Kusanya taarifa toka kwa wadau
Muhtasari
wataalamu wa ndani, kama vile waajiriwa wa mashirika na makampuni yanayotoa huduma za ugani, kwa kawaida wanakuwa na ujuzi wa kina juu ya mifumo ya uzalishaji wa kahawa, wakulima husika na hali yao, pamoja na changamoto kuu zinazitokea. Kwenye mahojiano au mikutano ya ana kwa ana, wadau hawa wanaweza kutoa taarifa muhimu juu ya athari zinazotokana na hali ya hewa, pamoja na mbinu mbali mbali za makabiliano.
mikutano au mahojiano na wadau (hasa wataalamu wa maeneo hayo)
- utambuzi wa athari kwa kilimo cha kahawa na ustawi wa wakulima zinazosabaishwa na hali ya hewa;
- utambuzi wa baadhi ya kinga kutokana na mazoea au utafiti
Nadharia
Lengo kuu la mikutano au mahojiano haya ni kugundua jinsi gani wataalamu hawa wameona athari za mabadiliko ya tabia nchi kwa mazingira yao, na kuangalia kama wana mawazo yoyote juu ya jinsi kuyatatua.
Mahojiano yanatakiwa kuwa na mpangilio wa kiasi, yakitumia maswali kama yafuatayo:
- Je, umegundua mabadiliko yoyote kwenye hali ya hewa ya ukanda wako kwa miaka 20 hadi 30 iliyopita? Kama nyido, ni lini mabadiliko haya yalianza kutokea? Je, umegundua mabadiliko ya mvua au joto kwenye miezi au misimu maalum? Kumwekuwa na mabadiliko kwenye misimu ya uzalishaji?
- Nini ni athari za mabadiliko ya tabia nchi zinazotarajiwa kwa ukanda huu?
- Nini itakuwa matokeo kwa uzalishaji wa kahawa? Mabadiliko haya yatakuwa na maana gani kwa wakulima wa kahawa na hususan kwa wakulima wadogo wadogo?
- Wakulima wanaangalia vipi mabadiliko ya tabia nchi na athari zake kwenye mashamba yao ya kahawa?
- Nini ni ushauri wako juu ya makabiliano na mabadiliko haya?
Kikwazo kikuu cha mikutano hii inaweza kuwa upungufu wa muda wa kutosha kwa upande wa wanaohojiwa (angalian “Kujifunza kutokana na uzoefu: Mikutano ya wadau au Mahojiano ya ana kwa ana?” hapo chini). Hii ikitokea, mahojiano ya ana kwa ana yanaweza kuwa njia nzuri ya mbadala, badala ya mikutano au semina. Andaa mpangilio rahisi wa mahojiano ambao utakusaidia kuwa thabiti na kunukuru kwa kutumia vigezo.
Mwongozo wa Vitendo
Lengo
- Kujifunza jinsi gani wadau tofauti wanadhani juu ya athari za mabadiliko ya tabia nchi kwa ngazi ya kienyeji na mawazo waliyokuwa nayo juu ya kukabiliana nazo.
- Kujumuisha ujuzi wa wataalam wa kienyeji kama pembejeo ya thamani kwa tathmini ya changamoto za mabadiliko ya tabia nchi
Matokeo tarajiwa
Muhtasari wa athari za mabadiliko ya tabia nchi kwa uzalishaji wa kahawa, na orodha ya mbinu zinazofaa kwa makabiliano.
Muda unaohitajika
Kulingana na utakavyotekeleza mahojiano, kama mkutano au kwa mkulima mmoja mmoja.
Mahitaji
Ubao wa flip chart na karatasi zake, peni za rangi tofauti (jumla ya ishirini hivi), kadi ndogo za karatasi, karatasi ya gundi na kazi za majina.

Mwongozo wa maswali kwa mahojiano ya wadau au mkutano:
- Je, umeona mabadiliko yoyoteya tabia nchi kwenye ukanda wako (mikondo ya mvua na jotoridi) kwa muda wa miaka 20 hadi 30 iliyopita? Kama ndiyo, tafadhali eleza zaidi.
- Je, kumetokea matukio iliyokidhiri kwa miaka ya nyuma? Ni matukio gani na mara ngapi?
- Ni kwa njia gani mabadiliko haya yameathiri uzalishaji wa hapo wa kahawa?
- Wakulima wanadhania nini juu ya mabadiliko ya tabia nchi na athari zake kwa mashamba yao ya kahawa? Kumekuwa na mabadiliko yoyote kwa misimu ya uzalishaji?
- Mabadiliko haya nana maana gani kwa wakulima wadogo wadogo wa kahawa? Ina matokeo gani kwa uzalishaji wa kahawa?
- Kumekuwa na mabadiliko ya tabia ya ukulima, labda kutokana na hali ya tabia nchi kubadilika?
- Nani anaathirika zaidi na utofauti wa tabia nchi (wanaume, wanawake, wavulana au wasichana) na ni kwa njia gani wanaathirika?
- Zipi ni athari zinazotarajiwa za mabadiliko ya tabia nchi kwa ukana huu?
- Nini ni ushauri wako wa kukabiliana na mabadiliko haya?
- Je, kuna mvutio wowote wa kujifunza zaidi juu ya changamoto hizi na mbinu mbali mbali za mwitikio?
Utaratibu
- Tayarisha ramani ya wadau: tambua wataalamu wenyeji kama vile wakulima wa kahawa, au maafisa ugani au waajiriwa wa wanunuzi wa kahawa, walio na ujuzi wa kina juu ya mifumo ya uzalishaji wa kahawa kwa ukanda maalum. Tambua pia changamoto kuu.
- Fanya mahojiano ya ana kwa ana, na/au mkutano rasmi wa wadau wa kahawa wa ukanda (kwa nusu siku au siku nzima).
- Ukipanga mkutano wa wadau, wape wahudhuria maelezo kwa ufupi juu ya mchakato wa c&c na changamoto za mabadiliko ya tabinachi.
- Unaweza pia kuunda makundi madogo madogo wakati wa mkutano ili kujibu maswali (angalia mwongozo wa maswali kwa mahojiano na wadau au mikutano hapo chini), au kusanya majibu kwa kupitia zoezi la kufukiria na kujadili (k.m. kila mhudhuria aandike jibu la kila swali utakalouliza kwenye kadi tofauti).
- Jadili majibu na kikundi kizima na waombe wahudhuria wote wafikie muafaka juu ya changamoto kuu.