Rudi
C

Utayarishaji wa mtiririko wa mradi wa Mabadiliko ya tabia nchi (TOC)

Muhtasari

Utayarishaji wa njia ya mradi wa c&cunaweza kusaidia sana wakati wa awamu za kupanga, kutekeleza na M&E za makabiliano.Mchakato huu mara nyingi unafahamika kwa jina lake lingine 'nadharia ya mabadiliko' ('theory of change') na ni kifaa cha kupangia na sehemu muhimu kwa marejeo ya

Mbinu

warsha ya wadau iliyosimamiwa na mwezeshaji

Matokeo
  • ramani ya sababu za mbinu na matarajio
  • Kufikiria mkakati wa utekelezaji na kuamua kama unawezekana na unafaa.

Nadharia

Njia ya mradi ni maelezo juu ya jinsi kikundi cha wadau wanavyotegemea kufikia lengo la jumla. Inasaidia kuiwekea mantiki mchakato wa utekelezaji, kuunganisha vitendo na matokeo, na kuwasilisha dhana zitakazoathiri maamuzi. Dhana hizi zinaeleza miungano ya kimantiki kat ya matokeo ya awali, ya kati na ya muda mrefu, na sababu gani shughuli zilizopendekezwa zinatarajiwa kusababisha matokeo haya. Ukitumia mfano wa Mradi wa Uendelezaji wa Ujasiri na Udhibiti wa Kutu (kwa kifupi PRPR) nchini Guatemala, hatua muhimu za kutayarisha njia ya mradi zimeelezwa hapo chini.

Mwongozo

Sharti la mwanzo inamaanisha sharti ambalo lazima litimizwe kabla shughuli nyingine zinaweza kutekelezwa.

Matokeo maana yake mabadiliko yanayotokana na utekelezaji wa shughuli (k.m. kuongezeka kwa ujuzi juu ya hatua za kuzuia kutu ya majani ni tokeo).kwenye njia yako ya mradi, kila tokeo ni sharti la mwanzo kwa linalofwata, k.m. lengo la jumla linaweza ufikika kama baadhi ya matokeo ya kati yatakuwepo, na matokeo haya ya kati yanaweza kutokea kama to matokeo ya awali yakitokea na kadhalika.

I. Fafanua matokeo au lenga lako la msingi

Kama vile unavyopanga safari ukiwa na picha ya mwisho wa safari kichwani mwako, mradi wako pia unatakiwa uanze na tokeo au lengo linalolengwa.

Mfano: lengo la muda mrefu la Mradi wa PRPR ni “wakuliwa wa kahawa wawe wastahimilivu zaidi dhidi ya matokeo ya kutu na wawe na uwezo mkubwa zaidi wa kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi.”

II. Tambua sharti la mwanzo linalohitajika ili kufikia lengo lako.

Hatua hii mara nyingine huitwa ‘backwards mapping’ kwani inakuhitaji utambue sharti la mwanzo zitakazohitajika ili kukamilisha malengo yako. Hii inakuhitaji kufikiria kwa kupiga hatua za kurudi nyuma, ukianza na lengo la muda mrefu na kuendelea malengo ya kati na kisha kufikia matokeo ya mwanzo na masharti yatakayohitajika. Hizi zinaweza kupangwa kwa mtiririko, kama njia.

Mfano: Ni mabadiliko yapi yanahitajika ili kukamilisha malengo ya Mradi wa PRPR? Nini ni masharti yatakayohitajika ili mabadiliko yaweze kufanyika?

Mchoro wa hapo chini unatoa maadhi ya mifano ya mashart ya mwanzo kwa hatua nne za Mradi wa PRPR. Mantiki kati ya hatua hizo ni wazi (mf. Ngazi ya 4 inaweza kufikiwa kama ngazi ya 3 ipo, ngazi ya 3 inafikiwa kama ngazi ya 2 ipo, na kadhalika, ukirudi nyuma kutoka lengo la mradi). Umbo Na 17 linaonyesha kuwa njia kamili ya mradi inatokana na vifungu matokeo na mashart ya utata zaidi.

Umbo la 16: Mfano wa masharti ya awali kwa tabaka nne tofauti za Mradi wa PRPR
mchoro unaoonyesha lengo kuu la wakulima wa kahawa

III. Tambua dhana

Haiepukiki kuwa uthitji kutayarisha dhana kwenye uchoraji wa ramani wa kinyume juu ya jinsi gani na kwa nini kila ngazi inataarifu ifuatayo. Kwa sababu miaka ya mbele hayana uhakika, ni muhimu kunukuru dhana hizi ili kuhakikisha kama bado zinafaa wakati wa utekelezaji hapo mbele. Utarahisishiwa ukifikiria kwa kutumia vigezo vya kuchagua makabiliano (angalia Hata ya 3)

  • Kukubalika
  • Uwezekano
  • Ufanisi
  • Unafuu/gharama
  • Majira /Dharura

Pamoja na dhana za njia, pia kuna kipengele cha kunukuru dhana kwenye mpango wa M&E (angalia Sehemu ya 2, Hatua ya 5).

Mfano: Kutokana na matokeo mawili yaliyoungana hapo chini, hapa unaona baadhi ya mifano ya dhana za njia ya mradi wa PRPR.

“Mpango wa mkopo mdogo wa kuwezesha upatikanaji wa fedha kwa vifaa” utasadidia “usambazaji wa miche kwa bei ya ruzuku” na pia kuboresha “upatikanaji wa zana na vifaa vinavyohitajika kuzuia kutu”. Dhana hizi zinaweza kuwa:

  • mpango wa mkopo unakubalika kiutamaduni
  • viwango vya riba vimepangwa kuwa kiasi kinachofaa na havitaongezeka
  • Wakulima wadhaifu (yaani, hawana mali na historia mbaya za madeni) wanaweza kupata mikopo
  • Bei za ruzuku za miche inaweza kumudiwa

IV. Tayarisha viashiria

Hatua inayofwata ni kutambua viashiria vitakavyoamua kama matokeo haya tofauti yanafikika. Mchakato wa uchinguzi unategemea uchaguzi wa viashiria ambavyo vitawakilisha mabadiliko kwa isahihi. Angalia kila tokeo kipekee na fikiria jinsi gani utapima maendeleo ya kulifikia kila moja. Mwongozo wa kina juu ya utayarishaji wa viashiria unapatikana kwenye kipengele cha M&E ukurasa wa 79. Jedwali Na 13 inaonyesha baadhi ya mifano ya viashiria vya Mradi wa PRPR.

Inawezekana kutumia viashria vya ujumla, kama vile kipato cha kaya, au asilimia ya matokeoya kutu ukandani. Ingawa ishiria hizi zina manufaa, ni vigumu zaidi kuzitumia kwa utekelezaji wa mbinu za makabiiano, hasa tukizingatia muda mrefu unohitajika kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

Kwa mfano, kumbukumbu za miaka mitatu za kutokuwepo kwa tukio la kutu si lazima iwe tokeo la hatua ya makabiliano iliyotekelezwa. Vile vile, kama tukio la kutu likitokea, si inshara ya kuwa hatua za makabiliano imefaulu. Hivyo, ingekuwa bora zaidi kupima kupotea kwa kipato kutokana na mlipuko wa kutu ukilinganisha na jamii ambazo hazijatekeleza mbinu za makabiliano.

V. Jenga njia

Baada ya hatua zote kukamilika, ziweke pamoja kwenye mchoro mmoja. Hii si lazima iwe kazi ya ufanisi sana, mchoro kutokana na mchakato wa kupanga utafaa tu. Labda unweza kuupiga mchoro picha kwa marejeo ya hapo mbele. Kumbuka kuwa njia ya mradi itahitaji kupitiliwa wakati wote wa utekelezaji wa mbinu za makabiliano. Kunaweza kuwa na sehemu laamumu ya kufanya hivyo, k.m. katikati ya mradi au baada ya kukamilisha awamu maalum.

Umbo la 17: Ramani ya njia ya mradi kwa mradi wa PRPR
mchoro unaoonyesha jinsi wakulima wa kahawa walivyo na uimara zaidi dhidi ya milipuko ya ugonjwa wa kutu ya kahawa na uwezo mkubwa wa kuhimili na kuzoea hatari za mabadiliko ya tabianchi
Jedwali 13: Baadhi ya Inshara za Mradi wa PRPR

Matokeo

Alma

Mbinu au Matatizo

Usimamizi bora wa kahawa (upogoleaji, kivuli, na kupulizia dawa kama kinga) unafuatwa

  • asilimia ya wakulima wanaotekeleza udhibiti wa kutu ya majani
  • Takwimu

Wakulima wanaweza kukakabiliana na mlipuko wa kutu ya majani haraka na kama ipasavyo

  • Asilimia ya wakulima walio na mpango wa kudhibiti kutu ya majani
  • Asilimia ya wakulima walio na uwezo wa kupata chokaa
  • Ni vigumu hadi hapo ugonjwa utakapijitokea, hivyo itabidi kubuni alama za kuonyesha utayari.

Wakulima wanachagua na kuotesha mbegu bora zilizo sugu dhidi ya kutu ya majani

  • Asilimia ya wakulima wanaokusudia kuotesha miche sugu
  • Asilimia ya wakulima walipanda miche sugu
  • Takwimu na mahojiano
  • Si wakulima wote watabadilisha miche yao wakati wa kipindi cha mradi, hvyo zingatia alama za kuonyesha maendeleo
  • Mahojiano yanaweza kueleza zaidi madhumuni ya wakulima

Wakulima wanaelewa jinsi mabadiliko ya tabia nchi yanavyoweza kuathiri kilimo cha kahawa kwa miaka ya mbele

  • Kudadisi hali ya ujuzi
  • Mahojino na mikutano na vikundi kabla na baada ya mafunzo

Wakulima wana uelevu mzuri juu ya kanuni muhimu ya kusimamia na kudhibiti uginjwa wa kutu ya majani

  • Kudadisi hali ya ujuzi
  • Mahojino na mikutano na vikundi kabla na baada ya mafunzo

Mpango unaofaa wa kufundisha wakulima umetayarishwa

  • Kudadisi hali ya ujuzi
  • Mahudhurio ya mafunzo
  • Idadi ya wakulima wanaotembelea shamba mfano kwa mwezi
  • Oanisha na dalili za matumizi ya ujuzi (k.m. asilimia ya wakulima wanaotekeleza hatua za kudhibiti kutu ya majani)
  • Tathmini za mafunzo
  • Vikundi maalum
  • Takwimu toka shamba mfano

Mfumo wa mikopo midogo umeandaliwa kwa ajili ya kutoa mikopo kwa matumizi ya mahitaju wa mradi

  • Kupata mikopo (hasa kwa vikundi duni)
  • Urejeshaji wa ikopo
  • Dalili za vifaa kupatikana
  • Takwimu/savey
  • Takwimu za mikopo
  • Mahojiano na vikundi maalum