu ya uzalishaji kwenye eneo (k.m. zaidi ya miaka kumi), kwani hawa watatoa taarifa zinazofaa kuhusu mabadiliko ya sasa ya tabia nchi na athari zake, lakini pia vihatarishi vya miaka ijayo kwa eneo zima.
  • Tembelea mashamba ya kahawa na fanya ukaguzi wa eneo na mahojiano kwa fupi na mkulima mmoja mmoja juu ya hali ya uzaliishaji na matatizo yanayoshusiana na hali ya hewa (angalia mwongozo kwa ujumla na ushauri juu ya mahojiano na wakulima na vigezo vya ubainishaji hapo chini). uu Wakati wa mahojiano, tambua matatizo makuu matatu.
  • Wakati wa ukaguzi wa shamba angalia hali ya ujumla ya eneo la uzalishaji.
  • Wakati wa hatua hii ya kwanza ya mahojiano, ni bora kutokutamka hali ya hewa au mabadiliko ya tabia nchi, ili mkulima asishochewe kuitaja. Kama mabadiliko ya tabia nchi hayatajitokeza kwenye majibu yake, hii inaweza kuwa dalili ya kuwa mabadiliko ya tabia nchi si muhimu au kuna maswala mengine yalioshika kipaumbele, kama vile bei ya kahawa. Inawezekana pia kuwa matatizo yatakayotajwa yanahusiana na tabia nchi, lakini mkulima hatambui hilo,k.m. kuongezeka kwa wadudu au magonjwa.
  • Wakati wa mahojiano, kusanya taarifa juu ya mabadiliko ya sasa ya tabia nchi (k.m. jotoridi, mvua, matukio iliyokidhiri, pamoja na mengine yatakayokuwa muhimu) kutokana na mtazamo wa wakulima na matatizo makuu matatu watakayoyataja kuhusiana na mabadiliko ya tabia nchi.
  • Kagua kwa makini hali ya mfumo mzima au kiwanja kizima cha uzalishaji wa kahawa (angalia mwongozo wa ukaguzi wa shamba hapo chini).
  • Tamba udhaifu (k.m. miti ya zamani ya kahawa,au kutokuwepo kwa mimea ya kufunika udongo) pamoja na mbinu za makabiliano (k.m. vitendo vya kilimo bora vinavyoufanya mfumo wa uzalishaji uwe jasiri zaidi.
  • Tambua udhaifu (k.m. miti miyee za kahawa au kutokuwepo na mayao za kufunika udongo) pamoja na mbinu bora za makabiliano (k.m. vitendo vya kilimo bora vinavyosaidid kuipa ujasiri mfumo wa uzalishaji.
  • Nukuru taarifa zote muhumu kwenye dondoo ya mahojiano
  • Panga na chambua taarifa zote ulizozikusanya na tambua matatizo makuu matata wakulima wanayokabiliana nayo. Matokeo kutoka ubainishaji wa wakulima yanaweza kuchambuliwa na kupangwa kwa kupanga matatizo yaliyotajwa na wakulima, k.m. pointi tatu kwa tatizo la kwanza lililotajwa, pointi mbili kwa tatizo la pili na pointi moja kwa tatizo la tatu (analia mfano wa kupanga hivi hapo chini)
  • Kwasababu si wakulima wote watazipa kipaumbele cangamoto zile zile, orodha ya matatizo kawaida itakuna na zaidi ya matatizo matatu. Kwenye Jedwali au ripoti, fupisha vihatarishi ya hali ya hewa kwa uzalishaji wa kahawa kwa sehemu maalum, athari zake na mbinu zinazowekana za makabiliano.
  • Taarifa hii iliyojuishwa na kutathminiwa itakusaidia kutambua matatizo makuu yanayohusiana na tabia nchi kutokana na mtazamo wa wazalishaji, na kutambua mahitaji ya wanza kwa ajili ya makabiliano.
mwanaume aliye na shati nyeupe mwenye mmea wa kijani mgongoni mwake anaongea na mwanamke aliye na shati la waridi

Mwongozo na ushauri wa ujumla wa kuhoji wakulima

  • Eleza kuwa madhumuni ya kuwatembelea ni kupata maoni ya mtazamo wa wakulima juu ya changamoto anazozipata kwenye uzalushaji (usijadili maswala ya mabadiliko ya tabia nchi kwa mahojiano haya) u
  • Nukuru taarifa za ujumla kama ilivyoelekezwa kwenye Jedwali la vigezo kwa ajili ya ubainishaji wa wakulima (angalia dondoo la mahojiano ya waulima hapo chini)
  • Mwulize mkulima changamoto yake kuu kwenye uzalishaji wake wa kahawa. Ni muhimu kumwuliza maswali yafwatayo ili kutambua kama tatizo lake linahusiana na maswala ya tabia nchi, k.m. kama tatizo lake kuu ni kushambuliwa na wadudu, mwulize: Ni mdudu yupi ndiye tatizo kubwa zaidi? Je, mmekuwa mkishambuliwa na mdudu huyu maeneo haya au ni mdudu mpya? Unafanya nini kumdhibiti mdudu huyu?
  • Mwulize mkulima kuhusu changamoto nyingine anayekabiliana nayo hususan kwa kumuliza maswali ya ufafanuzi. Jumla ya changamoto kuu tatu itatosha ili mahojiano yawe mafupi na yenye kutosheleza.
  • Mwulize mkulima kama ameona mabadiliko yoyote ya mikondo ya mvua na/au jotoridi kwenye miaka iliopita (kwa kawaida ni vema kuulizia mabadiliko yaliyotokea ndani ya miaka 20 hadi 30 iliyopita).
  • Mwulize mkulima kama kuna uwezekano wa kutembelea shamba lake.
wanaume wawili wanapiga magoti shambani wakitazama mmea mdogo .

Mwongozo kwa ukaguzi wa shamba

Angalia hali ya ujumla ya shamba kwa kufikiria maswali yafwatayo:

  • Mashamba ya kahawa yana umri gani? Je, unaweza kuona shughuli za upandaji mpya au upogolewaji?
  • Je, kahawa inaonekana kuwa na afya? Kuna dalili za kunyeuka au upungufu wa virutubisho?
  • Je, kuna dalili za mmomonyoko au mporomoko wa ardhi?
  • Je, kuna zao au matandazo ya kufunika udongo?
  • Je, mfumo ni wa kivuli, bila kivuli au mchaganyiko wa mazao na msitu?
  • Je, kuna dalili za wazi za mashambulizi ya wadudu au/na magonjwa? Kama ndiyo, Je hizi zinahusiana na hali maalum ya tabia nchi?
  • Udongo ukoje? Kuna maji yoyote kwenye au karibu na shamba?

Wakati wa mahojiano, na wakati wa matembezi shambani pia, nukuru kwa ufupi unachoona na kinachosemwa ili kukamilisha maadaye ukiwa na muda zaidi.

II. Mahojiano ya makundi maalum ya wakulima

Lengo:

  • Kufahamu jinsi gani wahudhuria wanavyodhani juu ya mabadiliko ya tabia nchi na kupata mtazamo wa kwanza wa mabadiliko ya eneo husika ya tabia nchi na athari zake kwa uzalishaji wa kahawa
  • Kupata dhana, mazoea na mitazamo kwa mahojiano ya kikundi maalum na kutambua vihatarishi vya tabia nchi kwa eneo maalum na athari zake kwa uzalishaji wa kahawa.
  • Kuweka muhtasari wa taarifa juu ya vihatarishi vya mabadiliko ya tabia nchi kwa sehemu husika, athari na mahitaji ya makabiliano.

Matokeo tarajiwa: Muhtasari wa vihatarishi vinavyohusiana na tabia nchi na athari kuu kwa uzalishaji wa kahawa zinatambulika na wazalishaji, na orodha ya mbinu za makabiliano (angalia repoti za mbinu ya pembetatu kwenye c&c toolbox)

Muda unaohitajika: Wiki moja hadi tatu, kutegemeana na upatikanaji wa maafisa ugani

Utaraibu:

  • Chagua kikundi cha wakulima tano hadi kumi, hasa walio na historia ndefu ya uzalishaji kwenye eneo hilo (yaani, zaidi ya miaka kumi)
  • Tafuta sehemu wazalishaji wanapoweza kukaa kwa astarehe
  • Lengea majadiliano kwenye maswali matatu hadi manne na nukuru majibu.
  • Waulize wakulima maswali yafwatayo:
    • Je, mnafikiria vipi mkisikia maneno 'mabadiliko ya tabia nchi'
    • Mmeona mabadiliko yoyote kwenye maeneo yenu ndani ya miaka 20 hadi 30 iliyopita? Kama ndiyo, ni mabadiliko gani?
    • Nukuru majibu yao kwenye kadi ndogo. Majibu yao bila shaka yatakuwa mchanganyiko kati ya vihatarishi za tabia nchi (k.m. mvua kali) na athari za tabia nchi (k.m. kuzidika kwa kutu ya majani)
    • Bandika kadi ukutani na panga majibu kwa makundi mawili: a) vihatarishi vya tabia nchi kama vile mabadiliko ya jotoridi au mvua, na b) athari za tabia nchi, kama vile matokeo wanayoyasikia wazalishaji yanayosababishwa na mabadiliko ya tabia nchi.
  • Baada za mzunguko huu wa kwanza wa maswali na baada ya kuyapanga kwa makundi, uliza maswali hususan zaidi, kama vile yafwatayo:
    • Je,umegundua tofauti yoyote za mvua au jotoridi kwa miezi maalum?
    • Kumekuwa na mabadiliko ya misimu yenu ya uzalishaji? -
    • Ni jinsi gani wanawake na wanaume wameathiriwa na athari za tabia nchi?
  • Kama wahudhuria wanasikia ugumu wa kujibu, unaweza kuwatolea mifano kufafanua maana ya maswali. Nukuru majibu kwenye vikadi vidogo na lenga kutambua baadhi ya mabadiliko ya tabia nchi ya kienyei na atahri zake.
  • Jaribu kuweka kipaumbele kwa mabadiliko mawili hadi matatu kwa tabia nchi ya pahala husika na athari zinazosababishwa kwa uzalishaji wa kahawa. Vipange kwa makundi kulingana na uhusiano wao, kwa mfano mvua kutonyesha kwa msimu.
  • Tathmini mitazamo ya mabadiliko ya tabia nchi yanaayotjwa. Ukutathmini, hakikisha unazingatia yafwatayo29:
    • Hakikisha unatofautisha athari za tabia nchi na athari nyingine na chunguza uhusiano kato ya hizi mbili. Athari za tabia nchi (k.m. ukame, mafuriko, au jotoridi kuongezeka) inaweza kuathiri athari nyingine zisizo za tabia nchi (k.m. athari za kibayolojia kama vile wadudu)
    • Inawezekana wahudhuria watataja uhadimu wa
Jedwali 22: Kuthamini idadi na viwango vya athari za hali ya hewa

Examples

General description

Detailed, more useful description

Frequency

More frequent droughts

Forty years ago, drought used to occur once every five years, but in the last decades, droughts have been occurring once a year or so.

Intensity

Moderate drought

Two to three weeks without rainfall and unusually warm temperatures.

Umbo la 29: Semina ya Shahidi wa tabia nchi kwenye mradi wa c&c Trifinio
mwanaume anatoa mwasilisho kwa kundi la watu walioketi kwenye benchi .

III. Semina ya Shahidi wa Tabia nchi 30 (semina ya kuhamasisha juu ya tabia nchi)

Lengo: Kutathmini wakulima wanavyodhania juu ya mabadiliko ya tabia nchi kwa maeneo yao na kuata dhana juu ya kukabiliana na changamoto

Ushauri:

  • Fanya warsha hii ya siku mbili na jamii maalum au na kikundi kilichofafanuliwa cha wakulima wa kahawa, wakiwemo wanaume na wanawake (si zaidi ya wahudhuria 25), k.m. mashirika. Wasimame utayarishaji wa mpango wa utekelezaji wa mawazo yao ya kukabiliana na changamoto zinazotokana na mabadiliko ya tabia nchi.
  • Weka pia swala la jinsia kama sehemu ya semina kwa kuhakikisha kuwa wanawake na wanaume wanahudhurua kwa idadi sawa. Pia fikiria makundi mchanyanyiko kwa kila shughuli ili kutathmini jinsi gani mabadiliko ya abianchi yanaathiri wanaume na wanawake.
Jedwali 23: Shughuli za Semina ya Ushahidi wa Mabadiliko ya Tabia Nchi

Siku ya Kwanza

Shughulli

Lengo

Ratiba

Kusaidia wakulima kuelewa zaidi matukio yaliyoathiri maisha na mazingira yao

Kalenda ya misimu

Kunukuru matukio yanayofanyika kwa msimu na kuangalia yalivyobadilika miaka ya nyuma

Orodha ya wanyama na mimea

Kukusanya taarifa juu ya viumbe hai vinavyopatikana na vilivyopotea,

Ainisha matokeo

Kutambua mabadiliko kweye mazingira na maisha ya wakulima, ambayo yanasababishwa na mabadiliko ya tabia nchi, kama ilivyotambuliwa awali

Maoni ya pande mbili

Kuimarisha majadiliano kuhusu mtazamo wa wakulima juu ya mabadiliko ya tabia nchi, jinsi inavyoathiri maisha yao na jinsi wangependa miaka ya mbele yawe kwao.

Jedwali 23: Shughuli za Semina ya Ushahidi wa Mabadiliko ya Tabia Nchi (inendelea)

Siku ya Pili

Shughulli

Lengo

Maadili muhimu

Wakulima wanaamua maadili yapi ni muhimu kwao, na ni yapi wangependa kuyaingiza atka maisha ya mbele.Shighuli hiiinazingatia kuwa “maadili” ni mali ghafi kama vile ardhi, waji, mimea maalum, mazao maalum, n.k.

Orodha ya matatizo

Matatizo yaliyotambuliwa na wakulima yanapangwa katika mfumo, na kurahisisha kufikiria makabiliano ya kuyatatua.

Mti wa matatizo

Kutambua kama changamoto kweli zinatokana na mabadiliko ya tabia nchi.

Zoezi la mionzo ya jua

Kuvunya matatizo katika sehemu ndogondogo ili kurahisisha utatuzi.

Tathmini ya mbinu za Makabiliano

Kusaidia wakulima kuamua ni matatizo yapi yapewe kipau mbele

Muhtasari wa matokeo

Kutowa picha ya jumla kuhusu athari za hali ya hewa, na mbinu za makabiliano kwa wakulima

Mtiririko wa muda ya shirika la wakulima na jamii

Mtiririko wa muda ni orodha ya matukio muhimu kwenye historia ya shirika na eneo lake, iliyopangwa kwa mtiririko. Inasaidia majadiliano na uchnguzi wa mienendo iliyopita, shughuli, matatizo na mafanikio. Inasaidia kuyarejea matukio na mazoea yaliyopita wakati wa kupanga malighafi na kufanya maamuzi, na kuangalia jinsi gani yaliathiri dhana na shughuli za sasa.

Matukio ya mtiririko wa muda yanaweza kuwa pia matukio ya kidini na kiutamaduni, uhamiaji wa watu, uanzaji wa teknolojia mpya, maafa asilia, matukio na maamuzi ya kisiasa, miradi ya maendelea na mengine.

Ili kutayarisha mtiririko wa muda, wahudhuria wananukuru matukio ya miaka iliyopita kurudi nyuma vizazi vingi iwezekanavyo. Majadiliano kwenye kikundi juu ya mtiririko wa muda yatatoa fursa nzuri kuwauliza wazee juu ya matukio yaliyotokea na mwitikio wa kiutamaduni.

Lengo: kusaidia shirika kuelewa vizuri zaidi matukio ya kiasilia na yaliyosababishwa na binadamu, yaliyoathiri maisha yao na mazingira yao.

Mahitaji: Karatasi (ukubwa wa ubao) na kalamu kubwa za wino (makapen)

Muda unaohitajika: Saa moja

Umbo la 30: Mtiririko wa muda, mradi wa c&c nchini Brazil
ratiba imeandikwa kwenye kipande cha karatasi .

Utaraibu:

  • Elezea lengo la mtiririko wa muda. Waombe wahudhuria kutambua matukio yaliyoathiri shughuli za mtu mmoja mmoja na shughuli za shirika. Anza na mtu mmoja kwa kutambua tukio moja muhimu kwa muda uliopita na jaribu kutambua ni mwaka gani ilipotokea. Si lazima hii iwe tukio la kwanza kabisa wanaloweza kulikumbuka. Nukuru tukio na mwaka wa tukio, kisha uliza tukio lingine kabla au baada ya tukio la kwanza. Lisaidie kikundi kuzidi kuenda miaka ya nyuma hadi matukio ya kwanza kabisa wanayoyaweza kuyakumbuka. uu Nawezekana kuwa majadiliano yataanza kwa kasi ndogo. Tumia mwongozo wa maswali yafwatayo ili kuongeza kasi kidogo:
    • Ni lini watu walianza kuhamia maeneo ya hapa na walitokea wapi? Ni lini vimbunga, mafuriko, mazao kushindwa kuota kabisa au maafa mengine ya kiasilia kutokea?
    • Ni shughuli zipi za maendelea yametekelezwa kwenye ukanda huu? uu Nukuru matokeo yote yanayotajwa kwenye karaasi ndefu. Tumia herufi kubwa na kwa lugha inayoeleweka na wote uu Kama kutatokea matatizo kwenye kutambua tarehe maalum za baadhi ya matukio, jaribu kuyahusisha na matuko yanayofahamka (k.m. kupatikana kwa uhuru wan nchi).
  • Mtiririko wa muda ukikamilika, mmojawapo wa wahudhuria awakilishe muhtasari wa matokeo.

Kalenda ya misimu

Kalenda ya misimu ni kifaa cha kunukuru vipindi vinayojirudia mara kwa mara (k.m. misimu) na matukio muhumu yanayoathiri shirika. Inatoa picha ya ujumla ya vipindi vya kimazingira, kimila, kisiasa na kiuchumi kwa mwaka mzima.

Kalenda ya misimu ina thamani maalum kwani inaruhusu watu wa eneo fulani kuwakilisha uelewa wao wa misimu kulingana na kilimo. Mara nyingi nii inatofautiana na miimu 'rasmi' na kaleda za kimataifa.

Lengo: Kutayarisha kalenda ya misimu ya ushirika.

Mahitaji: Karatasi, gundi ya karatasi (tepu) au pini, penseli, peni na peni za rangi au makapen.

Muda unaohitajika: Saa moja hadi masaa mawili.

Umbo la 31: Semina ya Shahidi wa Tabia nchi kwenye mradi wa c&c nchini Brazil
duara ya mchoro iliyo na maneno 'calendario temporal' juu

Utaraibu:

  • Unda makundi manne na uhakikishe unachanganya wadogo na wakubwa pia wanaume na wanawake
  • Unda makundi mannena hakikisha kila kikundi kimechanganyika kati ya wazee na vijana, pamoja na wanaume na wanawake. Chora duara kwenye makaratasi manne na weka alama kwenye sehemu ya juu kabisa ikiwa ni “mwanzo wa mwaka/Januari”. Eleza kuwa sehemu ya chini kabisa ya duara inawakilisha nusu mwaka na kufika alama ya juu kabisa inawakilisha kuwa mwaka mpya umeanza. Gawa duawa katika sehemu 12, ikiwakilisha kila mwezi. Gawanya karatasi iliyokwisha tayarishwa na mchoro huu kwa kila kikudi ili watayarishe kalenda yao ya misimu. Inashauriwa kuwa hii inatayarishwa kabla ya kuanza semina na kuyagawa kwa vikund baada ya kueleza utaratibu wa shughuli hii.
  • Gawa vikundi hivi vinne kwa mada zifwatazo na waombe wafafanue matukio yanayoendana na mada yao kwa kila mwenzi:
    • Mimea na wanyama: k.m. miti kuchanua, matunda na mboga kuiva, ndege kuhama, n.k.
    • Kilimo: k.m. muda wa kupanda na kuvuna, utayarishaji wa mashamba, kuweka mbolea, hatua za kutayarisha mazao n.k.
    • Tabia nchi: k.m. vipindi vya mvua, vipindi vya kiangazi, msimu wa vimbunga, ukame, upepo, jotoridi za juu/chini n.k.
    • Matukio ya kijamii: k.m. sikukuu, siku za sherehe maalum, siku za masoko
  • Wahudhuria wanaweza kutumia maandishi au ishara kuwakilisha matukio kwa mwaka mzima. Hakikisha kuwa kila kikundi wanajiwekea vielelezo na majina ya wenye kikundi kwenye kila kalenda.
  • Wote wakiwa wamekamilisha, mwombe mwakilishi mmoja kutoka kila kikundi kuwakilisha matokeo ya kikundi chake, ambayo yatajadiliwa na kukamilishwa na kikundi kizima.

Orodha ya wanyama na mimea

Wazalishaji mara nyingi watakuwa na ujuzi wa kina juu ya mimea na wanyama wanaopatikana kwenye mazingira yao. Baadhi yao watakuwa na ujuzi mkubwa juu ya uhusiano kati ya wanyama na mimea. Orodha hi itaruhusu kupata picha ya jumla ya mimea na wanyama kwenye ukanda wa shirika.

Lengo: Kukusanya taarifa juu ya viumbe anuwai vilivyopo.

Mahitaji: Karatasi (yenye ukubwa wa ubao wapini),
vitabu juu ya mimea ny wanyama wa maeneo husika,
makapen.

Muda unaohitajika: Saa moja hadi masaa mawili

Umbo la 32: Orodha ya wanyama na mimea, mradi wa c&c nchini Brazil
a man pointing at a board that says " uso " on it

Utaratibu:

  • Waombe wahudhuria wajipange katika makundi yao manne ya awali uu Liombe kila kikundi kutayarisha taarifa zifwatazo:
    • Jina la mmea/mnyama;
    • matumizi yake au umuhimu wake;
    • Uwingi wa kupatikana na upungufu
    • Maeneo ya kupatikana
  • Gawa makaratasi yaliyotayarishwa kwa kugawanywa kwa safu nne (na vichwa vyake vimeandikwa juu) vitakavyowekea kila kikundi msisitizo mmoja kama ifwatavyo:
    • Miti na mimea
    • Mimea za kilimo
    • ndege na wanyama
    • Mfumo wa kahawa
  • Kama muda utaruhusu, omba vikundi vizunguke ili kila kikundi kipate nafasi ya kufanyia kazi kila moja ya mada nne.
  • Mwombe mmoja wa kila kikundi kuwakilisha matokeo na wahudhuria wote kuyajadili

Uwasilishaji na marudio ya matokeo na kuyahusisha na mabadiliko ya tabia nchi

Lengo: Kutambua mabadiliko kwenye mazingira na maisha ya jamii ambayo yanahusika na mabadiliko ya tabia nchi.

Mahitaji: Matokea ya shughuli za awali na makapen

Muda unaohitajika: Saa moja hadi masaa mawili

Mtiririko wa Matukio: Waombe wahudhuria kugawanya taarifa kutoka mtiririko wa matukio kwenye mafungu kama vile matukio ya kimazingira/kiasilia (k.m. matukio ya maafa ya kiasilia) au matukio yaliyosababishwa na binadamu (k.m. shughuli za kiuchumi). Zungusha kila tukio la kimazingira/kiasilia kwa duara jekundu. Chagua baadhi ya matukio ya kimazingira, kama vile kimbunga au uhaba wa maji, na waombe wahudhuria kufafanua kama uwingi na/au nguvu ya tukio hili linaongezeka au kupungua. Nukuru majibu

Orodha ya wanyama na mimea: Waombe wahudhuria waangalie orodha na watambue wanyama wanaopatikana kwa uwingi kwa sasa. Waombe wajadili na kunukuru sababu zao kupotea na athari zinazoweza kutokana na upotefu huukwa maisha yao. Pia wajadili kama kuna aina ya wanyama ambao ni wapya kwa maeneo yao na kujadili athari zinazowezekana kutokana nao.

Kalenda ya misimu: Waombe wahudhuria kuzipitia tena kalenda za misimu. Jadili mabadiliko au matukio yasiyo ya kawaida amabyo wameyaona kulingana na misimu kwa miaka ya karibu. Matukio haya yanaweza kuwa kama vile ukame wa muda mrefu, kuzidi kwa mvua, miti kuwahi kuchanua au kutochanua kwa mpangilio, n.k. Nukuru mabadiliko yanayotajwa.

Kumbuka: mtazamo wa pande mbili

Lengo: Kuchunguza jinsi gani shirika linadhania mabadiliko ya tabia nchi, jinsi gani mabadiliko haya yataathiri maisha yao na jinsi gani wangependa maisha yao ya mbele yaonekane.

Muda unaohitajika: Dakika tano mwishoni mwa siku ya kwanza

Utaratibu:

  • Kabla ya kuondoka siku ya kwanza, waombe wahudhuria kufikiria uzalishaji wao wa kahawa kwa miaka ya mbele, na vile vile nyumba, familia na jamii zao.
  • Waombe wachunguze nini kitatokea kwa miaka ya mbele ikiwa kila kitu kitaendelea kama ilivyo sasa.
  • Baada ya hapo, waombe wawaze vipi wangependa maisha yao ya mbele yaonekane.
  • Waombe wawaze wakitembelea mashamba yao ya kahawa na wachague malighafi zao muhimu zaidi. Hivi viwe vitu wanavyoweza kushika mikononi mwao (k.m. maji, ardhi, mti maalum, tunda la kahawa n.k.). Watambue vitu vitatu vya aina hii.
  • Baaaya hapo, wafikirie chochote kinachoweza kuhatarisha vitu hivi kwa miaka ya mbele kama kila kitu itaendelea kama ilivyo sasa
  • Kwa siku ya pili, waombe warejee kwenye semina wakiwa na vitu vyao vitatu vyenye thamani kwao,pamoja na changamoto au matatizo amabayo inahatarisha au inaweza kuhatarisha vitu hivi (k.m. mdudu maalum, uhaba wa maji n.k.) ,

Thamani kuu

Thamani za shirika zinaweza kuwa za aina mbali mbali, kwani thamani inaweza kutofautiana kulinana na kila mjumbe. Hivyo ni muhimu kuweka kipaumbele ya thamani ambayo inakubalika na kikundi kizima kuwa ni muhimu.

Lengo: kuwasaidi wahudhuria kutambua ni thamani zipi ni muhimu kwa shirika lao kwa ujumla.

Mahitaji: karatasi, peni, makapen, na gundi ya karatasi

Muda unaohitajika: Saa moja hadi masaa mawili

Utaratibu:

  • Waombe wahudhuria kukumbuka vitu vyao vitatu walivyokuwa wamevifikiria mwishoni mwa siku ya kwanza.
  • Wakiwa wamejipanga watu wawili wawili, wabadilishane mawazo juu ya mbinu zao na sababu za kuchagua hivyo. Wajadili mbinu zao na pamoja wapunguze mbinu hizo zisizidi vitu vitatu vya muhimu kwao wawili.
  • Makundi haya ya watu wawili yakiwa tayari, waunganishe watu wanne wanne. Omba kila kikundi kurudia zoezi hili, ikiwa kila kikundi cha watu wawili kikijieleza kwa kikundi kingine cha watu wawili, na kama kikundi cha watu wanne, waamue juu ya vitu vitatu tu.
  • Unganisha makundi haya ya watu wanne kwenye makundi ya watu wanane na zudia zoezi. Baada ya hapo waunganishe kwenye makundi ya watu 16 na kadhalika hadi linabaki kundi moja tu.
  • Mwishoni kabisa, liombe kundi zima liwakilishe thamani zao tatu za ujumla na sababu za kuchagua hivyo. Pitia thamani ambazo ziwekwa kando. Uliza maswali kama “Mliamua vipi khusu hili?”, “Je, kulikuwa na mabishano yoyote makubwa?”, na “Mlifanyaje palipokuna na mabishano juu ya thamini kuu kwenye shirika lenu?”

Orodha ya matatizo

Ni muhimu wakati wote kuwapa wazallishaji nafasi ya kutambua matatizo na kufukia ufumbuzi wao wenyewe. Kuorodhesha matatizo kwenye karatasi ni njia rahisi lakini yenye ufanisi ya kuwasaidia wahudhuria kutambua na kufafanua kwa upana zaidi maswala yanayowapa wao na shirika lao changamoto zaidi.

Lengo: Kupanga kwa ufanisi matatizo na changamoto za shirika.

Mahitaji: karatasi na makapen

Muda unaohitajika: Nusu saa hadi saa nzima

Utaratibu:

  • Orodha ya matatio inaweza kutayarishwa kwa njia nyingi tofauti. Inaweza kutayarishwa kutokana na vyanzo vingi, ikiwemo mikutano, majadiliano ya vikundi na mt mmoja mmoja, mazoezi ya vikundi vidogo, matembezi au michezo ya maigizo. Orodha inatakiwa ibaki na shirika na kupitiwa mara kwa mara ili kuongeza taarifa wakati wote wa mchakato.
  • Kutokana na majadiliano ya siku ya kwanza, waombe wahudhuria wataje matatizo waliyoyatambua ambayo yanahatarisha thamani zao muhimu.
  • Nukuru matatizo na changamoto zote zinazotajwa.
  • Waombe watambua matatizo makuu matatu watakayotambua kama kikundi u
  • Weka alama kwenye matatizo na thamani ziliyochaguliwa na wote na bandika orodha hii ionekane na wote. Jaribu kuwa maalum iwezekanavyo.

Mti wa matatizo

Uelewa mzuri wa tatizo ni muhimu ili kuitafutia sululisho fanisi. Mti wa matatizo (tathmini ya sababu kuu) inwezesha wazalishaji kutambua sabau na athari ya tatizo. Ni muhimu kuwa na mtazamo mpana wa sababu zote zinazochangia tatizo ili kuepuka kuwa na dhana ya kuwa imesababishwa na mabadiliko ya tabia nchi.

Lengo: Kuchunguza kama matatizo yaliyopewa kipaumbele yanahusiana na mabadiliko ya tabia nchi au la.

Mahitaji: makaratasi ya flipchart na kalamu za rangi (makapen)

Muda unaohitajika: Masaa mawili

Umbo la 33: Mti wa matatizo
mchoro wa mti unaoonyesha sababu za uhaba wa maji

Utaratibu:

  • Kama mfano, tumia mojawapo ya orodha ya matatizo kutoka zoezi la awali, na fafanua kwa uwazi nini ni 'matatizo' ipi ni 'sababu' na ipi ni 'athari'. Wakilisha mti ukiwa na majani kwenye mchoro wa mfano. Kwenye shina la mti, ndiko yataandikwa matatizo. Eleza kuwa mti waku umeugua na onyesha matatizo yanayoathiri mti. Eleza kuwa miti huugua lutokana na matatizo yaliyo kwenye mizizi, ambako mti unapata chakula chake. Eleza kuwa, ili kuelewa kwa nini mti umeugua, tunahitaji kufwata ugonjwa hadi chanzo chake kwenye mizizi. Waruhusu wahudhuria nafasi kujadili na kufikiria sababu zinazoweza kusababisha tatizo hilo kwa kuwauliza “kwa nini?” Chora mzizi kwa kila sababu na andika sababu kwenye mzizi huo.
  • Rudia tena swali “kwa nini?” kwa kila sababu iliyotajwa ili kutambua sababu za pili. Zianfike hizi ngazi ya chini ya mizizi, chini ya sababu kuu za kwanza ambazo zilishatambuliwa. Waruhusu wahudhuria kuendelea na zoezi hili hadi hapo watakaposhindwa kutambua sababu zaidi.
  • Waombe watambue athari au matokeo ya tatizo kwa kuuliza “Nini ilitokea?” Chora tawi kwa kila athari na andika athari inayotajwa kwenye tawi.
  • Kwa kila tawi, rudia swali “Nini Ilitokea?” ambayo itaonyesha kuna athari za pili. Ziweke hizi kwenye matawi yaliyo juu ya matawi makuu ya kwanza. Waruhsu wahudhuria kuendelea hadi hapow atakaposhindwa kutambua athari nyingine.
  • Baada ya zoezi hili, wape kila kikundi (yawe makundi tatu hadi nne, kulingana na idadi ya matatizo yaliyotambuliwa kuwa ni makuu hapo awali) tatizo moja kutoka orodha ya matatozo yaliyowekewa kipaumbele, na waombe wafuate utaratibu huu wa kutambua sababu kuu ya matatiro na athari kwa uzalishaji, na hivy kwa maishio yao.
  • Baada ya vikundi kukamilisha miti yao ya matatizo, waombe wawakilishe michoro yao kwa kikundi kizima na kujadili.
Figure 34: Sunray exercise
a diagram of the irrigation system with a smiling sun in the center

Zoezi la Mishale ya Jua

linaruhusu kufikiria ufumbuzi wa matatizo kwa njia ya kufwata utaratibu na mantiki, na kugawanya ufumbuzi huu kwenye shughuli zinazoweza jutekelezwa. Jina la zoezi hili linatokana na namna ya kuwakilisha matokeo, inayofanana na jua na mishale yake.

Lengo: Kugawa matatizo na kutayarisha sululisho. Inaweza kutumika kama zoezi la mti wa matatizo.

Mahitaji: Karatasi, kalamu za rangi na kadi ndogo za kubandika.

Muda unaohitajika: Saa moja hidi masaa mawili.

Utaratibu:

  • Unda makundi yale yale kama iliyokuwa kwenye zoezi lililotangulia
  • Gawa picha ya jua, likiwa na tatizo kuu limeandikwa katikati, kwa kila kikundi.
  • Omba vikundi wafikirie na kujadii miongoni mwao na kupata masululisho ya jumla yatkayohitajika kutatua matatizo makuu. Andika masululisho kwenye kadi ndogo za kubandika na zibandike mwishoni mwa mishale ya jua (au jaandike moja kwa moja kwenye karatasi ya flipchart).
  • Waombe wanavikundi kufikiria jinsi gani kila sululisho lililo mwisho wa mishale ya jua linaweza kutatuliwa. Andika majibu yao kwenye karatasi lingine na weka kwenye mchoro wa mishale ya jua, chini la sululisho. Ongeza mishale kama inahitajika.
  • Kutotofautisha kama kikundi kimetambua shughuli kubwa au zenye uzito, zigawanye zote katika shughuli ndogo ndogo kwa kuongezea mawazo ya ziada yasiyo tayari kwenye mchoro. Endelea kuifanyia kazi mpaka hapo uwezo wote umefikiriwa.
  • Hakikisha kila mshale wa jua unaishia na sululisho kamili kwa kila tatizo. Ondoa kile kisichohitajika na ongeza sululisho jipya panapohitajika. Panga upya maswala yote kama hii itahitajika (hii ndiyo sababu kuu ya kutumia kadi ndogo za kubandika).
  • Mteue mtu mmoja kutoka kila kikundi kuwasilisha picha ya mwisho ya mishale ya jua kwa wenzake.

Tathmini ya Mbinu za makabiliano

Shughuli hii inawasaidia wazalishaji kuamua juu ya upana wa shughuli zinazotatua mabadiliko ya tabia nchi. Cha muhimu kabisa kwenye shughuli hii ni utayarishaji wa Jedwali la mbinu. Kwenye safu wa mwisho upande wa kushoto wa Jedwali, orodhesha maswala ya athari (k.m. mmomonyoko wa ardhi, maua kupuputika, n.k.). Acha safu iliyobaki kwa ajili ya kuorodhesha vitendo (au mbinu) vya kutatua mabadiliko ya taboanchi. Shirika litatathmini kufaa kwa kila sululisho linalowezakena.

Lengo: Kuwasaidia wazalishaji kuamua ni vitendo vipi wataamua kufanya ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

Mahitaji: Jedwali (lisilojazwa) la kutathmini mbinu, na peni.

Muda unaohitajika: Lisali moja

Utaratibu:

  • Eleza lengo la shughuli na unda makundi kama yalivyokuwa awali
  • Onyesha Jedwali la Jedwali la kutathmini mbinu na eleza jinsi gani kulitumia.
  • Andika matatizo yaliyotambuliwa (athari za mabadiliko ya tabia nchi) kwenye safu wa mwisho upande wa kushoto.
  • Jadili sululisho zinazowezekana kwa kila shughuli lililotambuliwa kwenye zoezi la mishale ya jua na ziandike kwenye Jedwali.
  • Waombe wanakikundi kupitia sululisho zao na kujadili uwezekano au ufanisi wa kuzitekeleza. Kila kikundi linahitaji kujaza Jedwali la tathmini ya mbinu (inashauriwa kuwa nakala zinakuwa zimetayarishwa kabla ya kuanza shuhuli hii).
  • Eleza kuwa maswala yanaaswa yapewe uzito. Kama kitendo kinaonekana kufaa kwa tatizo, iwekwe alama ya '+' kwnye mraba wake. Kama tendo halielekei kufaa maka sululisho basi iwekwe alama ya '-' kwenye mraba wake, na kama haifahamiki kama itafaa, weka alama ya '?'. Maelezo au taarifa maalum juu ya jinsi gani sululisho hili litafanya kazi ziandikwe kwene mraba au kando ya Jedwali. Kufaa kunaweza pia kupewa uzito wa sana, wastani, au kidogo. Waombe wahudhuria kueleza sababu zao za kuamua mbinu zao, kwani maza nyingine mbinu zinaweza kuwa zimetumika miaka ya nyuma na wahudhuria wameshaona ufanisi wake.
  • Waombe kila kikundi kuwakilisha tathmini na ushauri wao. Mwoshoni mwa kila uwasilishaji jadili matokeo na kikundi kizima.
  • Nukuru vitendo vinavyokubaliwa na wote mwisho wa zoezi. Muda ukuruhusu, rudia hatua hizi kwa maswala mengine yaliyotambuliwa.
Jedwali 24: Mfano wa Jedwali ya tathmini ya mbinu

Changamoto

Mbinu la makabiliano

Ufanisi

Chini

Wastani

Juu

Uhaba wa maji

Tayarisha mpango wa matumizi ya maji

-

Pata matenki ya maji

?

Kushambuliwa na wadudu

Mafunzo ya mbinu mbadala wa kudhibiti wadudu

+

*Tathmini hii ni mfano tu na haitoi ufanisi halisi kulingana na shughuli zilizoorotheshwa

Muhtasari wa matokeo

Lengo: Kufanya muhtasari wa matokeo ya semina na kutayarisha pendekezo la mbinu la utekelezaji wa mbinu za makabiliano yaliyotambuliwa.

Mahitaji: Karatasi (ya ukubwa wa bodi ya ukutani) iliyo na vigezo vya Jedwali la muhtasari, na makapeni

Muda unaohitajika: Saa moja

Utaratibu:

  • Jadili vitendo vilivyoorodheshwa kwenye Jedwali la tathmini ya mbinu na kusanya shughuli nyingine zinazohitaji kutekelezwa kwa kila mbinu (shuguli zinazoorodheshwa hapa hazihitaji zifwate mtiririko wowote maalum). Wahudhuria watambue shughuli hizi kwa undani iwezekanavyo, huku wakifikiria kila hatua itakayohitajika kwenye utekelezaji. Waombe pia wafiirie juu ya rasilimali zitakazohitajika (ikiwemo pia rasilimali watu) kwa kila shughuli.
  • Waombe kikundi kuorodhesha vitendo vyote kwa kipaumbele. Kulingana na umbo la kikundi, inawezekana ikawa rahisi zaidi kwa kupanga orodha ya kipaumbele wakiwa bado kwenye vikundi vidogo halafu kuwakilisha hii kwa wengine.
  • Waombe wahudhuria wote kupitia na kutathmini vitendo vyote vilivyoorodheshwa. Wakikubaliana juu ya kila kitendo, kiingize kwenye jendwali la muhtasari hapo chini (Jedwali la 25).
  • Rudia hatua hizi kwa kila kitendo kilichotambuliwa na kuorodheshwa kwa kipaumbele.
  • Eleza kuwa Jedwali hili la muhtasari na matokeo yake yanaunda kifaa kikuu cha tathmini ya maswala ya mabadiliko ya tabinachi kwa ukanda huo maalum.
Jedwali 25: Mfano wa muhtasari wa matokeo ya Semina ya Mabadiliko ya Tabia Nchi

Athari za Mabadiliko ya tabia nchi

  • maua kudondoka kutokana na ukame na joto kali

Mbinu la makabiliano

  • miundo mbinu ya umwagiliaji

Bidhaa inayotarajiwa

  • Mashamba mfano matatu yaliyo na miundo ya umwagiliaji
  • Wakulima 50 kwa kila matembezi shambani

Shighuli

  • Tayarisha ramani na vipimo vya kiwanja
  • Anzisha viwanja vya majaribio
  • Ufwatiliaji wa viwanja
  • Warsha ya mafunzo: kutembelea viwanja vya majaribio na kukagua mavuno

Mtu anayewajibika

  • Afisa Ungani

Muda

  • Oktoba 2014 had Aprili 2015

Rasilimali zinazohitajika

  • Ardhi inayofaa kwa kiwanja cha majaribio
  • wakulima watatu wa kujitolea
  • mfumo wa maji