Muhtasari

Mbinu za makabiliano zikichaguliwa na kuwekewa kipaumbele, sasa ni muda wa kutayarisha mpango wa utekelezaji kwa ajili ya kusahihisha na/au kuzitekeleza. Timu yako inatakiwa kufanya uamuzi wa awali juu ya majaribio ya shambani na viwanja vya mfano n.k. baada ya hatua za matayarisho kukamilika. Lazima mpango wa utekelezaji ulingane na mahitaji na maingira ya hatua za makabiliano. Kwa kawaida, inatakiwa iwe na malengo kamili na utaratibu ulio rahisi kufwata wa kusahihisha na kutekeleza kila mbinu. Pia, unahitaji kuwa na viwango vya vya ubora, matokeo yanayotarajiwa, wafanyakazi na mahitaji mengine, muda wa utekelezaji na mchakato wa kufwatilia maendeleo (angalia mpango wa utekelezaji kwenye jedwali Na 12)

Mbinu

warsha ya kupanga pamoja na maafisa ungani, wadau na wakulima (si lazima)

Matokeo

mkakati wa utekelezaji na mpango wa ufuatiiaji wa utekelezaji wa mbinu za makabiliano ziliyochaguliwa

Nadharia

Kwa kuchangia uzoefu wao, utaalam na uelevu wa mazingira ya kienyeji, wadau wanaweza kufafanua mchakato wa utekelezaji.

Unganisha mbinu mbali mbali za makabiliano ili kuonyesha ufanisi wake wa kupunguza maswala ya athari maalum ya hali ya hewa. Hii inaweza kuwa pia ujenzi wa uwezo kwa kutoa mafunzo, mifumo ya kienyeji ya kupunguza wadudu, kilimo mseto, mbinu endelevu usimamizi wa udongo n.k. Ni haba sana kuwa mbinu moja itatatua changamoto zote za mabadiliko ya hali ya hewa.

Kigezo muhimu sana cha mpango wa utekelezaji ni mfumo wa M&E, ambao utakuruhusu kufwatilia mabadiliko ya uwezo wa makabiliano ya mfumo wa uzalishaji wa kahawa na maishio ya wakulima ikiwa ndio matokeao ya mbinu la makabiliano. Mwongozo kamili wa M& unapatikana kwenye Hatua ya 5.

Jedwali 12: Mpango wa utekelezaji kwa Chagu za Makabiliano (mfano)

Kihatarishi

Joto kuongezeka

Tokeo (tatizo)

miti ya kahawa kupata magonjwa zaidi, hasa kutu ya majani

Chagu za Makabiliano

Otesha aina sugu za kahawa chini ya ukanda wa meta 1300 juu ja bahari, tumia mbinu bora za kilimo kama vile kupogoa, usimamizi wa kivuli, kupulizia dawa kama kinga, na kuweka chokaa

Lengo

Kuteleza hatua dhidi ya ugonjwa wa kutu ya majani

Shughuli

Tambua kitaru cha kutotesha miche ya aina ya Catimor au Sarchio, changia gharama anzilishi

  • Endeleza Shamba Darasa (SD) tatu kwa jumla ya wakulima 75
  • Anzisha SD kwenye mashamba yaliyochaguliwa (shamba lionyeshe uiano kati ya upogozi mzuri, usimamizi wa kivuli, na unyuyishaji kinga)
  • Eleza ratiba ya masomo na kubaliana mpango wa mafunzo na wahudhuria
  • Anzisha mashamba mfano kwa ushirikiano na vitaru vya miche ili kulinganisha Catimors na Sarchimors na aina za kawaida zilizolimwa
  • Fundisha wazalishaji 75 jinsi ya kutambua mapema dalili za ugonjwa wa kutu ya majani na jinsi ya kutayarisha chokaa
  • Wafundishe upogozi mzuri, usimamizi bora wa kivuli, na upulizaji kinga kwa viwango vidogo
  • Fuatilia na jadili matokeo kwenye SD (kutana shambani mara moja kwa mwezi)
  • Tathmini pamoja na wazalishaji matokeo, gharama, kukubalika kwa mbinu, na muda wa usimamizi wa kutu ya majani
  • Kulingana na matokeo, panga mafunzo ya ziada ya kukabiliana na kutu ya majani
  • panga usambazaji wa miche ya Camitor na Sarchimor (miche itafadhhiliwa kwa awamu ya kwanza)
  • Panga utararishaji na usambazaji wa shokaa kwa kupitia kikundi cha wakulima

Alama za mafanikio

  • Shamba Darasa tatu zimenazishwa na zinakutana kwa mpangilio
  • wazalishaji 75 wamepata mafunzo na wana uelewa juu ya usimamizi wa kutu ya majani
  • Kutaru kimoja kinazalisha miche ya Catimors au Sarchimors
  • Miche 75,000 imesambazwa baada ya miezi 24 uu Kikundi kimoja cha wakulima kinatayarisha na kusambaza chokaa kwa makulima wake
  • Wakulima 75 wana mpango wa kudhibiti kutu ya majani, na wanaufwata
  • Makulima wote walio chini ya ukanda wa meta 1300 juu ya usawa wa bahari wamepanda aina ya kahawa inayostamili kutu ya majani kwenye mashamba yao

Majukumu

Afisa Ungani (1)

Muda

Mwezi mmoja baaad ya kahawa kuchanua, kwa kipindi cha miezi 24

Malighafi

Afisa Ungani kwa SD

Fedha kwa vifaa vya SD

Fedha kwa kuanzisha kitaru

Fedha kwa kufadhili usambazaji wa miche

Alama za mabadiliko shambani

Kwa wakulima waliofwata mpango wa kuepukana na ugonjwa wa kutu ya majani:

  • kiasi na ukali wa mlipuko wa kutu ya majani (kuliinganisha na wasiotumia mbinu hii)
  • uzalishaji wa kahawa kwa hekta (kulinganisha na wasiotumia mbinu hii)
  • Gharama za usalishaji kwa hekta (kulinganisha na wasiotumia mbinu hii)
  • Faida kwa hekta (kulingana na wasiotumia mbinu hii)

Kwa wakulima waliopanda miche inayostamili ugonjwa wa kutu ya majani

  • Kasi ya miti kufa (ndani ya miezi 12 baada ya kupandwa)
  • Gharama ya miche bila ufadhili (kulingana na miche isiyostamili)

Mwongozo wa vitendo

Mpango wa uendeshaji ni mchakato wa kina unaotumika kutoa picha kamili jinsi timu itakavyochangia kwenye masahihisho na/au utekelezaji wa mbinu za makabiliano zilizochaguliwa kufanywa mashambani.

Lengo

  • Kueleza kinaganaga mpango wa uendeshaji kwa kusahihisha na kutekeleza mbinu zilizochaguliwa za makabiliano.
  • Kuwahusisha na kuwashirikisha wadau wa pahala hapo.

In general, an operational plan addresses six main questions:

  • Where are we now?
  • What do we want to achieve?
  • What kind of steps do we need to take in order to achieve these goals?
  • What resources are required to meet these goals?
  • How much time do we need? uu How do we measure our progress?

Utaratibu

  • The operational plan should be prepared by the people who will be involved in implementation (project coordinator, extension staff, selected stakeholders, etc.).
  • Although there are no strict rules for the format of an operational plan, they normally contain the following information:
    • Clear objectives (goals)
    • Activities required for achieving these objectives
    • Desired output (deliverable product)
    • Indicators (quality standards)
    • Staffing (human resources) and resource requirements
    • Implementation timetables
    • A process for monitoring progress
  • If you include the validation or testing of new adaptation options within a local context in your operational plan, an extra work plan for the test plots should be elaborated. A description of the main issues you must consider for design, work plan and measurements of these test plots can be found under Step 4, “Validation of new adaptation options on local context”.
Jedwali 29: Maswali ongozi na mifano ya kuandaa mpango utekelezaji kwa baadhi ya mbinu

Athari

Zipi ni athari kuu za hali ya hewa zinazoathiri mifumo ya kilimo cha kahawa pamoja na wakulima? Zipi ni changamoto kuu? K.m.:

  1. Kuongezeka kwa pimajoto, mvua kali, ukame, upepo mkali.

Rejea matokeo ya Hatua 2 (kujaza athari kuu za mabadiliko ya tabia nchi na kuchagua makabiliano yanayofaa zaidi)

Tatizo

Yapi ni matatizo makuu kwenye mfumo wa kilimo cha kahawa yanayosababishwa na mabadiliko ya tabia nchi? Ni changamoto zipi kuu tunazotaka kuzitatua? K.m.:

  • Kudondoka kwa maua, kuongezeka kwa mashambulizi ya CBB au kutu ya majani, mmomonyoko wa ardhi

Mbinu za Makabiliano

Ni mbinu zipi tunazozingatia kwenye kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi? Ni mbinu za makabiliano zipi zilizochaguliwa katika Hatua ya 2 ili kuimarisha mifumo ya uzalishaji wa kahawa? K.m.:

  • kuotesha mimea ya kutandaa kwa kuhifadhi udongo, mitego kama sehemu ya njia mbadala dhidi ya wadudu, kuotesha aina ya kahawa iliyo sugu dhidi ya kutu ya majani

Lengo

Yapi ni malengo makuu tunayoyakusudia hasa kwa mbinu la makabiliano? K.m.:

  • Kujaribisha shambani aina ya kahawa iliyo sugu dhidi ya kutu ya majani ili kupunguza athari za ugonjwa wakati wa unyevu
  • Kujaribisha mazao ya kutambaa ili kuboresha uwezo wa kahawa kumudu ukame shambani
  • Kuhamasisha utumizi wa mitego ili kuboresha usimamizi wa CBB shambani

Inshara za mafanikio

Ni matokeo gani tunayotaka kuyaona? Ni muhimu kuyaeleza matokeo, kwani hii itaamua ni shughuli zipi zitafanyika na kwa kutumia mbinu gani. K.m.:

  • Shamba darasa 3 (wakulima 75) wajaribishe mazao ya kutandaa kwa ajili ya kuhifadhi unyevu kwenye udongo
  • Wazalishaji 50 wafundishwe kuchunguza CBB na usimamizi kwa kutumia mitego na watekeleze shambani
  • Majaribio manne ya aina ya kahawa iliyo sugu dhidi ya kutu ya majani

Zingatia njia ya mradi. Tafadhali orodhesha hapa matokeo ya moja kwa moja kutokana na shughuli utakazozifanya, pamoja na matokeo unayoyatarajia. Inshara za mradi zielezwe kwa uangalifu ili mafanikio yaonekane wazi. Inshara ziwe maalum, ziweze kupimwa, ziwezekane, na ziwe na muda (SMART)

Shighuli

Eleza shughuli zitakazohitaji kufanyika ili kufikisha malengo

Zingatia ipi ni mbinu bora ya kufundisha jinsi ya kutekeleza makabiliano

mbali na kusambaza mbinu zinazofaa za makabiliano kwa kupitia mafunzo, ni muhimu pia (hasa kwa mbinu mpya) kuzijaribisha kwanza kwa kiwango kidigo, kama vile kwenye shamba mmoja moja au kwenye shamba darasa

Kwa kawaida, shughuli za kufundisha (semina, matembezi shambani, n.k.) zinabuniwa kwa mbinu za makabiliano ambazo zinafahamika, na ambazo matokeo yake mazuri yanajulikana

Mfano: Shughuli

  • Tayarisha SD tatu zenye wazalishaji 75 kwa ajili ya kujaribia mazao ya kutambaa kwa malengo ya kuboresha unyevu wa udongo mashambani Shughuli ndogo ndogo:
    • Anzisha SD kwenye baadhi ya mashaba (shamba tatu zenye dalili ya ukame)
    • Fafanua mitaala ya masomo na kubaliana ratiba wa mafuunzo na wahudhuria
    • Pata mbegu za mmea wa kutandaa
    • Tayarisha ratiba
    • Chunguza matokeo ya mazao yanayotambaa kwenye mashamba ya kahawa
    • Chunguza udongo kabla ya kupanda mazao ya kutandaa na baada ya miaka 2 ili kuhakiki tofauti
    • Eleza vipimo na nukuru uchunguzi kwenye mazao na udongo
    • Nukuru shughuli zilizofanyika ili kuazisha na kusimamia matandazo (gharama)
    • Tathmini matokeo pamoja na wakulima kwa kufuata vigezo vya gharama, muda n.k.
    • Tayaraisha ripoti ya ripoti ya mafunzo ya utekelezaji wamimea ya kutandaa

Kwa mwongozo zaidi juu ya mpango wa kazi wenye maelezo zaidi, angalia Sehemu ya 2, Hatua ya 4 ya kitabu hiki (Uthibiti Shambani wa Mbinu ya Makabiliano”)

Mwenye majukumu

Fafanua kwa ukamilifu nani anahusika kwenye kila shughuli

Muda

Fafanua tarehe ya kuanza kila shughuli, na tarehe ya kutarajia kukamilisha, K.m.:

  • Mwezi mmoja baada ya kahawa kuchanua maua, kwa miezi mitano.

Mahitaji

Ni mahitaji gani (afisa ungani, fedha, mahudhurio ya wadau n.k.) yatakitajika ili kufikisha malengo?

Kuwa mhakika iwezekanavyo. Mashamba mfano yanahitaji ufuatiliaji mkubwa, na kukosekana kwa watu kunaweza kukwamisha kutimiza malengo.

Ishara za mafanikio ya mbinu la makabiliano shambani

Ishara hizi zitasaidia kujibu maswali kuhusu matokeo ya makabiliano shabani. Hii inaweza ikajaribiwa kwenye mashamba ya majaribio au kutathminiwa pamoja na wakulima waliotekeleza mbinu (angalia Hatua ya 4)

Maswali muhimu:

  • Yapi na matokeo ya manufaa yanayotarajiwa
  • Ni jinsi gani tunaweza kupima kama yametokea?

Upimaji (Mfano):

  • Idadi na kiwango cha ushambulizi wa kutu ya majani (kulingana na wasiotumia njia za makabilian
  • Kipato/Faida kwa hekta (kulingana na wasiotumia njia za makabiliano)
  • Kiwango cha kufa kwa mimea (miezi 12 baada ya kupanda)

Ishara hizi zinajenga msingi wa tathmini ya mashamba ya majaribio na tathimini ya mafanikio ya ripoti ya uchunguzi/utafiti

Jedwali 31: Mpango wa utekelezaji (mfano)

Hazard

Changing rainfall patterns, drought

Main challenges

Improve coffee resistance to increasing drought

Adaptation options

Training about climate change and coffee

Cover crops

Inoculation of coffee seedlings with myccorhiza

Use of Gypsum

unknown practices = need to be validated

Objectives

Deliver sensitization workshops (Climate Witness Workshop) to raise awareness about climate change

Promote native cover crops to protect soil against drought

Establish community coffee nursery with mycorrhiza

Validate Gypsum to improve drought resistance

Activities

  • Identification of community
  • One exchange visit to demo plots with adaptation options (shade, cover crops)
  • Four workshops (sensitization)
  • Establish four FFS
  • Identify useful native cover crops for coffee
  • Establish demo plots on FFS level and do follow-up
  • Define number of coffee plants per group
  • Select coffee variety and mycorrhiza
  • Establish coffee nursery and do follow-up
  • Promote planting of inoculated coffee plants on farms
  • Design of test plots uu Establish three test plots on three different farms (FFS)
  • Monitor test plots and keep records
  • Evaluate results uu Develop case study

Indicators of success

  • 100 farmers trained
  • 100 farmers trained
  • Four demo plots established
  • 80 farmers apply native cover crops well
  • Four community coffee nurseries established
  • 100,000 coffee plants distributed
  • 95,000 coffee planets planted by participants

Three test plots to study the use of Gypsum on coffee (two different doses and comparison)

Responsible person

Extensionist

Farmers and extensionist

Community and extensionist

Extensionist and farmers (FFS)

Time

Three months

Twelve months

Twelve months

Two years

Resources needed

Low

Low

Middle (seeds, nursery structure, Mycorrhiza, man power)

Middle

Indicators for on-farm effectiveness of adaptation option

N/A

  • oil moisture
  • Production costs per ha
  • Gross-margin per ha
  • Root development
  • Production costs per ha