Tambua kwa nini, nini na nani kwa ajili ya mchakato wako wa M&E
Muhtasari
Shughuli hii inahusu uchunguzi na ufafanuzi wa matarajio yako kutokana na mchakato wa M&E, nini unachojaribu kuchunguza na kutathmini, na nani utamhusisha katika kazi hiyo.
Utatuzi wa maswala haya matatu utakuruhusu kutambua maswali ya utathmini na kutayarisha mchakato wa kukusanya taarifa na kuichanganua kwa njia iliyo na manufaa kwako.
- Majadiliano ya makundi maalum au mahojiano ya ana kwa ana inayowezeshwa na afisa ugani mwenyeji
- Mbinu shirikishi za uvumbizi za kukusanya na kubadilishana mitazamio tofauti kama vile ramani ya mazungumzo au picha zilizostawi
- Mazoezi shirikishi ya kupanga oroda ya ushindi ili kuwekea kipaumblele maeneo yanayohitaji mkazo wakati wa mchakato wa M&E.
- Kulinganisha na kazi za awali zilizofanyika za kuwashirikisha wadau (Hatua za 2 na 3)
- Uelewa unayolingana juu ya matokeo ambayo yangependwa yafikiwe na wadau
- Mipaka inayoeleweka juu ya upana wa tathmini, k.m. je inatathmini mbinu moja pekee, seti ya mbinu , au program nzima? Ni athari zipi zitazingatiwa (k.m. ukame, ongezeko la magonjwa, n.k.)
- Ufafanuzi juu ya wadau gani washirikishwe na jinsi gani watachangia kwenye mchakato wa M&E
Nadharia
Jedwali 16: Kutambua Madhumuni ya mpangilio utaratibu wa Ufuatiliaji na Tathmini (M&E)
Nini nia za kufanya utathmini kwa kipindi hiki | Fikiria pia: Ni nini juu ya mradi ungependa kufahamu zaidi? Ni nani atapewa ujumbe na wanahitaji nini zaidi? |
Je, unahitaji kuthibitisha kwa wengine kuwa |
|
Je, unahitaji kuthibitisha mafanikio ya mbinu za makabiliano? |
|
Je, unataka kuwasilisha mafanikia na sababu zake? |
|
Je, ungependa kuboresha utaratibu wa kufanyika kwa maamuzi? |
|
Je, ungependa matokeo yatumike kuongoza kazi za mbele? |
|
Je, unataka kuwashawishi wengine kuchikua hatua? |
|
I. Kwa nini: Kutambua madhumuni ya mchakato wako wa Ufuatiliaji na Tathmini (M&E)
Ni muhimu kuwa wazi juu ya sababu za kufanya shughuli za M&E kwani hii itaathiri jinsi utakavyopanga, nani atahusishwa na ushaidi utakaoamua kukusanya.
Sababu za kufanya M&E:
- Kuonyesha kuwa umetekeleza ulichosema utafanya
- Kufwatilia maendeleo
- Kuwasilisha vitu vinavyoenda vizuri na sababu zake
- Kuboresha mchakato wa kufikia maamuzi
- Kuongoza kazi ya miaka ijayo
- Kuwahamaisisha watu wengine kutenda
Pamoja na kutathmini utenaji wa kiufundi wa hatua za makabiliano (k.m. je, mtambo wa kutenga maji ya mvua unafanya kazi vizuri?)M&E pia inachunguza matokeo ya hatua hizi na jinsi gani yalifanikiwa kwa hali na mazingira mbali mbali.
Kwa mtambo wa kutenga maji ya mvua, hii inaweza kuwa pia kufananisha ufanisi wa mtambo huu na mbinu nyingine zilizopo, kulinganisha gharama na kufaa za mtambo, na kuamua nani atafaidika na mtambo (na nani hatafaidika nao), na kufafanua kama mtambo una atharizi mbaya zozote (K.m. unasababishwa utumizi mkubwa sana wa maji).
Wakati wa kutambua madhumuni, ni muhimu pia kuzingatia wakati utakaopanga kufanya kipengele cha utathmini wa mchakato wa M&E. Kwa mfano, kama utafanya utathmini ifikapo katikati ya ya awamu, madhumuni muhimu yanaweza kuwa ni kuelewa jisi gani sura mbalimbali za mradi zinaweza kuboreshwa au kuongezewa kwa kipindi kifupi.
Hakikisha unajadili na wadau muhimu juu ya madhumuni ya mchakato wako wa M&E. Ukieleza sababu za kufanya utathmini, na ukianza majadiliano juu ya manufaa ya matokeo ya M&E (yakiwemo manufaa kwao), wadau wanaweza kujishirikisha kwa njia nzuri.
II. Nini: Tambua ni nini unachokichunguza na kukitathmini
Pia ni muhimu kufikiria ni nini haswa unachokichunguza na kuktathmini. Kuna idadi kubwa sana ya mbinu na mbinu za makabiliano kama mwitikio wa mkusanyiko wa athari (joto, mva, magonjwa, ukayi wa upepo, n.k.). Inawezekana kuwa unachunguza na kutathmini mbinu moja to au programu au mradi mzima. Lakini, ukizingatia malego ya c&c, tunaweza kusema kuwa utakuwa unachunguza na kutathmini:
- Jinsi gani mbinu za makabiliano zinawasaidia wakulima wadogo wadogo wa kahawa kujenga ujasili wao shidi ya mabadiliko ya tabia nchi
- Jinsi gani mbinu za makabiliano zinaboresha uwezo wa wakulima wadogo wadogo wa kukabiliana
Hoja hizi mbili za upana zitahitaji kufafanuliwa kwa undani zaidi. Kuweka mipaka iliyo wazi kwa kile utakachokitathmini itakuaidia kuchagua mbinu iliyo bora zaidi. Kwa kufikiria kwa makini nini unachokichunguza na kukitathmini, na kuunganisha hicho na yale malengo yaliyofafanuliwa na jia yako ya mradi utakuwa umejenga msingi imara ambao juu yake utaweza kujenga a) isharia zinazifaa na b) seti imara ya maswali ya tathmini.
Mwongozo wa Maswali ya kufafanua nini unachochunguza na kutathmini
- Ni athari zipi (za moja kwa moja au za mzunguko) za mabadiliko ya tabia nchi nzizo unazoziitikia (k.m. kupunguza madhara ya ukame, mlipuko wa magonjwa, mmomomnyoko wa ardhi, n.k.)?
- Utajengaje ujasiri (k.m. kwa kupitia ubora wa mimea ya kahawa, kwa kuelekeza kipato cha kaya kwingine, kwa kuboresha upatikanaji wa masoko, n.k.)?
- Je,kazi itakazania kwa kikundi kimoja maalum?
- Je, unatarajia kujenga uwezo wa wakulima moja kwa moja, au kwa kuwafundisha maafisa ungani?
III. Nani: Kupanga nani atahusishwa kwenye mchakato wa M&E
Uamuzi juu ya nani ahusishwe kwenye machakato wa M&E na majukumu watayayokuwa nayo, inahitaji uwiano kati ya kuwajumuisha wote walio na ujuzi wenye manufaa na uzoefu, na kusimamia hali halisi kulingana na muda na malishafi zilizopo.
Mwongozo wa maswali kwa upangaji wa wahudhuria wa M&e:
- Nani ana wajubika kwenye kile kitakachochunguzwa na kutathminiwa?
- Nani anatarajiwa kunufaika, au kuathirika (moja kwa moja au kwa mzunguko) kutokana na kile kitakachotathminiwa ?
- Nani anaweza kuathiri kile knachochunguzwa na kutathminiwa?
- Nani anaweza kuathiri kama matokeo ya tathini yatatekelezwa?
Angalau wtu muhimu kama vile wakulima na maafisa ungani wachangie kwa kutoa taarifa na uzoefu wao. Lakini, mbinu shirikishi zaidi za uchunguzi na tathmini zinaweza kuwa zenye manufaa zaidi. Hizi zinahitaji wakulima na wadau kushiriki zaidi kwenye utayarishaji wa mchakato wa M&E. Pia watakuwa na majukumu muhimu ya kujadili jinsi gani kufafanua mafanikio ya makabiliano, ushahidi utakaohitajika na ukusanyaji wa takwimu pamoja na tathmini zake. Hivyo,jukumu la mtu au timu itakayokuwa na wajibu wa kutekeleza mchakato wa M&E unaweza kubadilika kutoka upande wa kuwa na madara kamili juu ya mchakato na kuhamia upade wa kuwa mwezeshaji w wengine.
Mwongozo
Uchunguzi, utathmini, fikra, na mafunzo shirikishi kwa makabiliano ya jamii (PMERL)
Mwezeshaji 'mzuri' anatoa huduma ya kusisimua fikra na majadiliano, badala ya kuongoza. Anawasaidia wahudhuria kuyaweka mawazo yao wazi na kukusanya fikra za wadau wa aina mbal mbali. Hii inahitaji ufanisi wa mapatano , na mara nyingine hata aweze kusululisha watu. Wawezeshaji wanatakiwa kuuliza maswali yanayofaa kwa muda muafaka, kusilikiza vizui kinachozungumzwa, na kujenga uaminifu, kuwatia moyo watu kubadilishana mawazo na wakati huo huo kuhakikisha kikundi kinabaki ndani ya mada.
Kuwa wazi juu ya jinsi gani utaamua nani atahudhuria itasaidia watu kuelewa ni nini inategemewa toka kwao. Kuwaleta wakulima na wadau wengine wa kienyeji pamoja kwa madhumuni ya kutathmini na kujifunza kutoka kazi inayofanyika inahitaji mbinu zinazothamini kuwa wote watakuwa na mtazamo na ushahidi tofauti (k.m. maoni, mazoea, takwimu halisi, na utamaduni). Baadhi ya wahudhuria watahitaji kusaidiwa zaidi (k.m. muda, mwongozo, kupata takwimu) ili waweze kuchangia kwa ufanisi.
Mwezeshaji anaweza kutumika kujenga uwezo wa timu ya M&E wa kuwahusisha watu, kusaidia mahudhurio na kuwatia moyo wenyeji kuchukua nafasi ya kuchangia kwa hali kwenye kusimamia mchakato wa M&E. Kama kutakuwa na utofauti mkubwa wa madaraka kati ya watu kwenye vikundi vya wahudhuria, itakuwa bora zaidi kukutana na kila kikundi peke yake kabla ya kuvikutanisha. Hii itawaruhusu kufikiria mtazamo wao wenyewe kwanza kabla ya kubadilishana na wengine.
Pia rejea kwenye ramani ya wadau iliyotayarishwa kwenye Hatua ya 2. Pengine wadau wengi waliotambuliwa na walioshirikishwa wakati wa hatua za kutathmini na kupanga makabiliano wanahitaji kushirikishwa kwenye mchakato wa M&E pia. Fikiria ni jinsi gani wadau hawa wameshirikishwa hadi leo na zingatia jinsi gani wataweza kuendelea kuchangia au kunufaika kutokana na mchakato wa M&E.
Jedwali 17: Kanuni za Tathmini Husishi kutoka PMERL
Mahudhurio | Panga zoezi la U&T liwazingatie wale wanaoaguswa zaidi na shughuli zinazofanyika. |
Mapatano | Toa nafasi kwa majadiliano huru juu ya sehemu zitakazochunguzwa na kufanyiwa tathmini. Matokeo yasitegemee maoni ya watu wenye madaraka tu. |
Mafunzo | Kila aliyehusishwa kwenye tathmini awe tayari kujifunza na apate taarifa za kutosha kumruhusu kufanya hivi; pia kubadilisha mawazo na apewe afasi ya kufikiria zaidi matokeo ya tathmini hii. |
Utayari wa kubadilika | Weka nafasi ya mipango kubadilika jinsi muda unevyokwenda ili kuzingatia mafunzo mapya na uelevu |
ni
- Nani anaweza kuchangia mtazamo au ushahidi wenye manufaa ambao ama umeathirika kutokana, na au uliathiri, mchakato wa makabiliano (k.m. wasimamizi wa miradi na wafanyakazi wa mashambani, mabia wa kienyeji, NGO za kienyeji, serikali za kienyeji, jamii)?
- Nani atakayekosekana na pia mchango wake utamaanisha kuwa taarifa muhimu nazo zitakosekana? Ni sababu zipi zitakomesha mahudhurio yao na utawezaje kukwepa hayo?
- Ni kwa njia gani utaweza kusaidia mahudhurio ya wakulima wadhaifu kwenye mchakato wa utathmini ambao unaweza kuwa ni kitu kigeni sana kwao?
- Ni uwezo wa nani wa kuchunguza unastahili uongezewe ili kuhakikisha kuwa mchakato ni endelevu?
- Nani ahudhurishwa kwenye kuhakiki maana ya tarifa zinazokisanywa?
- Je, wale waliohudhurishwa (wanasayansi, wakulima, wafadhili n.k.) wanathamini aina tofauti ya taarifa kwa usawa? Kama sivyo, hii itasimamiwa vipi?
- Je, wahudhuria watabadilika muda hadi muda? Hii itasimamiwa vipi?
- Je, kuna athari zozote za kimaadili zinazohitaji kuzingatiwa wakati wa kuwahusha watu kwenye M&E?
- Je, ni kwa kiasi gani maswala ya nje (k.m. taasisi, masoko, utawala) unaweza kuathiri kile kinachotarajiwa kufanikishwa kwa ngazi ya shamba? Hii ina maana gani na nani anatakiwa ahusishwe?
Mwongozo wa vitendo
Sehemu ifwatayo itatoa ushauri wa mazoezi yatakayokusaidia kuandaa na kutekeleza mpango wa uchunguzi na utathmini (M&E), ambaya ilikwisha jadiliwa kwa ufupi hapo awali, kwenye Hatua ya 5. Hautahitaji kutumia kila zoezi kama ilivyoelezwa hapa au kufwata orodha yoyote maalum, bali kuchagua zilie zinazokufaa wewe kwani mazoezi nanaweza kufanya kazi kwa baadhi ya vikundi na siyo kwa vingine.
Lengo
- Kutambua na kukubaliana madhumuni ya mchakat wa M&E
- Kutambua upana wa utekelezaji utakaofanya
- Kutambua nani anatakiwa kuhudhuria kwenye M&E na kwa njia gani
Madhumuni ya ujumla ya mpango wa c&c ni kujenga ujasiri wa sekta ya ndani ya kahawa dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi. Lakini, ni muhumu kuweka mpango huu mpana katika hali ya kienyeji na kufikiria vigezo vinavyowakilisha mfumo wa uzalishaji wa kahawa ulio jasiri (angalia tangulizi kwenye Sehemu ya 1). Tumia Jedwali ifwatayo kama mfano w kunukuru matokeo kwa kila hatua. Ukishajaza kila shughuli na kujaza kila sehemu ya Jedwali, utakuwa umekamilisha mpango wa M&E.Matokeo yanayotarajiwa
Matokeo tarajiwa
- Madhumuni wazi na malengo ya mafunzo kwa tathmini ambayo imekubalika na wale wanaotekeleza na/au wanaooathirika na mchakato wa makabiliano
- Muda na malighafi zikiruhusu, mpango wa kina wa wadau unaoeleza nani ashirikishwe na kwa madhumuni yapi.
- Makamilisho ya Sehemu A (I hadi III) ya mpango wa tathmini (madhumuni, upana na nani ahusishwe)
Muda unaohitajika
Itategemea muda utakaohitajika kuelewa madhumuni na pia kutegemea malighafi zitakazokuwepo.
Utaratibu
I. Fafanua kusudi
- Rejea madhumuni ya awali ya mradi, kwani madhumuni ya tathmini yanaweza kuendana nazo.
- Jadili maswali kwenye mwongozo hapo chini pamoja na watu muhimu (maafisa ugani, wafadhili, wakulima n.k.), ama kwa kupitia majadiliano ya vikundi maalum au mbinu ya ana kwa ana ili kujifunza nini wangependa kupata toka tathmini hiyo. Pengine orodha ifwatayo ya sababu zinazopendwa za tathmini itaweza kusaidi majadiliano yako. Amua ni yapi yanaendana na tathmini unayotaka kuifanya wewe (kwa taarifa zaidi angalia: www.ukcip.org.uk/ wizard/adaptme-toolkit/fundamentals/):
- kutathmini ufanisi
- kutathmini kufaa
- kuelewa uadilifu
- kuonyesha wajibu
- kutathmini matokeo
- kuboresha mafunzo
- Kuboresha shughuli na miradi ya mbele
- Kulinganisha matokeo na shughuli au miradi mingine inayofanana
- Tambua wapi palipo na makubaliano au uwezekano wa migigiro kati ya wale waliohusishwa, na dhana zao kulingana na mathumuni ya tathmini.
II. Fafanua upana wa mradi
- Ukirejea nyuma hadi malengo ya mradi na njia ya madi, tambua maeneo makuu ya msisitizo kwa ajiili ya tathmini yako, k.m.:
- Je itakazania utekelezaji wa mbinu moja tu ya makabiliano au baadhi ya mbinu?
- Vipi ni vihatarishi muhimu, k.m. ongezeko la ukame, ongezeko la joto, kutokea kwa dhoruba, au mchanganyiko wa vyote hivi?
- Ni vundi vipi ungependa kukazania, k.m. wakulima wote kienyeji wa wa kahawa pamoja na kaya zao, jamii za wakulima wa kahawa, au wakulima tu?
III. Amua nani atashirikishwa na kwa njia gani
- Rejea tathmini yoyote ya wadau iliyofanyika wakati wa mchakato wa makabiliano na tambua ni vikundi vipi, mashirika gani au watu gani binafsi wameshirikishwa hadi leo na nini haswa imekuwa mchango wao.
- Kama hakuna tathmini yoyote ya wadau iliyofanyika, au kama ilifanyika lakini si kwa ukamilifu, mazoezi shirikishi yanaweza kukusaidia kuweka ramani ya nani ameshirikishwa na ni kwa njia gani wangeweza kuchangia M&E.
- Ni muhimu kuhakikisha unaelewa juu ya:
- nani aliye na wajibu kwa tathmni
- Nani anatarajiwa kunufaika, au kuathirika na tathmini
- Nani anaweza kuathiri tathmini
- nani anweza kuhakikisha kuwa matokeo ya tathmini yanatekelezwa
- Kama una muda na rasilimali, tumia Jedwali mfano kwa kutayarisha mpango wa kuwashirikisha wadau katika tathmini
Jedwali 38: Mpango wa utekelezaji wa Wadau (Vigezo)
Mpango wa utekelezaji wa Wadau | |
1 | Fafanua Madhumuni Ni nini unataka kufikia kwenye harakati za Tathmini? Ndipo unaweza kuamua nani ahusishwe ili kufikisha mathumuni haya (rejea Kipengele A cha Mpango wa U&T) |
2 | Tambua wadau Nani anahitaji kuhusishwa? Reea kazi ya mwisho iliyofanywa kuhusu wadau na matokeo ya mazoezi yaliyopita, k.m. majadiliano, michoro, jedwali Anzisha:
Pai uliza: Ni kwa kiasi gani sababu nyingine (k.v. taasisi,masoko, serikali) zinaweza kuathiri matokeo yanayoweza kufanyika shambani? Na hii ina maana gani ukizingatia kuhusishwa kwa wadau? |
3 | Panga wajibu Nani atashika majukumu yapi? Wajibu kwenye U&T inahusisha pia mabadiliko kwenye mlolongo mzima wa tathmini, k.m.:
|
4 | Elewa wadau Unajua nini kuhusu wadau hawa? Nini unaweza kutambua juu ya wadau kutoka majadiliano yaliyopita, ukizingatia pia maoni yao, ujuzi, maslahi, mvutano wa nguvu, na jinsi wanavyoingiliana wao kwa wao, na uhusiano kati yao na wengine? |
5 | Chagua Wadau Ni watu wapi wanaweza kuwa wawakilishi wazuri wa taasisi au jamii zao wakati wa mkakati wa U&T? Ukishatambua vikundi maalumu vya wadau, sasa unahitaji kupata majina ya watu husika wanaofaa. |
6 | Zingatia miundombinu/mazingira Upi ni muda mzuri wa kuwafikia wadau hawa? Je, ni bora kuwahusisha mwanzo, au mwishoni au kipindi kizima? Ni kwenye msimu upi, siku zipi za wiki, na wakati gani wa siku utawafikia? Wapi ni sehemu bora ya kuwafikia wadau? Je, utakutana nao mmoja mmoja, au utawakusanya kwa ujumla? Utawakusanya kwenye jengo la jamii, sehemu ya umma, nyumbani au sehemu zao za kazi? |
7 | Tarajia mataizo/shida Ni matatizo yapi /shida zipi unaweza kuzitambua kabla ya kuanza? Je, waliohusishwa (wanasayansi, wakulima, washauri, wafadhili, n.k.) wanathamini aina tofauti za taarifa? Kama sivyo, utasimia vipi jambo hili? Ni kwa njia gani unaweza kusaidia ushirikisho wa wakulima masikini wa kahawa kwenye harakati za tathmini, ambayo ni kitu kigeni kwao? Je, wanahudhuria watabadilika jinsi muda unavyoenda? Utasimamia vipi jambo hili? |
Mwongozo wa maswali kwa ajili ya kutambua kwa nini, nini na nani
- Nini unaona ni madhumuni ya tathmini yako
- Nini ungependa kujifunza? Nani mwingine angefaa kujifunza, wangetakiwa wajifunze nini na ni kwa njia ipi hii inaweza kufanyika?
- Utawezaje kusimamia madhumuni yanayopingana? Ni mapunguzo yapi utahitaji kuyafanya na unaweza kueleza sababu zake?
- Nani wataangalia matokeo ya tathmini na mahitaji yao ni yapi?
- Nini unajua tayari juu ya wadau hawa kutokana hatua za awali?
- Ni watu gani wanaweza kuwa wawakilishi wazuri kwa mashirika yao au jamii zao?
- Ni mipango gani ya kilojistiki yanaweza kutarajiwa?
Mbinu za kiufundi
- majadiliano ya makundi maalum au majadiliano ya ana kwa ana yanayowezeshwa na maafisa ugani wenyeji.
- Mbinu shirikishi ya uvumbuzi kwa ajili ya kukusanya na kubadilishana maoni mbali mbali juu ya jambi, kama vile ramani ya mazungumzo au picha.
- mazoezi shirikishi ya kupanga orodha ya ushindi ili kuwekea kipaumbele maeneo ya kukazania kwenye tathmini
- Inawezekana kuwa tathmini ya wadau ilishafanyikwa kwenye hatua za awali za mchakato, ikimaanisha kuwa utahitaji kurejea kumbukumbu za kazi hyio. Kama tathmini ya wadau hakufanyika, kuna ushauri juu ya mbinu tfauti zitakazokusaidia kutekeleza tathmini ya wadau, angalia Sehemu ya 2, Hatua ya 2.