Rudi
B

Jaribu na sahihisha mbinu mpya za makabiliano

Mwongozo wa vitendo

I. Uchaguzi wa eneo la shamba, uteuzi wa mkulima na mafunzo

Lengo

  • Kutayarisha viwanja vya majarabio kwenye mashamba na kwa hali ya SD kwa ushirikiano na wakulima kwa ajili ya kujaribisha mbinu mpy za makabiliano yaliyotambuliwa na wakulima awali kufaa kutekelezwa.
  • Kufanya majaribio yaliyo na yasiyo ya makabiliano (kwenye viwanja vya majaribio na viwanja vya kawaida).

Matokeo tarajiwa

  • Idadi nzuri ya viwanja (mashamba) vinapatikana kwa kutafiti mbinu kwa kushirikiana na wakulima.
  • Kaya za wakulima zinafundishwa mbinu mpya ya makabiliano.
  • Makubaliano ya wakulima au makundi ya wakulima (SD) kujaribu mbinu zilizopo za makabiliano kwenye mashamba yao.
  • Mipango iliyoandikwa na kutekelezwa kwa viwanja vya majaribio. uu Tathmini na upangaji wa matokeo (ya viwango na ubora).

  • Shughuli za marekebisho ya mbinu mpya za makabiiano lazima zifanyike kwa ushirikiano. Kufanya kazi na wakulima moja kwa moja ili kujaribia zana ni njia ya haraka ya kutambua kama kuna tabia zinazofaa kwa makabiliano kwa mazingira maalum, na vile vile kuweka wazi matatizo (k.m. zana zinaweza kuwa na gharama kubwa, ziwe ngumu kutumia, kuchukuwa muda mrefu kutekeleza au kutokuwa fanisi)
  • Manufaa ya majaribio mashambani ni: unaweza kupata maoni haraka kutoka kwa wakulima juu ya majaribio, kukubalika kwake na faida yake. Unaweza kujaribu zana kwenye mazingira tofauti kushinda kungetumia kituo kimoja ua viwili.
  • Hasara: huna maamuzi juu ya yatakayotokea, kwani wakulima wanaweza kukata tamaa mapema, au kutofanya majaribio kwa kufwata utaratibu uliokubalika.
  • Kama miundombinu inapatikana, ingefaa kuwa na mashamba ya majaribio yaliyosimamiwa kama inavyostahili, hawa kwa majaribio ya mawazo mapya au marekebisho ya mbinu zilizopo lakini ambazo pengine gharama zake ni juu sana au kuwa na vihatarishi kwa kujaribu na wakulima moja kwa moja.

Utaratibu

  • Tambua viwanja vya majaribio. Panapowezekana, chagua mikanda inayowaikilisha urefu mbali mbali kutoka na usawa wa bahari, hasa kwenye maeneo ambapo matatizo yameshatambuliwa kwa kupitia mbinu ya pembetatu (Hatua ya 2)
  • Nukuru sifa ya kila kiwanja kwa kufwata kanuni mbali mbali. Angalia Jedwali la mfano hapo chini na ongezea au kuirekebisha kama ipasavyo.
  • Unda timu ya mafundi wa shambani na/au maafisa ugani na wafundishe mbinu shirikishi za shambani.
  • Tafuta ushirikiano kutoka kwa wakulima na mashirika ya wakulima kwenye ukanda wako.
  • Toa taarifa kwa kupitia vipindi vya uhamasisho wa kaya za wakulima ambao wameamuwa kuhudhuia (k.m. semina za uhamasisho au semina ya shahidi wa tabia nchi)
  • Pale malighafi na muda zinaporuhusu, fikiria kutoa mafunzo ya upana zaidi ya kujenga uwezo wa makabiliano.

II. Muundo na mpangokazi za viwanja vya majaribio

Lengo

  • Kutayarisha muundo wa viwanja vya majaribio vilivyokubaliana na wakulima na mafundi kwa ajili ya kujaribisha mbinu z amakabiliano zilizopo
  • Kufafanua kwa undani shughuli zote, lini zitakapofanyika, na nani antakekuwa na wajibu kwa kila shughuli
  • Kuhakikisha kuwa muda na pahala pa majaribio zinaruhusu wanawake kuhudhuria kwenye shughuli

Utaratibu

  • Fanya mkutano wa kwanza pamoja na wakulima ili kufafanua malengo, kuchagua mbinu zilizopo, kuchagua viwanja vya majaribio na kupanga ratiba ya utekelezaji wa shughuli.
  • Tembelea viwanja vya majaribio ili kufanya uamuzi wa mwisho. Hakikisha kuwa kazi iliyopangwa na viwanja vilivyochaguliwa vinawakilisha matatizo yanayowakunba wakulima.
  • Eleza kwa undani umbo la mradi na andika mpangokazi kwa kila kiwanja cha majaribio ya makabiliano (Jedwali za 32 na 33)
  • Fafanua kwa uwazi matokeo tarajiwa – yaani nini inatarajiwa kutokana na mbinu ya makabiliano (k.m. tija bora, usugu dhidi ya ukame, usimamizi fanisi dhidi ya wadudu waharibifu n.k.)?
Jedwali 33: Maelezo juu ya majaribio na mkakati wa vipimo kwa kutathimin mbinu mpya za makabiliano

Athari

Ukame

Hatari

Miche ya kahawa huwa na mizizi dhaifu

Madhara/ Matokeo

Miche mingi hufa wakati wa kuhamisha shambani

Malengo

Tathmini utumiaji wa Mycorrhiza na Trichoderma kwa kuboresha kukua kwa mfumo wa mizizi na kupunguza kufa kwa miche kwenye shamba maalumu

Aina za matibabu

Tiba A

Weka Mycorrhiza kwenye mbegu chipukizi (sawa na gramu 5 kwa mmea)

Tiba B

Weka Trichoderma (gramu 28 kwa mita moja ya mraba)

Tiba C

Bila kuweka chochote

Study design

(number of plants, repetitions, etc.)

  • Mbegu kwenye mchanga : sentimeta 20 kwa 20
  • Mychorrhiza: gramu 5 kwa mmea
  • Kitaru cha miche 200
  • Mifuko/Viroba kwa Kitaru
  • Udongo: mbolea ya maganda ya kahawa (1:1)
  • Mbegu kwenye mchanga : sentimeta 20 kwa 20
  • Trichoderma: gramu 28 kwa mita moja ya mraba uu Kitaru cha miche 200
  • Mifuko/Viroba kwa Kitaru
  • Udongo: mbolea ya maganda ya kahawa (1:1)
  • Mbegu kwenye mchanga : sentimeta 20 kwa 20
  • Trichoderma: gramu 28 kwa mita moja ya mraba
  • Kitaru cha miche 200
  • Mifuko/Viroba kwa Kitaru
  • Udongo: mbolea ya maganda ya kahawa (1:1)

Mpango wa jaribio (idadi ya mimea, marudio, n.k.)

Mwezi wa 1:

  • Andaa vifaa kwa kuotesha mbegu
  • Safisha udongo wa kuoteshea mbegu
  • Ambukiza/Chanja udongo na Mycorrhiza au Trichoderma; Tiba C bila kuambukiza

Panda miche kwenye vitalu Mwezi wa 2 na wa 3:

  • Mwagilia miche
  • Tayarisha udongo wa kuoteshea na jaza kwenye viroba
  • Pandikiza miche kwenye vitalu

Mwezi wa 4 hadi wa 7:

  • Mwagilia na ondoa magugu
  • Weka mbolea
Jedwali 34: Ufuatiliaji wa kiwanja cha majaribio; ishara na vipimo

Mbinu la Makabiliano

Myccorhiza na Trichoderma

Malengo

Kutathmini matumizi ya Mycorrhiza na Trichoderma kwa kuboresha uoto wa mfumo wa mizizi na kupunguza kufa kwa miche wakati wa kupandikiza shamba maalumu

Ishara ya mafanikio shambani

Uoto wa mizizi

Gharama

Maelezo ya vipimo

Urefu wa mzizi mkuu

Uzito wa mizizi

Uwingi wa miche inayofyonza maji

Nakara

Kifaa cha vipimo

Urefu (sentimeta)

Gramu

Kuangalia: picha

zana na kazi

Idadi ya vipimo

Miche (kila miezi 2)

Kitalu cha kahawa (kila miezi 4)

Kumalizia kutalu

Kila mwezi

Kila mwezi

Mwenye majukumu

Afisa Ungani na Wakulima

III. Mwanzo na uchunguzi wa viwanja vya majaribio

Kabla ya kuanza majaribio shambani, angalia kama viwanja vilivyochaguliwa vinakidhi mahitaji ya wakulima kama ilivyokubalika kwenye Hatua ya 2. Hakikisha kuwa kuna fursa sawa kwa wanawake na wanaume kuhudhuria kwenye utekelezaji wa shughuli za mradi.

Lengo

Kuanza kiwanja cha majaribio na kutekeleza shughuli zilizofafanuliwa kwenye mpangokazi kwa kiwanja hicho. elaborated in the work plan of the test plot.

Vifaa vinavyohitajika

  • Zana za kupimia kulingana na kifaa kilichochaguliwa, k.m. pimajoto, kifaa cha kupimia unyevunyevu wa udongo au kifaa cha kupimia viwango vya mvua inayonyesha
  • Viwanja vya majaribio vinavyotembelewa mara kwa mara

Muda unaohitajika

Miezi michache kwa miaka mingi - inategemeana na aina ya mbinu ya makabiliano

Vidokezo

  • Mpangokazi uliokubalika unatakiwa ufwatwe vizuri iwezekanavyo. Lakini, kama shughuli hazitaenda kama zilivyopangwa, pengine itabidi kuifikiria ratiba upya. Jiulize sababu za kuahirisha shughuli na kama kuna maswala ambayo haukuyafikiria wakati wa kutayarisha wakati wa vipindi vya upangaji.
  • Ni muhimu kuwa na mazungumzo na kutathmini gharama za utekelezaji pamoja na wakulima wakati wote.
  • Mwanzo wa shughuli ni muhimu sana na mafundi wanatakiwa kufika kila inapokubaliana kukutana
  • Ripoti fupi juu ya kila kipindi cha matembezi ni muhimu, Hakikisha kuwa unanukuru matukio yoyote yasiyotarajiwa (angalia Jedwali la 34)
  • Mafundi wavutiwe kupiga picha kwa muda muafaka ili kuweka kumbukumbu za maendeleo
  • Muda unaohitajika: miezi hadi miaka kadhaa, kulingana na aina ya mbinu ya makabiliano.
  • Ingesaidia kuanza kunukuru orodha ya maswala, matatizo, mawazo au matukio yoyote yasiyo ya kawaida kwa ajili ya kutathmini baadaye.
  • Linganisha maendeleo ya mpangokazi mara kwa mara na nukuru sasabu zozote za kushindwa au kuahirisha.
  • Fikiria swala la jinsia wakati wote. Kwa mfano, kwenje Jedwali la 35, safu iliyowekwa kwa ajili ya kunukuru maoni ya wakulima litaonyesha mawazo ya wakinababa na wakinamama.
  • Pale inapowezekana, vipimo na matokeo kutoka shambani yanukuriwe kwenye maJedwali na kuchorewa chati mara kwa mara ili kuhakikishia kuwa kazi inaenda kama ilivyopangwa. Viwango viangaliwe kuhakiksha kama inaenda kama ilivyotarajiwa (angalia Jedwali la 35).
  • Jadili matokeo na wakulima mara kwa mara.
  • Na mwishowe, elezea kwa undani utafiti uliofanyika (angalia Sehemu ya 2, Hatua ya 5 “matumizi ya matokeo yako – Toa ushauri kwa mipango ya mbele”.

Mwongozo wa maswali kwa masahihisho ya mbinu maalum ya makabiliano::

  • Je, kuna ushahidi wa kutosha kutoka majaribio ili kuweza kutoa ushauri kwa kiwago kikubwa cha mrado (k.m. ili kukuza mipaka ya mradi)?
  • Je, kuna mawazo mapya yanayotokana na majaribio ambayo yangefaa kuendelezwa kuwa majaribio mapya?
  • Je, kuna matokeo kutoka tathmini ya zana ambazo zinatoa ushahisi wa kuridhisha juu ya kutokufaa kwa zana maalum (k.m. gharama yake ni kubwa mno, au haifanyi kazi kama inavypaswa) au kusababisha mgogoro wowote kwenye kaya za wakulima?
  • Je, ishara za kutathmini mbinu za makabiliano zilisaidia? Je, zinapima matokeo kwa wanaume na kwa wanawake?
  • Je, malengo ya awali na vigezo vilivyotumika vilisaidia na vilikuwa halali? Kama sivyo, ni vegezo vipi ungeweza kutumia badala yake?
  • Je, unaweza kutambua vihatarishi muhimu vinavyohusika na utekelezaji wa kila mbinu la makabiliano (k.m. gharama kuwa juu mno, kuchukua muda mrefu kutekeleza)?
  • Je, kuna Kihatarishi chochote kuwa zana inaweza kufanya vitu viwe vibaya zaidi (k.m. matandazo kuleta Kihatarishi cha moto kipindi cha kiangazi kirefu)?
  • Je utafikiaje mchakato mzima wa makabiliano?
  • Utawezaje kuunganisha zana tofauti ili kufanya mfumo wako uwe jasiri zaidi?
Umbo la 41: wakulima wanapima urefu wa mizizi ya miche ya kahawa iliyo na isiyo na matibabu ya Trichoderma na Mycorrhizae, kwenye mradi wa c&c ukanda wa Trifinio
kikundi cha watu kimesimama kuzunguka rundo la mimea.
Jedwali 36: Jedwali la Maoni na uchunguzi wa mbinu la makabiliano kwenye viwanja vya majaribio

Mbinu la makabiliano

Ishara ya mafanikio shambani

Vipimo

Matokeo/ Tathmini

Uamuzi

Mychorrizha

Urefu wa mzizi mkuu

Sentimeta 19.25

Kahawa yenye Micorrhiza ina mzizi mkuu mrefu zaidi

Uambukizaji wa Micorrhiza kwenye miche imeonyesha matokeo bora zaidi kwenye urefu na uzito wa mizizi, pamoja na idado ya mizizi midogo midogo, kushinda tiba ya Trichoderma na jaribio linganishi.

Hapo miche iliyoambukizw na isiyoambukizwa ikipandikizwa shambani, ni muhimu kufwatilia kiwango cha kufa kwa miche.

Trichoderma

Urefu wa mzizi mkuu

Sentimeta 16.5

Bila

Urefu wa mzizi mkuu

Sentimeta 12.5

Root biomass

Gramu 60

Kahawa yenye Micorrhiza ina uzito zaidi

Gramu 54

Gramu 32

Abundance of absorbing roots

Nyingi sana

Kahawa yenye Micorrhiza ina mzizi midogo midogo mingi zaidi

Nyingi kidogo