Chagua mbinu la makabiliano linlofaa zaidi
- mkutano wa wadau kwa ajili ya kuorodhesha makabiliano kwa kipaumbele
- warsha na wakulima
kuchakua na kuorodhesha kwa kipaumbele mbinu za makabiliano kwa sehemu husika
Hatua ya 3 inakazania mbinu zinazofaa zaidi kwa hali maalum ya kienyeji na matayarisho ya mpango wa utekelezaji kwa kutegemea matokeo ya tathmini na orodha ya mbinu za makabiliano yanayowezekana yaliyotambuliwa katika Hatua ya 2.
Wiki moja hadi mwezi mmoja.
Mchakato wa uchaguzi ufanyike kwa pamoja na wadau muhimu wa kahawa (k.m. kwenye mkutano wa wadau) kwenye sekemu au ukanda husika. Wadau wanaweza kuchangia sana kutokana na uzoefu wao, kujuzi na uelewa wa mazingira ya kienyeji, na uhudhuio wao unaweza pia kuongeza uhamasisho wa maswala ya hali ya hewa na kuchochea wakulima kumiliki vitendo. Pia ni muhimu kutambuakuwa kufanikiwa au kushindwa kwa mbinu la kabiliano inaweza kusababishwa na jinsi ilivyotekelezwa na kutokana na usawa wa mbinu hilo. Lazima wadau wa kienyeji watumie wajibu wao kwa kutafsiri usahihi wa mbinu kwa hali yao maalum ya kienyeji.
Mbinu zinazowezekana zinaweza kuwa za kubadilisha tabia za kilimo (k.m. kwa kuanzisha mazao ya kuanzaa) hadi kutatua maswala ya mazingira (kuanzisha mitambo ya uvuna maji ya mvua kwa ajili ya kumwagilia kahawa, au kubadilisha mazao ili kuhakikisha usalama wa chakula. Mpango wa c&c mpaka sasa umefanya kazi hasa kwa ngazi ya shamba ikikazania makabiliano ya kiufundi. Lakini ujenzi wa uwezo wa ukanda na makabiliano yaliyo nje ya shamba na kuingia hadi kwenye jamii ni muhimu vile vile.
Ukishacagua mbinu la makabiliano, unahitaji kutayarisha mpango wa utekelezaji ambao unazingatia hatua kamili za utekelezaji, pamoja na mahitaji na muda kwa kila shughuli. Ni kwenye hatua hii ambapo itakusaidia kutayarisha ‘theory of change’, yaani njia ya mradi. Hii ni mbinu tu ya kukubali, kuelewa na kujarisha malengo, mantiki na dhana zinazoumba mbinu. Kulitambua mantiki hii itakusaidia pia kutayarisha alama za kuchunguza na kutathmini (M&E) mbinu ya makabiliano kuanzia hatua za mwanzo.
Kabla ya utekelezaji wa kikamilifu wa mbinu la makabiliano kwa kiasi kikubwa, ni muhimu kwanza kutathmini kufaa kwake kwa ngazi ya kienyeji (angalia hatua ya 4 kwa taarifa zaidi juu ya utekelezaji na tathmini ya mbinu za makabiliano).
Matokeo ya Hatua ya 3 yanatakiwa yawe orodha ya mbinu za makabiliano yanayofaa pamoja na mpango wa utekelezaji kwa ajili ya kujaribu na kutekeleza mbinu hizo. Hii inajumuisha pia ufafanuzi wa upana wa utekelezaji (mf. Kama masahihisho ya mbinu maalum yanahitajika au kama itawezekana kuitekeleza kwa kiwango kikubwa moja kwa moja) na mtiririko wa mambo ya kufanya. Masahihisho yanaweza kuwa baadhi ya shghuli, ikiwemo shamba mfano, wakulima kutembeleana, Shamba Dasara au mbin nyingine (angalia hatua ya 4).
Upande mwingine muhimu ni utayarishaji wa ramani ya mantiki au njia ya mradi ambayo itafafanua malengo, dhana na mantiki ya mbinu za makabiliano. Kwa kuwahusisha wadau maalum kwenye shighuli za masahihisho na utekelezaji, wanaweza kuwa na ufahamu juu ya hatua za makabiliano ambazo ziwepewa kipaumbele na kuanza kuanganzwa juu ya majukumu na mchango wao.
kuchakua na kuorodhesha kwa kipaumbele mbinu za makabiliano kwa sehemu husika
warsha ya kupanga pamoja na maafisa ungani, wadau na wakulima (si lazima)
mkakati wa utekelezaji na mpango wa ufuatiiaji wa utekelezaji wa mbinu za makabiliano ziliyochaguliwa
warsha ya wadau iliyosimamiwa na mwezeshaji