Utangulizi wa mabadiliko ya tabianchi na tofauti za hali ya hewa
Mabadiliko ya tabia nchi na utofauti wa hali ya hewa nini ni?
Taasisi ya Jopo la Kimataifa la Mabadiliko ya Tabia nchi (IPCC) inafafanua mabadiliko ya tabia nchi kama ifwatavyo “tofauti lolote la tabia nchi lenye uzito, kama vile joto au mvua, linayodumu kwa muda mrefu, kawaida kwa miongo, inayotokana na hali ya kawaida au kusababishwa na shughuli za binadamu”.
Mabadiliko ya tabia nchi kimsingi ni matokeo ya ardhi kupata joto, ambalo ni jambo la kawaida. Lakini shughuli za kibinadamu zimesababisha kiwango cha ongezekola gesi ukaa hewani, kitu ambacho kinachochea na kuharakisha ongezeko hili, na kusababisha mabadiliko ya joto yanayohisika, mabadiliko ya misimu ya mvua, na kiwango na idadi ya matukio iliyokidhiri kama vile dhoruba na mafuriko, pamoja na hali ya hewa isiyotabirika pote duniani (angalia pia Sehemu ya 2 “Nini ni matokeo ya gesi chokaa na ongezeko la joto dnuiani”?
Mabadiliko ya tabia nchi yameanza kuwa tatizo linalotambulika na kimataifa, na madhara yake yameshuhudiwa pote duniani, na kwa sekta nyingi, ikiwemo pia kilimo. Mabadiliko makuu yanaotokana na ongezeko la woto duniani ni kuongezeka kwa joto, mabadiliko ya mikondo ya mvua,na kiwango na idadi ya matukio iliyokidhiri kama vile dhoruba, mafuriko, au ukame. Matukio yote haya ya maji na hewa yanaitwa .
Ufafanuzi
Tabia nchi na Hali ya hewa
Tabia nchi mara nyingi hufafanuliwa kama wastani wa hali ya hewa kwa kipindi kirefu (kawaida miaka 30)
Hali ya hewa inaeleza hali ya angahewa pahala fulani kwa kutimia sifa za joto la hewa, shinikizo, unyevunyevu, kasi ya upepepo, mawingu na mvua.
Vihatarishi vya tabia nchi au vichochezi vya tabia nchi vinavyosababishwa na kuongezeka kwa joto la dunia
- ongezeko la wastani wa joto la dunia
- mabadiliko ya mikondo ya mvua, yaani, mabadiliko ya muda na viwango vya mvua (k.m. mvua kuchelewa kuanza, mtawanyiko wa mvua, nguvu yake, kipindi cha kunyesha na idadi ya matokeo ya ukame kutokea katikati ya msimu).
- Ongezeko la idadi na nguvu ya hali ya hewa iliyokidhiri (k.m. dhoruba, mafuriko, vimbunga)
- ongezeko la joto za bahari
- Ongezeko la joto za ncha za dunia na kupoteza barafu za baharini kutokana na kimo cha maji ya bahari kuongezeka
Pamoja na mabadiliko ya tabia nchi duniani, tukio la ugeukaji wa tabia nchi pia unatakiwa uzingatiwe. Ugeukaji wa tabia nchi inamaanisha kugeuka kwa hali ya sasa ya tabinachi, k.m. kiwango cha mvua tunachokipata mwaka hadi mwaka. Mifano ya ugeukaji wa tabia nchi pia ni ukame wa muda mrefu, mafriko na hali inayotokana na matukio ya el Nino na El Nina (ENSO). Ingawa kumbukumbu za hali ya hewa zinaonyesha kuwa joto la dunia linaongezeka, tathmini ya mkondo ya mvua haina uhakika sana na haionyeshi mwelekeo ulio wazi hadi sasa.
Lakiini inaendelea kugeuka msimu hadi msimu.
Sekta ya kiuchumi inayoathirika sana na mabadiliko ya tabia nchi pia ni mojawapo inayotegemea sana mazingira na mali asili kuwa imara: yaani kilimo. Lakini, matatizo mengi yanayowakuta wakulima si matokeo ya mabadiliko na mageuzo ya tabia nchi pekee. Mabadiliko na ugeukaji wa tabia nchi yanaongeza uwezekano wa janga kutokea, na yanaingiliana na vihatarishi vilivyopo na vitaakavyokuwa na hivyo kuweka hali ambayo haikutarajika.
Kwa mfano, ongezeko la nguvu ya mvua (jambo ambalo ni kawaida) inaweza kusemekana kusababisha ongezko la mmomomnyoko wa ardhi. Lakini, sababu la tukio kama hili linaweza kuwa ongezeko la matumizi ya madawa ya kuua magugu na kuondoa miti ya kuvuli kwenye mashamba ya kahawa, inayosababisha maji kupita kwa kasi zaidi. Hali ya hewa inachangia, .
Kwa ujumla, mabadiliko ya tabia nchi kwa muda mrefu yanatarajiwa kusababisha ongezeko la idadi na uzito wa vihatarishi vya hali ya hewa. Hii inaweza kuwa pia muda, idadi na mtawanyiko wa mvua, pamoja na mafuriko, ukame na vimbunga.
Athari za hewa ukaa na ongezeko la joto la dunia ni nini?
Umuhimu wa athari ya hewa ukaa
Athari ya hewa ukaa ni tukio la kawaida linalowezesha maisha duniani. Maneno haya yanatumika kumaanisha kuwa dunia na angahewa yake inapata joto zaidi, hii inafanfa na kitalu shamba kubwa linapopata joto kutokana na jua. Gesi kuu za hewa ukaa ni H2O (maji), CO2 (hewa mkaa), CH4 (methane), and N20 (nitrous oxide).
Dunia inapata nishati kutoka juani kwa kupitia mnururisho wa masafa mafupi. Mnururisho wa jua unaipenya angahewa na kufika kwenye uso wa dunia. Dunia inafyonza kiasi cha nishati hii na kuimulika kiasi nyingine kwenye angahewa kwa kupitia mnururisho ulio chini ya miali ya rangi nyekundu katika upinde wa mvua (infrared) hewa ukaa inazuia baadhi ya mnururisho huo kutoka kweye angahewa yetu, yaani kiwango fulani cha joto haliwezi kutoka, na kurudi angani. Hivyo, hewa ukaa inakuwa kama blanketi na angehewa inapata joto (angalia Umbo la 20).
Bila gesijoto au bila athari ya gesijoto, dunia ingekuwa ayari iliyojaa barafu, isingeweza kuwa na uhai kama tunavyoona. Bila madabidiko (au na mabadiliko madogo sana) ya gesijoto kwenye angahewa, jotoridi ingeweza kubaki ilie ile kwa miongo mingi.

Athari za gesijoto zilizosababishwa na binadamu na kuongezeka kwa joto la dunia
Ongezeko la wastani wa jotoridi dunianitangu katikati ya karne ya 20 imesababishwa kwa kiwango kikubwa zaidi na ongezeko la gesijoto kutokana na shughuli za kibinadamu, ambazo zinaongeza kiwango na kasi ya ongezeko la joto la dunia. Gesijoto inazidi kuongezeka kutokana na shughuli za kibinadamu, kama vile uzalishaji wa nishati, shughuli za viwandani, ujenzi wa miundombinu au shughuli za kilimo (angalia Umbo la 21)

Jinsi uzalishaji wa gesijoto unavyozidi kuongezeka, angahewa itazidi kupata joto. Kulingana na makadiriano ya uzalishaji wa gesijoto, wastani wa jotoridi unaweza kuongezeka kati ya 1.1 C na 6.4 Y ifikapo mwisho wa karne ya 21 (IPCC). Kiasi cha ongezeko a joto inategemea hali ya mbele itakayochaguliwa na binadamu, yaani, ama kupunguza uzalishaji wa gesijoto ili kutokuwa na athari kabisa, kupunguza athari, au kuedelea na hali ya sasa ya kuongezeka kwa joto. Umbo la 22 linaonyesha mfano uliyotayarishwa na IPCC wa.

matokeo yanayowezekana ya ongezeko la joto la uso wa dunia mwaka 2100, kutokana na aina nne za uwezekano wa uzalishaji. Ikiwa uzalishaji wa kiuchumi utabaki jii (mstari mwekndu) ongezeko linaweza kufikia nyizi nne. Takwimu hizi zinaweza zikaonekana ni ndogo, lakini athari zake zitakuwa na matokeo kwa uzalishaji wa kahawa (angalia Sura ya 1.2)
Kama uzalishaji wa gesijoto ungepungua kulingana na kukuwa kwa uchumi kwa kiasi kidogo (mstari wa bluu), tunaweza kutarajia ongezeko la jotoridi dunian la chini ya nyuzi mbili ya sentigredi kwa miaka 100 ijayo.
Kuongezeka kwa joto duniani na utabiri wa baadae wa mabadiliko ya tabianchi
Ingawa tabia ya nchi si kitu cha uhakika na itendelea kutofautiana mwaka hadi mwaka, makadirio ya muda mrefu ya tabia nchi yanasema kuwa kwa ujumla tunaweza kutegemea wastani wa jotoridi iliyo juu zaidi, kwa masaa ya mchana na usiku (angalia Umbo la 23 kwa mfano wa maongezeko ya jotoridi kwa sasa), na ongezeko la idadi na viwango vya matokeo kidhiri isiyoweza kukadiriwa (vihatarishi vya hali ya hewa).
Ongezeko la jotoridi duniani linategemewa kusababisha ongezeko la mvukizo na hivyo mfumo wa mzunguko wa maji hewani kuwa na uzito zaidi wa mawingu na mvua, hasa kwenye kanda za kitropiki. Baadhi ya sehemu zitakuwa na mvua zaidi, lakini sehemu nyingine zitapata mvyua chache, jamb ambalo litaathiri mazao. Si kiwango cha mvua tu kitakachobadilika bali pia utofauti, kwani baadhi ya miaka itakuwa na unyevunyevu sana na miaka mingine itakuwa kavu sana. Tatizo lingine litakuwa utofauti wa mvua kwa mwaka mzima, ikimaanisha kuwa misimu ya mvua itasogea.

Ongezeko la joto kwa ukanda
Pamoja na ongezeko la joto la dunia, pia lazima kuzingatia ongezeko la joto kwa mikanda. Ongezeko la joto la kawaida linaweza kusababishwa na mabadiliko ya matumizi ya ardhi na hivyo kuchochea hali na kidhiri ya tabia nchi ya kienyeji. Umbo la 24 linaonyesha mfano wa jinsi gani mabadiliko ya matumizi ya ardhi kwa ngazi ya kienyeji inaweza kusababisha ukidhiri kuongezeka. Misitu inaweza kuwa bafa (kinga?) dhidi ya ukidhiri wa hali ya hewa kwani manaji ya miti inasababisha mvukizo na hivyo kupunguza joto la tabia nchi ya kienyeji, na hivyo uzalishaji wa mawingu na mvua. Pale, msitu unapoharibiwa, punguzo la joto kutokana na mvukizo vinasababisha jotoridi kuongezeka na ukame. Kwa hivyo, ukame hausababishwi moja kwa moja na mabadiliko ya tabia nchi ya dunia, bali unaweza kusababshwa kuwa kidhiri zaidi.
