Rudi
A

Chagua mbinu la makabiliano linlofaa zaidi

Muhtasari

Uchaguzi wa mbinu unatakiwa ufanyike wakati wa mkutano wa wadau ambamo waliohudhuria wanaombwa watambue ni mbinu lipi la makabiliano litawafaa zaidi kwa mazingira yao. Msingi wa mbinu zao utategemeana na vigezo vya tathmini, ikiwemo kukubalika kwa wakulima, uwezekano, ufanisi, unafuu na majira (angalia Jedwali Na 10 na case studies in c&c toolbox). Tathmini ya mbinu za makabiliano shambani ni zoezi tofauti ambalo ni sehemoya Hatua ya 4.

Mbinu
  • mkutano wa wadau kwa ajili ya kuorodhesha makabiliano kwa kipaumbele
  • warsha na wakulima
Matokeo

kuchakua na kuorodhesha kwa kipaumbele mbinu za makabiliano kwa sehemu husika

Nadharia

Jedwali 10: Maana ya sifa muhimu za uchaguzi

Kukubalika

Je, kumekuwa na upingamizi wowote ktoka kwa wakulima dhidi ya kukubalika kwa chago?

Uwezekano

Je, mbinu linawezekana kiutaalamu na kiufundi kwa mazingira hayo?

Matokeo

Je, shughuli zitakazofnyika na mbinu zitakazoteke lezwa zitafanikisha manufaa yanayolengwa kwa wakulima?

Gharama

Je, gharama za utekelezaji mzima wa mbinu ziko ndani ya uwezo wa wakulimana na kuendana na shughuli zao za kawaida?

Muda/Dharura

Je, muda wa kutekeleza mbinu unakubalika na wakulima? Je, muda wa kupata manufaa kutokana na mbinu unakubalika na wakulima?

Maswali ya mwongozo kwa kuchagua mbinu ya makabiliano

  • Kuna ushahidi gani kuwa mbinu hili la makabiliano ndilo linafaa kwa mazingira yako? Vyanzo vya ushahidi huu ni zipi?
  • Je, nini ni kiwango cha kuwezekana au kukubalika kwa cha mbinu inayopendekezwa kwenye mazingira ya kienyeji?
  • Je, nini ni kiwango cha ufanisi wa mbinu iliyopendekezwa kwenye kutatua changamoto zilizopo za mabadiliko ya tabia nchi? Kuna ushahidi gani?
  • Mbinu hili la makabiliano litakuwa na gharama gani? Je, wakulima wataweza kumudu gharama za makabiliano hayo?
  • Muda unaohiajika kati ya utekelezaji na matokeo kuanza kuonekana unawafaa wakulima? (Inawezekana utabidi kuwaelezea wakulima sababu za kuzingatia mbinu za makabiliano ya muda mrefu)

Unashauriwa kwanza kutathmini na kuweka kipaumbele mbinu zanazofaa pamoja na waajiriwa wenzako kwanza kabla ya kuwahusisha wadau kwenye majadiliano na uchaguzi. Unaweza kuzipanga mbinu za makabiliano zinazowezekana kwa kutumia jedwali ya maelezo ya jumla iliyotayarishwa mwisoni mwa Hatua ya 2 (Jedwali Na 8). Ukizipanga mbinu, hakikisha unazingatia maana kamili ya kila kigezo. Jedwali Na 11 intoa mfano wa jinsi gani matokeo ya jumla yanaweza kupigiwa hesabu.

Mbinu za makabiliano zenye maksi nyingi zaidi kwa vigezo vya ufanisi, uwezekano, kukubalika kwa wakulima, unafuu na majira ndizo za kutegemewa zaidi. Kwenye mkutano wa wadau, wakilisha matokeo awamu ya tathmani ya athari (Hatua ya 2) na wahimize wahudhuria kufikiria kwa ubinifu kila kipengele cha athari na pendekeza mbinu za makabiliano za ziada. Vigezo vya hapo juu ni msingi tu wa zoezi la pamoja la mpangilio wa kipaumbele, lakini ni bora kwanza kuzijadili na kuzikubali pamoja na wahudhuria kabla ya kupendekeza zoezi hili.

Semina hii inatakiwa pia kusaidia wadau kufikiri juu ya upana wa kila mbinu la makabiliano lililopendekezwa (angalia maswali ya mwongozo hapo chini). Zingatia taasisi zinazoweza kusaidi wakati wa awamu ya utekelezaji, pamoja na maswala ya kijinsia, upatikanaji wa kienyeji wa zana zitakazohitajika na uwezekano wa kupata fhedha.

Jedwali 11: Orodha ya mbinu za makabiliano sahihi (mfano)

Tokeo

(Tatizo)

Udongo kuporomoka kutokana na mvua kali

Kihatarishi: udongo kwenye mteremko haujafunikwa kutokana na matumizi ya dawa za kuua magugu

Kihatarishi: udongo kwenye mteremko haujafunikwa kutokana na matumizi ya dawa za kuua magugu

Mbinu shauri la makabiliano

Matandazo

Weed wiper

mimea ya kufunika udongo

Kukubalika/ Uwezekano (upande wa ufundi)

Juu (5)

Chini – Wastani (2)

inahitaji mafunzo na utaalamu kutumia, viguu kutumia kwenye mteremko

Wastani (3)

inategema upatikanaji kwa sehemu husika

Matokeo (upande wa ufundi)

Wastani - Juu (4)

matandazo yanalinda udongo vizuri, lakini lazima kutandazwa mara kwa mara

Wastani (3)

Matokeo yataonekana baada ya muda mfupi, lakini magugu yote yatakufa

Juu (5)

matokeo yataonekana hapo mimea itakapostawi

Kukubalika/ gharama (kwa wakulima)

Chini (1)

Matandazo hayapatikani kwenye mashamba ya kahawa, kuogopa moto kipindi cha kiangazi

Chini (1)

kifaa hakijulikani, utaalamu haujulikani, kifaa hakipatikani

Chini (1)

baadhi ya mimea inayodidimiza magugu hupatikana mashambani

Muda

Chini (1)

Matandazo yanapatikana lakini yana gharama

Wastani (3)

matokeo yanaonekana baada ya muda mfupi

Wastani (3)

matandazo yanahitaji muda mpaka yastawi vizuri

Jumla ya maksi = mbinu la kwanza

Jumla: 11

Shamba mfano

Jumla: 9

haitachaguliwa

Jumla: 13

tafiti mimea inayoweza kutumika

anzisha mashamba mfano matatu kwa mimea iliyochaguliwa

Maswali ya mwongozo kwa kufikiria mbinu zinazowezekana za makabiliano:

  • Ni shughuli zipi za makabiliano zimesha fanyika na wakulima. Je, inawezekana kuzirekebisha mbinu zilizopo kwa kuzingatia utabiri wa mabadiliko ya tabia nchi?
  • Je, inawezekana kutambua mbinu la 'kutojutia' (k.m. pendekezo zitakazomnufaisha mkulima kata kama matukio ya hali ya hewa hayatatokea kwa kipindi cha muda mfupi)? Mbinu za kutojuta zinatakiwa zifanye kazi vizuri kwa mazingira ya leo na pia kwa mazingira ya miaka ya mbele.
  • Ni aina gani za mbinu zizingatiwe? Hizi zinaweza kuwa za 'kutojuta' tu au za kujenga ujasiri wa muda mrefu ambazo zitahitaji mtaji mkubwa (k.m. ujenzi wa mtambo wa umwagiliaji). Zinaweza pia kuwa za kujenga uwezo au mbinu za kiufundi, mbinu zinazotatua maswala kwa njia ya moja kwa moya au zile zinazotatua changamoto za kiuchumi na kijamii zinazosababishwa na mabadiliko ya tabia nchi.
  • Je, mbinu zinaweza kufafanuliwa kwa njia iliyolegea ili kuruhusu kutokuwepo kwa uhakika (k.m. mbinu zitatambuliwa ambazo zinaweza kutekelezwa kwa kiwangokikubwa zaidi, siku za mbele, au kwa awamu ili kuruhusu viwango vulivyolegea vya kuitikia athari?). Je mbinu litafanya kazi kwa baadhi ya mandhari za mabadiliko za hali ya hewa?
  • Kuchelewesha pia ni mbinu mojawapo. Je, itawezekana au inashauriwa kuchelewesha utekelezaji hadi muda mwafaka zaidi (k.m. je ni fanisi zaidi kuanza kupanda aina mpya ya kahawa hapo miti iliyopo ikizeeka na kutoa mavuno madogo zaidi, ndipo yabadilishwe?). Nini ni athari ya kufanya hivyo?

Ukishakamilisha zoezi la uchaguzi pamoja na wadau, fananisha atokeo haya na matokeo ya tathmini yako ya ndani.

Mwongozo wa vitendo

Lengo

  • Kuchagua mbinu ya makabiliano inayofaa zaidi kwa kufanya mfumo wa ndani wa uzalishaji wa kahawa kuwa jasiri zaidi.
  • Kuwahusisha na kuwashirikisha wadau wa ndani kwenye mchakato wa uchaguzi

Matokeo tarajiwa

Orodha ya mbinu zinazofaa za makabiliano kwa ajili ya majaribio (masahihisho) au utekkelezaji kwenye hatua ya 4

Muda unaohitajika

Wiki moja hadi mwezi mmoja.

Mwongozo wa maswali

  • Ni mbinu zipi za makabiliano zinatumika tayari na wakulima? Hii ni chanzo kizuri ca ujuzi wa vitendo hai. Je, inawezekana kurekebisha mbinu zilizopo ili kuzingatia mabadiliko ya tabia nchi yaliyotabiliwa?
  • Je, mbinu za 'kutojuta' zinaweza kutambuliwa? K.m. ushauri unaowafaidisha wakulima hata kama tukio la tabia nchi (k.m. ukame wa muda mrefu) hautatokea kwa kipindi cha muda mfupi ujao. Mbinu za 'kutojuta' zilizopo zinahitaji kuleta mafanikio kwa hali ya tabia nchi ya sasa, pamoja na mifano yote ya tabia nchi ya miaka ya mbele.
  • Ni aina gani za mbinu zinapaswa kuchaguliwa? Hizi zinaweza kuwa mbinu za 'kutojuto' tu, au mbinu za kujenga ujasiri wa muda mrefu ambazo zinahitaji mtaji mkubwa (k.m. ujezi wa mtambo wa umwagiliaji).
  • Je, mbinu hizi zinaweza kufafanuliwa kwa njia inayoruhusu mabadiliko kwa urahisi ili kuruhusu utabili usio na uhakika (k.m. mbinu zitakazoweza kutekelezwa kwa kiwango kikubwa baadaye, au kutekelezwa pamoja kwa na kwa kufwatana ili kuruhusu viwango vitakavyobadilika vya mwitiko dhidi ya vihatarishi)?
  • Kuairisha pia ni mbinu mojawapo. Je, itawezekana au inashauriwa kuairisha kufanya uamuzi mpaka taarifa nyingi zaidi zitakapopatikana.

Utaratibu

  • Baada ya marudio ya kwanza ya ndani ya Jedwali la kupanga vihatarishi kwa orodha ya ushindi na mbinu zilizopo za makabiliano kama ilivyoonekana kwenye Hatua ya 2, panga mkutano wa maafisa ugani. Ikiwezekana, waalike wadau wengine husika kujadili hii tathmini ya awali ya vihatarishi vya tabia nchi (mf. Jeedwali la 28) na kufanya marekebisho.
  • Wavutie wadau na wataalam kutoa ushauri juu ya mbinu nyingine za ziada, na kuwekea vihaarisho na matatizo ya tabia nchi kipaumbele.
  • Kutokana na taarifa zilizokusanywa awali, tambua maoni ya nyongeza kwenye kutano huu. Hatua za makabuliano zinazofaa zinaweza kujaribiwa shambani na wakulima. Kumbuka kuwa tatizo (athari ya tabia nchi) moja linaweza kuwa na hatua kadhaa za makabiliano.
  • Kwenze uchaguzi wa mbinu ya makabiliano, zingatia vigezo kama ufanisi, uwezekano au kukubalika, kumudu gharama na muda muafaka kama misingi za yoeyi la pamoja la kupanga orodha ya ushindi (Jedwali la 27). Jadiliana na kubaliana vigezo va ziada vya uchaguzi pamoja na wdau wote wahusika kabla ya kuanza zoezi la kupanga orodha ya ushindi ya mbinu za makabiliano.
  • Kwa kila mbinu la makabiliano linaloshauriwa, sababu za kuchagua zitathminiwe kwa kufwata vipimo vilivyokwisha fafanuliwa awali vinavyoendana na kila aina ya sababu. Kwa mfano, sababu kama vile gharama, msaada wa wadau na kukubalika kwa wataalamu zinaweza kupimwa kwa kigezo cha kupendwa kama ifwatavyo: kidogo (1), kiasi (3) au sana (5). kwa vigezo kama ufanisi, tathmini ya ya kutumia viwango vya ukina zaidi vitahitajika. Mfumo wa kupanga sababu kwa orodha ya ushindi unatakiwa ukubalike na watakaofanya maamuzi na wadau kabla ya kuanza zoezi.
  • Mbinu za makabiliano zilizoshinda katika orodha hii ndizozitakuwa bora zaidi kutekeleza shambani.
Jedwali 28: Vigeo nyongeza vya uchaguzi

Vigezo

Maelezo kwa ufupi

Gharama

Gharama yakutekeleza mbinu za makabiliano au gharama bila kubadilisha mradi ulivyokusudia

Manufaa

manufaa ya mbinu la makabiiano kama sululisho kwa athari zinazotokana na mabadiliko ya tabia nchi (k.m. manufaa, uharibifu ulioepuka, gharama zilizookolewa, maisha ya watu yaliyookolewa)

Uwiano kati ya manufaa na gharama kwa kipindi kirefu

Kawaida, epuka makabiliano ya gharama kubwa; lakini ni muhimu kiyafikiria manuafaa na gharama kwa kipindi kirefu, kwani makabiliano huchukua muda hadi mafanikio kuonekana. Hivyo, zingatia gharama za utekelezaji lakini pia gharama zulizookolewa kwa kuepukana na athari za hali ya hewa

Urahisi wa kutekeleza

Inazingtia pia vizuizi vya utekelezaji na uhitaji wa kubadilisha sera ili kuruhusu makabiliano yafanyike

Kukubalika na wataalamu

Inawezekana kuwa mbinu zote za makabiliano zinafaa kiutaalamu, lakini si zote zinpendwa na wadau kutokana na sababu za kisiasa, kiuchumi, kijamii au kiutamaduni/ kimila

Kukubalika na wadau

Waamuzi wa baadhi za nchi watachagua makabiliano yaliyopendekezwa kulingana na jinsi yanavyoendana na mifano mizuri ya kitaifa

Muda

Muda wa kutekeleza mbinu la makabiliano unaruhusu manufaa bila kuongeza gharama

Inasaidia vikundi dhaifu

Vikundi vyenye uwezo mdogo kushinda vyote wana haja kubwa zaidi ya kuongeza uezo wao wa makabiliano. Unaweza kutambua vikundi vinavyodharauliwa na lutengwa, inayosababishwa kuwa dhaifu, kwa kuangalia baadhi ya mikutano ya ushauri na vikundi hivi.Pia zingatia vikundi visivyopewa nafasi ya kufanya maamuzi juu ya matumizi ya rasilimali muhimu ili kujiongezea uwezo wa kukabiliana na athari za hali ya hewa.

Inazingatia usawa wa wame na wake

Ni muhimu kutathmini kama mbinu la makabiliano linaweza kuwaongezea kazi na muda wakinamama. Mbinu lazima ziwarahisishei kazi na maisha wakinamama, na zisiingiliane na shughuli nyingine za kiuchumi au za kilimo wanazozifanya.

Matokeo kwa jamii

hii inamaanisha kuwa jamii kwa ujumla inaweza kuathirika na mbinu la makabiliano (k.m. asilimia ya wakulima wanaohudhuria mradi, ajira kwa watu, n.k.)

Uendelevu katika mabadiliko ya tabia nchi kwa muda mrefu

Hii inahakiki kuwa a tabia nchi ya muda mrefu yanazingatiwa kwenye muhtasari wa tathmini

Uwezo wa taasisi

Ni uwezo na ujuzi gani wa ziada unahitaji kuongezewa ili makabiliano yaweze kutekelezwa?

Idadi ya wanaonufaika

Je, kuna athari kutokana na makabiliano kwa hali ya hewa ya sasa? Baadhi ya mbinu zinaweza zikalengea hali ya hewa ya miaka ya mbele, lakini zina gharama na matokeo kwa muda huu.

Inafaa Hali ya hewa ya sasa

Mara nyingi, makabiliano yanayolengea yenyee manufaa madogo kwa watu wengi yanapendwa zaidi kuloko makabiliano yenye mafanikio makubwa kwa watu wachache.

Inafaa utamaduni

Mabadiliko yanayotokana na shughulli ngeni yanahitaji kuheshimu utamaduni ili yakubalike. Kinyume na hiyo, utaweza kuona kuwa mabadiliko hayafanywi na watu wengi.

Utoaji wa gesi ukaa

Uunganishaji wa mbinu mbili kati ya kupunguza kaboni na maendeleo ya ustahimilivu dhidi ya tabia nchi