Tambua maswali yako ya tathmini
Muhtasari
Ukishakuwa umefafanua madhumuni ya mchakato wa M&E, sasa ni wakati wa kufikiria juu ya maswali ya tathmini ambayo yatasaidia fanikisha madhumuni hayo. Sehemu nzuri ya kuanzia ni kufikiria mantiki ya hatua zako za makabiliano na dhana ulizokuwa umeziweka kwenye hatua ya kupanga. Kama umetayarisha njia ya mradi (Hatua ya 3), tayari utakuwa umeweka ramani ya mantiki hii pamoja na dhana zilizopo. Maswali ya tathmini yanatakiwa yajaribu na kutia changamoto mantiki iliyofafanuliwa kwenye njia yako ya mradi, na kukusaidia kuelewa nini kilichoenda vizuri, nini kilichoenda vibaya na kwa nini.
- majadiliano kwa vikundi vya wadau muhimu walioshirikishwa kwenye kupanga mradi
- Majadiiano yanaongozwa na njia ya mradi (angalia Hatua ya 3), madhumuni ya M&E na matokeo ya majadiliano na semina ya awali
- Orodha ya maswali yaliyopangwa kwa kipaumbele ya kuelekeza mchakato wa M&E
Nadharia
Jendwali Na 18 hapo chini inatoa mfano wa ujumla wa aina za maswali unayoweza kuyazingatia. Haya yatahitaji yarekebishwe kulingana na mazingira na hai yako ya makabilian. Idadi ya maswali utakayochagua itategemea uzito wa mchakato wako wa makabiliano, rasilimali fedha uliyokuwa nayo, na madhumuni yako ya M&E. Nivema zaidi kutambua maswali ya tathmini kati ya tatu na nne, ambayo yanaweza kuwa na maswali mengine ndani yao.
Baadhi ya mafunzo muhimu yanaweza kupatikana kwa kuangalia nyuma ya yale uliyotarajia yatatokea na upelelezi wa yale yasiyotarajiwa. Hii inaweza kuwa vitu vizuri (k.m. mafunzo ya wakulima kwa wakulima yamesababisha kuchangia kwa nguvukazi kwa misimu muhimu ya mwaka) au mabaya (k.m. shughuli za kiufundi zilifanya kazi vizuri, lakini kukubalika kulikuwa dhaifu kwa sababu viongozi wa jamii hawakushirikishwa tangu mwanzo).
Hakikisha unaweka pia maswali yaliyo wazi ili kuzingatia maswala haya. Kwa mfano, badala ya kuuliza “Je, wakulima waliona kuwa mafunzo yana manufaa kwao?” uliza “Nini wakulima waliona ina manufaa kwao kutokana na mafunzo?” Hii inaweza kuleta jibu ambalo hukutarajia, na hivyo kukusaidia kuboresha mipango yako kwa awamu inayofwata.
Jedwali 18: Mifano ya Maswali ya Tathmini ya utaratibu wa makabiliano
Vipengele vya mchakato wa Makabiliano | Mfano wa maswali |
Mchakato wa shughuli zilizopangwa (Je, tumefanya kila kitu sawa?) |
|
Wajibu na Majukumu ya wadau na wakulima, pamoja na kiwango cha ushiriki wao kwenye utekelezaji |
|
Kufaa kwa mantiki ya mpango wa utekelezaji (Je, tumepatia kinachostahili?) |
|
Kama na kwa njia zipi matkeo yasiyotarajiwa |
|
Mwongozo wa vitendo
Lengo
- Kutambua maswali ya tathmini, ambayo yataamua kama “unafanya vitu ipasavyo” na “unafanya vitu vinavyofaa”
- Kutambua maswali yatakayokusaidia kupata taarifa zinazokamilisha madhumuni ya tathmini, pamoja na vifwatavyo:
- maendeleo ya shughuli na matokeo yaliyopangwa
- majukumu, wajibu na kiwango cha ushirikiano wa wakulima na wadau wengine wanaohusika kwenye utekelezaji
- kufaa kwa mantiki iliyotumika kwenye kutayarisha mpango wa uendeshaji, na dhana juu ya shughuli zitakazokusaidia kutimiza madhumuni ya jumla
- Kama na kwa njia gani matokeo yanayotarajiwa na yasiyotarajiwa yametokea na athari zake.
Matokeo tarajiwa
- Orodha ya maswali kutumia kwa mchakato wa tathmini uu kukamilisha Sehemu B ya mpango wa tathmini.
Muda unaohitajika
utatofautiana kulingana na kiwang cha ushirikiano kutoka wahudhuria
Mwongozo wa maswali
Jedwali ifwatayo inatoa mfano wa maswali ya tathmini kwa kila moja ya sehemu nne kuu za kutathmini mchakato wa makabiliano. Jiskie huru kuyabadilisha maswali kulingana na tathmini yako mwenyewe, au kufikiria maswali ya ziada kwa kila sehemu.
Utaratibu
- Unda maswali kuuliza wakati wa tathmini ambayo yatafwatilia maendelea yaliyofanyika kuelekea kufanikisha malengo ya awali ya utekelezaji
- Pamoja na hayo, tumia dhana ulizotambua kwenye njia yako ya mradi (kwenye Hatua ya 3) ili kufafanua maswali ya tathmini amabayo yataangalia kama dhana hizi zilikuwa zenye matiki na kama bado zinawakilisha ukweli.
- Kama hukutayarisha njia ya mradi, tumia Jedwali kwenye kipengele kifwatacho kama mwongozo wa kuunda maswali ya tathmini
- Pitia tena madhumuni ya tathmini na angalia kama maswali uliyounda yatatua mahitaji hayo.
Jedwali 39: Jinsi ya kuhakiki maswali yako ya tathmini – baadhi ya mifano
Sura nne kuu za mkakati wa tathmini ya makabiliano | Mifano ya maswali ya tathmini |
Mkakati wa shughuli zilizopangwa “Je, tumepatia vitendo tulivyotenda?” |
|
Wajibu, Majukumu, na kiwango cha wakulima na wadau wengine kujihusisha kwenye utekelezaji |
|
Kufaa kwa mantiki ya mpango wa utekelezaji, pamoja na dhana juu ya jinsi shughuli zinavyoambatana na mathumuni yote kwa ujumla “Je, tumefanya vitendo sahihi?” |
|
Kama na kwa njia zipi matokeo yasiyotarajiwa yametokea |
|
Mbinu za ufundi
Majadiliano na watu wakuu wanaohusika kwenye umbo la mradi (angalia Sehemu A), wakiongozwa na malengo ya mradi, dhana kutoka theory of change na matokeo ya majadiliano na semina zilizokwisha fanyika