Tayarisha mpango wa kukusanya ushahidi
Muhtasari
Hatua hii inazingatia aina ya ushahidi unaohitajika, changamoto za kukusanya ushahidi na jinsi ya kutengeneza viashiria.
- Fikiria malengo ya mradi, madhumuni ya M&E, njia ya mradi na maswali ya tathmini yanayotokea kwenye michakato hii
- Fikiria aina za ushahidi na mbinu za kuzikusanya, pamoja na maana yake kwa rasilimali
- tathmini ya kuunga mkono au kupinga ishara na aina nyingine za ushahidi
- Unda mbinu ya gharama ndogo na inayofaa kwa jamii kwa ajili ya kukusanya ushahidi.
Nadharia
Aina ya ushahidi
Aina mbili za ushahidi zinazotajwa sana kwenye M&E ni ya ukubwa au uwingi (zinaweza kupimwa au kuwekewa viwango) na ya kutegemea sifa (kutathmini ubora). Zote mbili ni muhimu kwa kujibu maswali ya tathmini. Ukitumia Mradi wa PRPR kama ilivyoelezwa ukurasa wa 58 kama mfano, takwimu za uwingi juu ya idadi ya wakulima wanaohudhuria mafunzo inaweza kuwa ya maana, lakini itahitaji kusaidiwa na takwimu za sifa (k.m. kutokana na mahojiano) ili uelewa kama, na jinsi gani, wakulima walitumia taarifa walizozipata toka mafunzo kwenye mashamba yao. Viashiria vilivyo rahisi kupima vinavutia, lakini mara nyingi vinahitaji taarifa ya nyongeza ya sifa ili kusaidia kuelewa hadhithi iliyofichika nyuma ya tarakimu.
Mwongozo
Ushahidi wa Uwingi ni njia nzuri ya kupima utekelezaji wa shighuli na kutathmii kama utekelezaji wa makabiliano unaendana na malengo ya kuleta matokeo yaliyokusidiwa. Pia inaeza kutumika kwa kujenga hali ya sasa ambayo itatumika kupima mabadiliko kwa tathmini za miaka ya mbele. Kuwa na viishiria vya uwingi vinavyofahamika ni muhimu kwa kuinganisha maendeleo ya shughuli zilezile zinazotendeka mahali pengine. Miongoni mwa viishiria vya uwingi ni k.m.:
- Kukubali na kutumia mbinu za makabiliano
- Mabadiliko ya faida kwa waliokubali na kutumia
- Kupima kiwango cha uchafuaji wa maji, n.k.
- Kiwango cha athari za hali ya hewa
Ushahidi wa sifa ni mzuri kwa kutambua nini kinachoathiri uwezo wa kukabiliana or ujasiri wa wakulima wadogo wa kahawa. Viashiria vya kuzingatia sifa ni kama vifwatavyo:
- Utayari na uwezo wa kuwekeza kwenye uboreshaji wa mali asili
- Mtazamo wa matumizi ya fedha ya kaya
- Sababu za tofauti wa uwezo wa kuzalisha kipato cha ziada kwa misimu tofauti
- Utayari wa ubunifu na kukubalika kwa mbinu bora za maishio
- Uwezo wa wanajamii kuunganisha nguvu
Changamoto za kawaida
Kwa sababu muda na rasilimali fedha mara nyingu kuwa pungufu, ni vizuri kujadili changamoto zitakaojitokea wakati wa kukusanya takwimu. Hivyo, unaweza kuwa wa wazi juu ya athari za mbinu zako za kupanga tathmini (imetoholewa kutoka PMERL)
- Kutumia takwimu zinazopatikana au kupata takwimu mpya: Wakati wote kutakuwa na usawa kati ya kile unachopenda kukichunguza na kukitathmini, na kile kinachowezekana ukizingatia muda na rasilimali fedha inayoatikana. Matumizi ya takwimu ambazo zipo na zinapatikana kwa urahisi ni wazo ziri, hasa kama rasilimali fedha ni finyo, lakini takwimu hizi zinaweza kuwa hazifai kwa shughuli yako na kuwa duni mno, au hata kupotosha kabisa kutoka lengo la kujenga ujasiri. Kwa mfano, takwimu zilizopo zinaweza kukupa vipimo vya wastani vya unyevunyevu wa udongo shambani, lakini ukitaka kuangalia kiwanja kikubwa cha mimea, hii haifai kwa vipimo vidogo vya unyevunyevu ambapo vipim vya vinazingatia mabadiliko ya aina ya udongo ny mwinuko wa kiwanja.
- Kutambua viashiria vinavyofaa kwa mazingira ya kienyeji au kutumia viashiria vilivyotungwa nje: Makabiliano mazuri kawaida huzingatia mazingira ya kienyeji na mifumo ya M&E inahitaji kurekebishwa kulingana na hali ya kienyeji. Lakini, kuwashirikisha wakulima na wadau wengine kwenye kutayarisha viashiria hivi inaweza kuchukua muda mrefu sana, na hii inasababisha matumizi ya viashiria kutoka nje kuvutia zaidi. Vipimo vya nje vinaweza kulinganishwa na maeneo mengine. Njia mojawapo ya kutatua hili ni kuvitafsiri viashiria toka nje ili kuhakikisha vinaendana na hali ya kienyeji. Kwa mfano, kiashiria kilicotungwa nje kinaweza kuwa upatikanaji wa takwimu za uhakika ya hali ya hewa. Hii inaweza kutafsiriwa kwa kienyeji kwa kuuliza kama kuna uhusiano mzuri na vituo vya hali ya hewa na mashirka ya utafiti.
- Kujenga uwezo wa kutekeleza M&E au kutumia wataalam wa nje: M&E inaweza kutumika kama fursa ya kuwawezesha wakulima na wadau kujifunza kutokana na mazoea yao kwa kupitia mpango wa kitaalam. Ili kujenga uwezo wao wa muda mrefu, wakulima hawaitaji tu kushirikia katika michakato ya makabiliano bali pia kuunda na kusimamia michakatao hii wenyewe. Hii inahitaji watu kuwekeza muda mwingi zaidi kwani mabadiliko haya hayafanyiki ndani ya muda mfupi. Pengine wataalam toka nje wangeweza kuifanya kazi hii kwa muda mfupi zaidi, lakini ingejenga uwezo mdogo sana wa makabiliano ya wenyeji. Ingekuwa vema kabisa kama wakulima wangepata mafunzo na kutekeleza utathmini wenyewe, jamo ambalo lingewajengea wao uwezo wa kutambua kiwango cha athari ya kihatariso cha hali ya hewa, kutambua dhana juu ya shughuli zipi zingejenga ujasiri, na kuunda mipango yao ya kukusanya ushahidi ili kuzijaribu dhana hizi.
- Kutathmini mafanikio ya shughuli zilizotekelezwa au kujifunza kutoka athari zisisotarajiwa: Ushahidi unohitajika na M&E mara nyingi ni mchanganyiko wa takwimo zilizo rahisi kuzipima na 'hadithi za mabadiliko' zinazofunmbua mambo yasiyotarajiwa tangu mwanzo wa mradi. Masimulizi haya ya mabadiliko ni muhimu kwani yanasaidia kukosoa dhana juu ya nini inasaidia tabia nzuri na nini inaipinga.
Mwongozo
- Uhalali: Je, watu wanaotumia taarifa wanaamini kuwa mbinu hii ni halali (k.m. wanaweza kutathmini kwa uhakika ishara inayotakwa?)
- Utumainifu: Je, mbinu hii itafanya kazi itakapohitajika?
- Uhusiano: Je, mbinu inazalisha taarifa inayohitajika?
- Uwezo wa kutambua: je mbinu hii inaweza kutambua tofauti ya takwimu kwa uhakika wakutosha?
- Ufanisi wa gharama: je, mbinu inazalisha taarifa kwa gharama ndogo?
- Muda: inawezekana kukwepa kuchelewa kati ya ukusanyaji, tathmini na matumizi?
Kuandaa na kuchagua ishara
Ishara inatoa taarifa maalum juu ya hali ya kitu fulani. Kwenye M&E, mara nyingi inahusiana na kutoa taarifa juu ya mabadiliko (k.m. je, wakulima wamekuwa wajasiri zaidi?). ishara ni sehemu muhimu ya uelewa wa mchakato ya mabadiliko na kuvumbua mbinu za makabiliano zinazofanya kazi au zisizo fanya kazi, kwa mazingira yapi na kwa nini.
Hakuna seti moja pekee ya isairia itakayofanya kazi kwa michakato yote ya utekelezaji wa makabiliano. ishara zinapaswa zichaguliwe kulingana na shughuli za makabiliano zilizopangwa na mazingira ya ndani ya pale shughuli izi zilipotekelezwa. Kwa kutayarisha viashiria kama sehemu ya njia ya mradi, utakuwa umehakikisha kuwa yanahusiana na malengo yako.
Tukidhani kuwa umetayarisha njia ya mradi kwenye Hatua ya 3, kazi hii itakusaidia kukusanya taarifa ili uelewe jinsi gani njia hii inafanya kazi kwa hali halisi. Kama hukutayarisha njia ya mradi, kazi hii itakusaidia kukusanya ushahidi utakaohitajika kwenye shughuli zako za M&E, lakini tunashauri kwanza uangalie Hatua ya 3.
Ishara zipo kwenye michakato ya uchunguzi na ya utathmini lakini si ishara zote zitatumika kwa shughuli zote mbili. Kwa mfano, inaweza kuwa gharama kubwa na vigumu kufwatilia dhana za wakulima kipindi chote cha utekelezaji wa mbinu za makabiliano (kama sehemu mojawapo ya uchunguzi wako), lakini inawezekana kuwa ungependa kufanya hivyo ifikapo tathmini ya nusu awamu. Vile vile, pengine tathmini yako haihitaji takwimu za kila mwezi kutoka mashamba ya majaribio, lakini badala yake utatumia muhtasari wa takwimu juu ya jinsi gani viwanja vya majaribio vimefanikiwa kwa ujumla. Uchunguzi wa maendeleo unategemea uchaguzi wa ishara zinazoweza kuonyesha mabadiliko. ishara hizi zinapaswa kuunganisha juhudi zako za utekelezaji na mbinu zilizopo za makabiliano (k.m. kutumia takwimu za maangalizi ya viwanja vya majaribio, angalia Jedwali na 19).
Aina ya ishara
Kuna aina mbili za msingi za ishara kwa M&% na idadi kubwa ya michakato inachangaya aina zote mbili: Ishara za matokeo zinaonyesha kuwa tokeo fulani limefanikiwa (k.m. punguzo la kupotea kwa kipato kutokana na magonjwa miongoni mwa wakulima wadogowadogo.).
Ishara za matokeo ni muhimu sana lakini mara nyingi zinaweza kuwa ngumu kutathmini kwani mara nyingi muda unaopita kati ya utekelezaji wa mbinu la makabiliano na matokeo kuonekana unaweza kuwa mrefu (k.m. kama hakuna mlipuko wa ugonjwa wa kutu kwenye eneo maalum, tutawezaje kufahamu kama hasara zimepungizwa kama mojawapo ya matokeo ya mradi?). Hivyo inasaidia kutumia ishara za mchakato kupima maendeleo yanayoelekea kufikisha matokeo (k.m. idadi ya wakulima wanaotumia mbinu za kudhibiti kutu ya majani kwa sasa au idadi ya wakulima waliopata mafunzo). Hizi ishara za mchakato zina thamani kwa kuelewa kama ujasiri unaongezeka, hata kama ujasiri bado haujajaribiwa na tukio la hatari ya hali ya hewa. Ili kuchagua ushahidi upi ukusanywe (au ishara zipi zipimwe), angalia maswali ya tathmni uliyotayarisha kwenye kipengele kilichotangulia na fikiria kwa kila mmoja aina ya ushahidi au ishara inayofaa zaidi, ukizingatia rasilimali na uwezo uliokuwa nao. Weka kumbukumbu za matokeo makuu ya shughuli hii kwenye Jedwali a vigezo vya mpango wa M&E, Sehemu ya 2, hatua ya 5.
Mwongozo wa vitendo
Lengo
Kuunda mpango hai na unaotumia fedha kwa ufanisi kwa ajili ya kukusanya ushahidi utakaosaidia kujibu maswali ya tathmini
Matokeo tarajiwa
- mpango wa kukusanya ushahidi, pamoja na orodha ya mbinu na zana unazopanga kutumia kujibu maswali yako ya tathmini uu Kukamilisha sehemu ya C ya mpango wako wa tathmini
Muda unaohitajika
Hii itatofautiana kulingana na mbinu utakazochagua kutumia, kina cha taarifa zinazhitajika na idadi ya watu wanaoshiriki.
Utaratibu
Fikiria mawali yafwatayo
Anza na maswali ya tathmini yaliyotambuliwa.
- Je, kuna mchanganyiko wa ishara za matokeo na mchakato
- Je, kuna mchanganyiko wa ishara za viwango na za sifa?
- Fikiria changamoto zinazotokana kama ilivyoelezwa kwene Hatua ya 5 ya kitabu hiki, ambazo zikiwepo zinaweza kulet utata. Hii inamaanisha nini? Kwa mfano:
- Utatumia takwimu zilizopo au utapata takwiu mpya?
- Ishara unazopanga kutumia yanafaa kwa maeneo yako au yameamuliwa kutoka nje?
- Mchakato wa kuksanya ushahidi unajenga uwezo wa wenyeji kufanya M&E au unatumia wataalam kutoka nje?
- Ungependa kutathmini mafanikio ya shughuli zilizopangwa au kujifunza kutokana na matokeo yasiyotarajiwa ya kazi yako, au yote mawili?
I. Tambua ushahidi upi na ishara zipi kutumia
Maswali mengi ya tathmini yanahitaji uchanganye aina tfauti ya ushahidi ili kupata picha kamili inayoonyesha yaliyotokea. Angalia swali moja la tathmini na fikiria aina za ushahidi zitakazotumika kulijibu.
II. Linganisha aina tofauti za ushahidi
Zoezi hili linasaidia kulinganisha faida na hasara za aina tofauti za ushahidi.
- Kutoka zoezi la kuchangia mawazo Sehemu ya I), pitia faida na hasara za kila aina ya ushahidi, pia fikiria ni kitu gani kinakushangaza juu zao. Hakikisha kufanya hii kwa ufanisi wa gharama. Tumia mfano kutoka PRPR hapo chini kama mwongozo:
Mfano wa swali la tathmini: Je, shughuli zilizolengea usimamizi wa kupunguza ukali wa mlipuko wa kutu ya majani zilikuwa na ufanisi gani?
Mchango mawazo kwa mfano wa PRPR huko Chiquimula, Guatemala ungeweza kuwa na matokeo yafwatayo:
- Maoni binafsi kutokana na mahijiano ya wakulima
- Asilimia ya matukio ya kutu
- Kiwango cha uharibifu wa milipuko ya kutu
- Kipato cha wastani cha mwaka kwa mkulima mdogo wa kahawa kwa eneo hilo
- Upangaji kwa orodha ya ushindi wa mbinu mbali mbali za kudhibiti kutu uliofanywa na wakulima
Kwa kila aina ya ushahidi, fikiria faida, hasara na vipengele maslahi. Kumbuka kuangalia ushahidi kulingana na uwezo wake kujibu maswali yako ya tathmini. Fikiria kama inawasilisha hali yako halisi, urahisi wa upatikanaji na ukusanyaji na kama ni sahihi na hazijapitiwa na muda.
Mfano wa PRPR kutoka Chiquimula, Guatemala unaweza kusababisha matokeo yafwatayo (angalia Jedwali la 42):
- Ukishatathmini ushahidi sasa unaweza kulinganisha sehemu nzuri na mbaya ya kila moja ili kujenga uelevu wa kina zaidi juu ya taarifa ambazo unatakiwa kuzikusanya.
- Rudia mchakato huu kwa kila swali la tathmini
- Kumbuka kuwa watu tofauti watakuwa na maoni tofauti juu ya nini ni faida, nini ni hasara na nini ni kipengele cha maslahi. Hivyo, pengine ni wazo zuri kurudia zoezi hili na watu wa makundi tofauti (wanawake, wakulima wadogowadogo, wakulima walio na mashamba makubwa zaidi au aina tofauti za biashara, mashirika,n.k.) ili kuangalia kama tofauti yoyote itaibuka.
III. Unda mpango wenye uhalisi na wa ufanisi wa gharama wa kukusanya ushahidi
- Ukiwa umeshafikiria faida na hasara za aina tofauti za ushahidi, andaa mpango unaoonyesha kwa ufupi ushahidi na ishara utakazopenda kukusanya, pamoja na mbinu unazopanga kutimia kukusanya ushahidi huu.
- Fikiria dhana zozote, mahitaji ya rasilimali au pungufu za mbinu hizi. Hii inaweza kufanyika kwa kutumia sampuli ifwatayo (Jedwali la 40)
Jedwali 41: Mfano wa utathimini wa ushahidi mbali mbali tofauti
Ushahidi | Faida | Hasara | Dodoso |
Maoni binafsi kutokana na mahojiano na wakulima |
|
|
|
Asilimia ya matokeo ya kutu ya majani |
|
|
|
Ukali wa matokeo ya kutu |
|
|
|
Kipato cha wastani cha mwaka kwa mkulima mdogo mdogo kwa maeneo haya |
|
|
|
Mpango cheo wa wakulima wa mbinu mbali mbali ya kusimamia kutu |
|
|
|
Jedwali 42: Mfano wa mpango wa kukusanya ushaidi kutoka Kesi ya Utafiti ya Chiquimula, Guatemala
Swali la Uthibiti | Mbinu Mmojawapo | Dhana au hali ya kuruhusu mbinu iwe na faida | Mahitaji ya kuweza kutekela mbinu hii | Upungufu wa mbinu hii |
Je, kile ulichofanikiwa kinalingana na ulichotegemea kutokea? (Yaani, SD tatu zilianzishwa na wazalishaji 75 walipata mafunzo ya kudhibiti mashambulizi ya kutu ya majani?) | Kukamilisha Jedwali 45 hapo chini pamoja na watu waliotekeleza mbinu dhibiti. |
|
| Baadhi ya shughuli kutotekelezwa inaweza kuonekana kama 'kufeli' na hivyo watu kutopenda kuzungumzia au hata kufichwa kabisa, badala ya kufanya hii kuwa fursa ya kujifunzia. |
Je, shughuli zilitendwa kwa kuzingatia ufanisi, gharama nafuu, na kwa wakati unaofaa? | Jadili kwa makundi ya watekelezaji juu ya maana ya maneno: 'ufanisi', 'gharama nafuu', 'kufaa' na 'muda mwafaka' Eleza sifa ya kila neno kwa kuzingatia uzalishaji wa kahawa. Thibitisha shughuli za utekelezaji kwa kuzingatia ubora wa mafanikio yaliyotokea. |
|
| Idadi ya takwimu inategemea majadiliano, kiwango cha kujihusisha na pia uelevu unaojengeka. Majadiliano yasipowezeshwa vizuri, baadhi ya makundi au watu wanaweza kutawala na hivyo kusababisha upendelezo wa matokeo. |
Je, mahitaji yalitosha kutekeleza shughli zote zilizopangwa? (Jei, afisa ungani walitosha kwa SD? Fedha zilitosha kwa kuanzosha vitalu na kusambaza miche?) | Ukusanyaji wa takwimu za idadi za pembejeo (mf. mbolea, nguvukazi, umwagiliaji, madawa ya kudhibiti wadudu, n.k.) Linganisha gharama za pembejeo zilizotegemewa na halisi Majadiliano kuhusu sababu zinazosabaisha tofauti kati ya gharama za pembejeo zilizotegemewa na halisi, pia kidokezo ya hii kwa mradi. Je, ungerudia mradi tena, ni nini ungebadilisha? |
|
| Utathimini wa utoshelezi utakuwa na sura nyingi, hivyo ni muhimu kujadili maana ya “kutosheleza” kweye muktadha yako kabla ya kujaribu kujibu swali hili. |