Muhtasari

Kwenye tathmini, suahidi unapitiliwa ili kutathmini maendeleao, hatua zifwatazo zinatambuliwa na mafunzo yanawasilishwa kwa wengine. Hatua hii ni fursa ya kuwaunganishwa watu maalum ili kubadilishana mitazamo juu ya vile vilivyoenda viziri, nini imesaidia na nini imekwaza na kama uwezo wa ujasiri umeongezeka. Hii inawza kufanyika kwa kupitia warsha ya mafunzo.

Mbinu
  • Warsha ya mafunzo kwa wahudhuria wote wa mradi ili kutathmini taarifa zinazoibuka kutoka ukusanyaji wa takwimu (inahusu makundi maalum na zoezi la kupanga orodha ya ushindi)
  • Kutumia njia ya simulizi zaidi ambayo inakidhi uhalisia uliopo k.m njia ya video, picha, n.k
Matokeo
  • Uelewa wa kina zaidi juu ya ushahidi uliokusanywa ili kusaidia kujibu maswali ya tathmini
  • Utamabuzi wa mapengo kwenye upatikanaji wa takwimu na changamoto za dhana uu Hadithi za mabadiliko' zinazoeleza jinsi mradi ulivyojenga uwezo na kuongeza utengafu dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi

Nadharia

Inaweza kuwa na manufaa kwako kurejea maswali yako ya tathmini na njia yako ya mradi kwa ajili ya tathmini hii. Maswali yako ya tathmini ni sehemu nzuri pa kuanzia na inaweza pia kutoa umbo la kujenea tathmini yako, wakati njia yako ya mradi inweza kukusaidia kuelewa nini umejifunza juu ya dhana ulizotambua mwanzoni na matokeo uliyoyatarajia.

Ni muhimu kuwapa wale waliohudhuria kwenye ukusanyaji wa ushahidi nafasi ya kuona matokeo ya mchakato huo na walete maoni yao. Kwa kuwakilisha hii kazi ya tathmini kwa watu maalum, wakiwemo pia wakulima, inaweza kuchukua muda mrefu zaidi kuliko timu ya utathmini ikihusishwa peke yake, lakini kuna manufaa mengi, k.m.:

  • Inatoa nafasi ya kuangalia kiwango cha uaminifu wa takwimu zilizokusanywa, na hivyo kuzifanya ziwe bora na zene kina.
  • Waliohudhuria wanaweza kuona mawazo yao yalipowakilishwa na mazoea yao yanapolingana na yale ya makundi mengine na pali pasipo na makubaliano.
  • Kuna fursa ya kujifunza kwa pamoja kati ya wahudhurua kwa kuunganisha mitazamo tofauti, kuangalia palipo na chati na kuvutia maswali kwa ajili ya fikra za ziada.
  • Inaongeza uaminifu wa wahudhuria juu ya ujuzi wao na uwezo wa kuchangia michakato ya maamuzi, na uwezo wao wa kukosoa dhana za ujenzi wa ujasiri, na hii ni muhimu kwa kujenga ujasiri kwa miaka ya mbele.
  • Inaboresha uelewa wa mifumo ya uzalishaji wa kahawa kwa ujumla na wapi mabadiliko yanahitajika ili kuhakikisha ujasili upo kwa muda mrefu
  • Hatua zozote zitakazopangwa kufwata zitakuwa na uhusiano zaidi na zitakuwa muhimu zaidi ikiwa zimetayarishwa kwa pamoja na wale waliohusishwa kenye utekelezaji.

Ushahidi unaweza kuchanganuliwa ili ujibu maswali maalum ya tathmini. Kwa mfano, kwa swali “Nini ni njia fanisi zaidi za kupunguza kutu ya majani?”, maandidhi ya utafiti kesi na ushahidi kutokana na mahojiano na wakulima zinaweza kujumuishwa kwenye jedwali , k.m.

Jedwali hii ingeweza kuwasilishwa kwa wakulima tena kwenye semina ya mafunzo au mahojiano ili kupata maoni kuhusu kama wanafikiri hii ni sawa, nini kinakosekana na maswali mapya yanayotokana na ufumbuzi huu.

Hata hivyo, kama maswali yako ya tathmini yalikuwa yakiuliza kama ujasiri umejengeka na wakulima, utambuzi wa sifa za ujasiri unaweza kuhitaji tathmini ya uwingi wa kiwango cha ubora wa sifa hizi kuonekana kwenye kazi hadi leo. Hii inapaswa imulikie vitu vinavyoenda vizuri na sehemu zinazohitaji kufanyiwa maboresho. Nukuru matokeo maalum kutokana na shighuli hii kwenye jedwali ya vigezi vya mpambo wa M&E, angalia Sehemu ya 2, Hatua ya 5.

Meza 19: Mfano wa Tathmini ya Mbinu la Makabiliano

Unafuu

Kukubalika na wakulima

Majira

Ufanisi

Kupanda aina A iliyo sugu dhidi ya kutu ya majani

***

*

**

*

Kupanda aina B iliyo sugu dhidi ya kutu ya majani

**

*

**

-

Kupanda miti ya kivuli

*

***

*

**

Kuanda ukanda juu ya futi 1,000 tu

n/r

n/r

*

***

*** = vizuri sana, ** = vizuri sana, * = vibaya, - = poor, n/r = lisilo husika

Mwongozo wa vitendo

Lengo

  • Kuhakikisha kuwa matokeo yanaweza kuaminika
  • Kuleta maana ya aina tofauti za ushahidi ili iweze kutumika kajibu maswali ya tathmini.

Matokeo tarajiwa

  • Tathmini ya ushahidi kulingana na inavyojibu maswali ya tathmini
  • Ujumbe muhimu kutoka mchakato wa tathmini ambao unaweza kutumika kwenye kusambazaji
  • Kukamilisha sehemu D ya mpango waku wa tathmini

Muda unaohitajika

itategemeana na mbinu itakayotumika, idadi ya watu watakaoshiriki na ukina wa taarifa zinazohitajika.

Mwongozo

Uthibitisho

Ni muimu kuthibitisha kuwa ushahidi uliokusanywa ni sahihi na unaaminika. Kusahihisha taarifa inachukua muda, lakini inaongeza uborawa takwimu kwa kiwango kikubwa. Kuhakikisha na walioshirikishwa itakusaidia kupata uelevu wa kina zaidi juu ya maswala na kuruhusu kupata maoni mengine yaliyokuwa yamefichika. Ni muhimu kuwa wazi juu ya nini kinacothibitishwa. Kwa mfano, pengine ungependa:

  • kuthibitisha nani amehudhuria na maoni ya nani hayajawakilishwa
  • kuthibitisha palipo na makubaliano na watu walipokuwa na mawazo tofauti
  • kuhakikisha kuwa mawazo yaliyowakilishwa ni mawazo ya ukweli ya watu na kuwa mafunzo yanayoibuka kutokana na zoezi yameeleweka na kuwakilishwa vizuri.

Shukrani kwa (matamshi/mawasiliano binafsi)

Utaratibu

  • fikiria kupanga semina ya mafunzo kwa wadau mahumu ambao watatoa ushahidi na watasaidia tathmini (hii itatatua sehemu C and D ya Hatua ya 5). Kwa kila hatua ya tathmini, uamuzi utahitajika kutambua vipengele vya ushahidi vilivyo na umuhimu zaidi kwa kujibu madwali ya tathmini. Inatakiwa uanze hatua ya uchambuzi na seti ya mawazo ambayo hayajajaribiwa na kumalizia na idadi ndogozaidi ya ujumbe mkuu na ushauri. Wawezeshaji watahitajika kuhakikisha kuwa kunukuru, kuwakilisha na kuwekea kipaumbele ushahidi inafanyika na kuwa semina inafwata mpango na madhumuni.
  • Hata kama semina nzimia ya mafunzo haitawezekana, kuna idadi ya mazoezi ambayo yanaweza kutimika na wadau kwenye mahojiano na makundi maalum yatakayokusaidia kukusanya na kuyapanga kwa kipaumbele mafunzo kutokana na ushahidi.
  • aza sampuli ya mpango wa M&E ili kukusaidia kupanga shughuli za mbele.

Mbinu za kiufundi

  • Zana nyingi shirikishi zilizotajwa awali kwa ukusanyaji wa takwimu zinaweza pia kutmika kwenye hatua ya uchanganuzi, kwenye mbinu kama ya ramani ya maongezi, mito ya maisha, upangaji orodha ya ushindi, michoro ya H, uwanja wa nguvu, na kama muda ukiruhusu mbinu za maelezo zaidi kama vile picha shirikishi au mafunzo ya historia. Hizi zote zimeelezwa zaidi mwishoni mwa Sehemu hii.
  • Semina ya mafunzo pia inasaidia kutambua mazoezi yanayowawezesha washiriki kuhama kutoka uelewa kwa ujumla (k.m. kuchangia mawazo) kuelekea kwenye mtazamo wa kiini juu ya maswala nyeti. Hii itawaruhusu kutoa mafunzo nyeti na ujumbe kwa wote na kutambua hatua za muda mfupi, muda wa kati na muda mrefu za kujenga ujasiri dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi.

Mazoezi yanayoweza kusaidia kutekeleza vipengele maalum vya uchanganuzi ni pamoja na:

Kuamua kama shughuli zilitekelezwa kwa ufanisi, gharama nafuu, kwa njia inayofaa na kwa muda

Kwa kila shughuli iliyotekelezwa kwenye mchakato wako wa makabiliano, tathmini matimizo ya vigezo vya ufanisi, gharama, kufaa na muda. Pengine hii itahitaji majadiliano ya awali juu ya maana ya maneno haya kwa kupitia uhusiano wa malengo ya mchakato wa makabiliano, yaani, watu walioshirikishwa kutekekeza mradi wanahitaji kutambua maana ya kienyeji ya kila neno kulingana na mfumo wao maalum wa uzalishaji wa kahawa.

Tumia Jedwali kama iliyopo hapo chini ili kunkuru ufafanuzi huu (Jedwali la 43).

Jedwali la 43: Kutathmini utekelezaji wa shughuli za makabiliano

Vigezo

Bora

Kuridhisha

Dhaifu

Kutoridhisha

Ufanisi

Shughuli ilifanikisha malengo yaliyotegemewa kwa ufanisi mkubwa

Shughuli ilifanikisha malengo yaliyotegemewa kwa ufanisi wa kutosha/bahasa

Shughuli ilionekana kufikisha malengo yaliyotegemewa kwa udhaifu

Shughuli haikufikisha malengo yaliyotegemewa

Gharama nafuu

Shuguli ilionekana kuwa ya faisha kubwa kulinana na gharama yake

Shuguli ilionekana kuwa ya faida bahasa kulinana na gharama yake

Shughuli ilionekana kuwa ya gharama

sgharama ya shughuli ilikuwa kubwa kias kwamba wakulima hawakuwa tayari kuifanya

Kufaa

Shughuli ilionekana kuwafaa watekelezaji waliolihitaji

Kulikuwa na wasiwasi kidogo juu wa kufaa kwa shughuli kwa watekelezaji

Wasiwasi uliwasilishwa juu ya kufaa kwa shughuli na wale waliotakiwa kutekeleza

Shughuli haiwafai kabisa wanaotakiwa kuitekeleza, k.m. kwa sababu ilikuwa kazi ngumu mno, au haikuendana na utamaduni wao, n.k.

Muda

Shughuli iliendana kwa urahisi na ratiba zilizopo za watekelezaji

Shughuli iliendana kwa urahisi na ratiba zilizopo za watekelezaji

Kulikuwa na wasiwasi juu ya mwingiliano kati ya shghuli na ratiba zilizopo

Muda uliohitajika kuteleleza shughuli haukuendana kabisa na ratiba zilizopo

II. Kutathmini ufanisi wa ushiriki wa wadau

Ujasiri dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi unahitaji muunganiko kati ya watu tofauti wanaohusika kwenye uzalishaji wa kahawa pamoja na mitandao yao,k.m. kati ya jamii, serikali au biashara. Inahitaji pia michakato kuwa rahisi kubadilika na fursa za kujifunza kutokana na shughuli zinazotendekaili kuhakikisha kuwa mafunzo yanatumiaka kama taarifa kwa mipango ya mbele. Mwishoni mwa mchaato wa makabiliano, ni muhimu kutathmini kiwango cha mchango wa wakulima na wadau wengine kwenye ufumbuzi wa umbo, utekelezaji na tathmini ya mradi.

Jedwali inayofwata inatoa ushauri mchache kuhusi ukusanyaji wa ushahidi uneoweza kujibu maswali juu ya kiwango cha kuhusishwa kwa wadau kwenye umbo na maamuzi, au uwekezaji wa wadau kwenye mbinu shirikishi 37. Jisiie huru kubadilisha na kuongezea orodha hii kama utakavyohitaji. Maswali haya yanaweza kujibiwa kwa kupitia majadiliano ya vikundi maalum, mahojiano ya ana kwa ana, au kwa semina. Bila shaka kutakuwa na maoni tofauti kuhusu ubora na viwango vya mahudhurio. Lakini kwa kupitia majadiliano haya, itaanza kuwa wazi nini ni maana ya mchango wenye maana kwa wakulima na kama wao (pamoja na wadau wengine) walijiskia kuwa fursa za kuhudhuria zilifaa na kuwa za kutosha, na kama la, jinsi gani kuboresha mchakato kwa nafasi nyingine.

Jedwali 44: Mfano wa kukusanya ushaidi kutoka kwa mahusishi ya wadau

Maswali kuhusu uhusishi ya wadau

Mfano wa Viashiria

Nani au nini iliamuwa masharti ya utekelezaji?

  • Wakulima wadogo wa kahawa na jamii iliyopo wanahusika sawasawa kwenye kuweka sheria na maada ya mradi

Je, usawa wa nguvu za watu na taasisi tofauti ukoje?

  • Wakulima wa kahawa (na wakilishi wa jamii iliyopo) wana nguvu sawa na wadau wengine

Je, ni wakati gani kwenye mchakato ndipo wazalishaji wa kahawa na jamii za karibu zinahusishwa?

  • Wakulima wa kahawa na wakilishi wa jamii iliyopo (kama inafaa) wanahusishwa katika vipengele vyote vya mradi

Nini ni kiwango cha hiari/uamuzi wa wakulima wa kahawa na jamii za karibu juu ya maamuzi

  • Wakulima wa kahawa na wakilishi wa jamii iliyopo wanapewa fursa ya kuwa na taathiri na nguvu.

Ni mazingio yapi yanafanwa kuendeleza na kuhimili ushiriki wa wakulima wa kahawa (na jamii iliyopo)?

  • Mradi unawekeza muda, fedha na rasilimali za kutosha kuwezesha mahudhurio

Je, mkakati wa ushiriki unaruhusu njia tofauti za mchakato kwa wakulima na wawasilishi wa jamii?

  • Umakini unakuwepo kwenye kuimarisha mbinu zote za mahudhurio ya wakulima wa kahaaw na jamii zilizopo

Je, mikutano inafikiwa na wote?

  • Mikutano inafiliwa na wakulima wa kahawa na mawakilishi wa jamii zilizopo.

Je, mikutano ya mradi inaendeshwa kwa ufanisi na umoja?

  • Mikutano ya mradi inafanya kazi kwa ufanisi, uwazi na umoja. (tafadhali zingatia: maneno “ufanisi”, “uwazi” na “umoja” yanahitaji kufafanuliwa kabla ya kujibu hili.)

III. Muhtasari wa ujumbe mkuu juu ya shughuli zilizokuwa na mafanikio zaidi

Itasaidia kutumia zoezi la orodha ya ushindi kutathmini jinsi gani wahudhuria tofauti walivyoona kila shghuli ya mchakato wa makabiliano. Kuna njia nyingi za kufanya zoezi la orodha a ushindi. Njia rahisi ni kuwapa wahudhuria mawe manne (au kitu chochote kingine, kama vile peremende) na kuwaomba kuziweka kwenye Jedwali ilipotayarishwa kwenye karatasi kubwa. Kwa mfano, kama ungekuwa unalinganisha shughuli tatu, basi Jedwali la 45 lingeweza kutumika.

Kama mhudhuria alifikiri kuwa shughuli ilikuwa na ufanisi sana, yenye gharama ndogo, na kufaa kwa wakulima, lakini muda wake ulikuwa mbaya sana, mawe yake yataonekena kama ilivyo kwenye Jedwali la 45 hapo chini. Ungwaomba wahudhuria waano wengine kuweka mawe yao, unaweza kupata itu kinachofanana na Jedwali la 46.

Kutokana na zoezi hii,wawezeshaji wanaweza kuanza kuona vielelezo na kuvijadili kwenye kikundi. Kwa mfano, mwezeshaji anaweza kuuliza, “Inaelekea kuwa kuna makubaliano kwa kiasi fulani juu ya muda mbaya wa shughuli hii, na kama ni hivyo, kuna yeyote angependa kunieleza zaidi juu ya hilo?” Au, “Inaelekea kuna maoni yanayotofautiana sana kuhusu udanisi wa shughuli. Je, yule anayefikiria shughuli kuwa 'fanisi sana' anielezee sababu za mbinu lake, na yule aliyechagua “si fanisi kabisa” naye aeleze sababu ya mbinu lake.”Kawaida ni wakati wa majadiliano haya mafunzo muhimi zaidi yanaibuka.

Jedwali 45: Mfano wa kutathmini shughuli kwa kutumia zoezi la cheo (Mtu mmoja amejibu)

Vigezo

Bora

(++)

Kuridhisha

(+)

Dhaifu

(-)

Kutoridhisha

(--)

Ufanisi

*

Gharama nafuu

*

Kufaa

*

Muda

*

Jedwali 46: Mfano wa kutathmini shughuli kwa kutumia zoezi la cheo (Watu 5 wamejibu)

Vigezo

Bora

(++)

Kuridhisha

(+)

Dhaifu

(-)

Kutoridhisha

(--)

Ufanisi

**

*

*

**

Gharama nafuu

**

***

*

Kufaa

****

**

Muda

*

*****

IV. Zana na mazoezi shirikishi za ziada

Kuna zana nyingi na mazoeza mengi shirikishi zinazoweza kukusaidia kwenye majadiliano ya ana kwa ana na wakulima, makundi maalum au kama sehemu ya semina ya mafunzo ili kukusanya takwimu na kuzichuguza ka kina zaidi. Mazoezi na zana hizi zinaweza kuwasaidia wahudhuria kupanga uelevu wao wa mahusiano yenye utata, mwongiliano na athari. Hizi zimeorodheshwa kenye Jedwali la 47 na kuelezwa kwa kina zaini mwishon mwa sehemu hii.

Pamoja na tathmini ya mchakato wa makabiliano kwa ngazi ya shamba, pengine ingekuwa na maana pia kufikiria jinsi gani kutatua vipengele pana zaidi vya mfumo wa uzalishaji wa kahawa. maafisa ugani, wakufunzi au watu wengine wanaotumia mpango wa c&c wanaweza kutimia Jedwali la 48 kama mwongozo wa kufikiria jinsi gani ujasiri dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi yanaweza kujengwa kwa uzalishaji wa kahawa kwa kiwango kikubwa zaidi. Mazoea mazuri kwa ngazi ya shamba yanahitaji kuchochewa na mazoea mazuri kwa sehemu nyingine za mfumo wa uzalishaji wa kahawa ili makabiliano dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi yawe na mafanikio mazuri iwezekanavyo.

Orodha hii itakusaidia kutambua nguvu na udhaifu na kufikiria wapa rasilimali ziwekezwe ili kujenga uwezo wa muda mrefu wa ujasiri kwa mfumo wa kienyeji wa uzalishaji kahawa.

Kwa mfano, uwezo wa kuelewa taarifa mpya juu ya mabadiliko ya tabia nchi ili kutathmini nihatarisho vipya ni fani muhimu ya kuzingatia kwenye maamuzi juu ya makabiliano dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi. Afisa ungani anapaswa kufukiria, kwa mfano, uwezo wa wakulima kutathmini na kuelewa taarifa mpya za mabadiliko ya tabia nchi. Wanatakiwa wafikirie jinsi gani wanaweza kuwasaidia wakulima kwenye swala hili na kipaumbele cha ujenzi wa uwezo huu. Wanaweza kuamua kuwa haina kipaumbele kulingana na shughuli nyingine zilizo muhimu zaidi, kama vile kuanzisha mitambo mipya ya umwagiliaji.

Jedwali 47: Mifano ya Mbinu husishi na mazoezi ya Tathimini

Mbinu husishi maalum

(kwa matumizi kwenye mahojiano, makundi na semina)

Mazoezi mengine ya picha na masimulizi

(muda na malighafi zaidi zinahitajika)

  • Mistari ya Wigo
  • Maigizo Husishi
  • Michoro ya H
  • Video Husishi
  • Mashamba kikosi
  • Hadithi za Picha Husishi
  • Mto wa Maisha
  • Ramani na GIS Husishi
  • Ramani ya Mazungumzo
  • Ramani ya Matokeo
  • Zoezi la Cheo
  • Mafunzo ya Historia