Tumia matokeo na toa mapendekezo kwa mipango ya mbele
Muhtasari
Ili tathmini iwe na uzito, lazima iwasilishwe kwa uwazi kwa wale watakaokuwa na taathiri ju ya mipango ya mbele, pamoja na wengine ambao wangeweza kunufaika kutokana na mafunzo (k.m. wasimamizi wa programu, maafisa ungani wa zao la kahawa, na wakuliwa wengine wa kahawa).. Ni muhimu kwa hatua hii kufikiria nyuma hadi Shughuli A) Madhumuni ya tathini na B) Maswali ya tathmini. Hizi zingetungwa pamoja na wadau wakuu – yaani, walisema kuwa walitaka mchakato wa M&E kufikia malengo yapi? Jibu la swali hili litasaidia kuchanganua taarifa ipi inapaswa kuwakilshwa kwa vikundi gani.
- Andaa mpango wa kubadilishana matokeo na wasikilizaji tofauti tofauti na kwa namna mbalimbali
- Nukuru ya mafunzo na utayarishaji wa ripoti fupi kwa ajili ya c&c toolbox
- Uwasilishaji wa ujumbe kwa njia ipasavyo juu ya mbinu zilizotekelezwa
- Utambuzi wa nafasi za kuingiza masomo kwenye mipango ya mbele
Nadharia
Pamoja na kutoamapendekezo kwa muda wa mbele, pia ni muhimu kwamba mafunzo yaliyofankika yaathiri utayarishaji wa mipango ya hatua zinazifwata. Jedwali ya rahisi sana inayopanga taarifa juu ya tarehe za kufanya maamuzi juu ya mipango inaweza kusaidia kupanga ukusanyaji wa takwimu na tathmini ya mahitaji ya kufanya uamuzi, hasa pale maamuzi yanapokuwa na athari za muda mrefu (k.m. mbinu juu za kupanda aina mpya ya kahawa au kuchagu wapi kuanzisha mashamba mapya).
Mwongozo wa maswali kwa ajili ya kutumia matokeo:
- Nani atanufaika na kusikia juu ya yaliyotokea?
- Fursa zipi zipo za kuleta mafunzo ili kutaarifu na kuboresha mipango ya mbele, na nani ana uamuzi juu ya hilo?
- Mafunzokutoka tathmini yatawakilishwa na kutamkwa kwa njia gani
- Maendeleo juu ya mapendekezo yatachnguzwaje na kutathminiwa?
- Ungewezaje kuendeleza mafunzo zaidi?
- Ni maswali gani ya ziada tunapaswa tuyaulize?
Fikiria kwa makini juu ya hadharia unaotaka wafaidike na matokeo na ujumbe unaotaka wapate na njia bora ya kuwafikishia. Kwa mfano, inawezekana kuwa baadhi ya wataalamu wa sekta ya kahawa wangependa taarifa za kiufundi wakati wengine wangependa muhtasari wa matokeo (watunga sera hupenda taarifa fupi na kamili zilizowakilishwa kwa kurasa chache). Kinyume na hayo, kuwasilisha ujumbe muhimu kwa wakulima inaweza kumaanisha kutoa repoti kwenye mikutano, kupanga warsha au matangazo siku za soko au kutumia redio za kienyeji. Fikiria usambazaji wa taarifa mapema ili uweze kuingiza gharama zake kwenye mpango wako wa fedha. Nukuru matokeo muhimu ya shighuli hii kwenye jedwali ya vigezo vya mpango wa M&E, angalia Sehemu ya 2, Hatua ya 5.
Kubadilishana mazoea na utafiti kesi kwa kupitia sanduku la Vitendeakazi vya c&c (c&c toolbox)
Njia moja rahisi na yenye ufanisi ya kubadilishana nmazoea yako ya utekelezaji wa shghuli za makabiliano ni kujaza jedwali ya utafiti kesi kwenye Sehemu ya 2 na kuiweka hii kwenye sanduku la Vitendeakazi vya c&c (c&c toolbox). Mbinu za makabiliano zinazoonyesha matokeo yaliyotarajiwa na yanayleta matumaini ya sululisho la kuongeza uwezo wa ujasiri ni mifano mizuri kwa wengine kutoka sekta ya kahawa.
Sanduku la Vitendeakazi vya c&c (c&c toolbox) inakuwa ikipitiliwa na kufanyiwa marekebisho mara kwa mara. Tunakushauri uwe sehemu mojawapo ya mtandao wa c&c kwa kuiongezea mazoea yako. Hii inweza kufanyika kwa kubuni utafiti kesi zako mwenyewe za kutekeleza mbinu maalum ya makabiliano na kuiwakilisha kwa wengine kwa kupitia mtandao wa c&c. Taarifa zaidi juu ya utafiti kesi zinapatikana kwa mawasiliano ya moja kwa moja na timu ya c&c (c&c team).
Orodha ya tovuti na vituo vya taarifa
Zifwatazo ni vyanzo vyenye anufaa kwa kuppata taarifa zaidi juu ya tabia bora za M&E
UKCIP’s AdaptMe Monitoring and Evaluation for adaptation tool: www.ukcip.org.uk/wizard/adaptme-toolkit/
SEAChange: a Community of Practice on M&E and evaluation for adaptation to climate change www.seachangecop.org/
Learning to ADAPT: monitoring and evaluation approaches in climate change adaptation and disaster risk reduction – challenges, gaps and ways forward www.ids.ac.uk/files/dmfile/SilvaVillanueva_2012_ Learning-to-ADAPTDP92.pdf
CARE’s Community-Based Adaptation Toolkit www.careclimatechange.org/files/toolkit/CARE_ CBA_Toolkit.pdf
CARE’s Manual “Participatory Monitoring, Evaluation, Reflection and Learning for Community-based Adaptation” (PMERL) www.care.org/sites/default/files/documents/CC- 2012-CARE_PMERL_Manual_2012.pdf
World Resources Institute report “Making Adaptation Count” providing concepts and options for Monitoring and Evaluation of Climate Change Adaptation pdf.wri.org/making_adaptation_count.pdf
UKCIP Guidance Note: “Twelve reasons why climate change adaptation M&E is challenging” www.ukcip.org.uk/wp-content/PDFs/MandEGuidance- Note1.pdf
Mwongozo wa vitendo
Lengo
- Kuhakikisha kuwa matokeo kutoka tathmini yanawasilishwa kwa ufanisi kwa wengine watakaoweza kufaidika nayo
- Kuhakikisha kuwa mabadiliko yanayohitajika yanafanywa kwa mipango ya mbele.
Matokeo tarajiwa
- Utafiti kesi inaandikwa kwa kufwata mpango wa c&c na inawekwa kwenye c&c toolbox iliyo mtandaoni
- Tathmini ya maamuzi ya baadaye yatakayohitajika ili kuzingatia athari ya mabadiliko ya tabia nchi, na muda wa kufanya maamuzi hayo
- Kama inavyohitajika, mpango wa kupeleka mbele shughuli zilizotambuliwa.
- Kukamilisha sehemu E ya mpango wa tathmini
Muda unaohitajika
Kwa wastani, nusu siku kwa kila kesi utafiti. Kujaza sampuli inaeza kufanyika ndani ya dakika 30 hadi saa moja, kulingana na majadiliano ambayo yameshafanyika na kiwango cha uelevu cha kikundi.
Mwongozo wa maswali
- Je,kumekuwa na mwongezeko wa ufahamu juu ya makabiliano dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi kwenye kaya za wakulima na wadau wengine kwa ujumla wanaohusika na mchakato wa utekelezaji? Nani aliongoza hii?
- Ni ushirikiano upi wa wadau uliokuwa na mafanikio zaidi wa kujenga uwezo wa kukabiliana na kwa nini (k.m. mafunzo, matembezi ya shambani, n.k. )?
- Je, mchakato wa c&c, au viengele vyake maalum, unweza kuboreshwa kwa njia gani (k.m. Semina ya Ushahidi wa Tabia nchi, SD, n.k.)?
- Kulikuwa na tofauti gani cha kiwango cha mapokezi kati ya wakulima wa kike na wa kiume kwa tabia mbali mbali? Kulikuwa na tofauti gani kwenye ugumu au urahisi wa kuwashawishi wakulima wa kike na wa kiume kwenye kuzipokea hatua za makabailiano zilizokuwa zikishauriwa?
- Wewe ungepanga kipaumbele gani kwa mbinu mbali mbali za makabiliano zilizotekelezwa, ukizigatia ufanisi wake kwa makabiliano dhidi ya tabia nchi, lakini pia uwezekano wa kutekelezwa na wakulima wa kike na wa kiume, pamoja na familia zao?
- Gharama ya utekelezaje ilikuwaje? Je kulikuwa na gharama (k.m. gharama za mtaji na za uenedeshaji) ambazo hazikutambulika toka mwanzo?
Utaratibu
- Nukuru mafunzo yaliyoibuka kwa kutunga kesi utafiti kwa ajili ya c&c toolbox.
- Tayarisha muhtasari wa vitu ulivyojifunza wakati wa kutekeleza mchakato wa mpango wa c&c (ukigusia shughuli zote za Hatua ya 1 hadi ya 4) kwa kutumia sampuli iliyopo kwenye c&c toolbox. Muhtasari hii inaweza kuwekwa kwenye c&c toolbox ili kuwasaidia wengine kutunga shughuli zao za makabiliano. Sampuli ya kesi utafiti (angalia mfano ukurasa wa 166) inatoa umbo itakayokusaidia kufikiria mafunzo uliyoyapata kulingana na zana ulizotumia na shughuli ulizotekeleza, na pia mambo mengine muhimu kama vile mahudhurio ya wadau na jukumu la jinsia.
- Tumia sampuli za utekelezaji wa mpango na shughuli kuhakikisha kuwa mapendekezo yako yanataarifu mipango ya mbele (zaidi juu ya kupanga utekelezaji na shughuli inafwata hapo chini)
Sampuli za mpango wa utekelezaji na shughuli
Sampuli ya utekelezaji
Ukishapata idadi ya mapendekezo, sampuli hii inweza kukusaidia kupata mwelekeo wa kipaumbele na kuona urahisi wa kutekeleza shughuli fulani (k.m. kuingana na gharama, muda, nani atahitai kushirikishwa, n.k.)
Sampuli ya mpango wa shughuli
Sampuli hii inweza kutumia kama una orodha ya mapendekezo kutoka tathmini ambayo ungependa kuweka katika mipango ya mbele.
Zana shirikishi za tathmini
Lengo
- kupata na kugawanya taarifa za msingi kwa kufwata sprektra kutoka upande mmoja hadi mwingine.
- Kupata na kugawanya taarifa za msingi kwa kufwata mwelekeo mmoja tu wa swala, k.m. kiwango, upana au kiasi cha kitu fulani.
Wapi pakutumia mistari ya spektra
Mistari ya spektra ina matumizi tofati.Inaweza kutimika kukusanya taarifa za kimsingikuhusu nani aliyehudhuria kwenye vipindi vya mafunzo au shughuli za c&c na hisia za wahudhuria kuhusu msaada waliopewa. Inatoa maoni juu ya kiwango cha imani ya wakulima kujenga ujasiri. Ukitaka kupata takwimu za ziada kwa swali maalum, k.m. kama kuna tofauti kati ya wanaume na wanawake, unaweza kuwaomba wanaume na wanawake kutumia alama za rangi zinazotofautiana.

Jinsi ya kutumia mistari ya spektra
Kuna aina kuu mbili ya maswali unayoweza kuuliza juu ya mistari ya spektra:
- Swali kuhusu taarifa za kimsingi iliyo na viwango vya malengo vinavyoonekana kwenye spektra, k.m. “Shamba lako la kahawa
- Swali linaloulizia maoni au msimamo, k.m. “Kuna uwezo gani kuwa utawashauri wakulima wengine wapate mafunzo uliyopata wewe?” au “Msaada wa kuzalisha mpango wa makabiliano”
Mistari hii ya spektra inakuruhusu kuchunguza zaidi sababu za mhudhuria kuwema alama yake kwenye sehemu maalum ya mstari, ama kwa kumwuliza moja kwa moja au kwa kuwaomba wahudhuria kuweka alama kwenye mstari, kama ilivyo kwenye Umbo la 51 Unaweza kuanza kufikiria mabadiliko yatakayohitajika ili wasogeze alama zao kulia au kushoto. Pia angalia mwenendo kulingana na muda, pamoja na tumaini na mlengo/tamaa kwa kuwaomba wahudhuria kuweka alama zao pale palipo na uhusiano kati ya swali hili kwa kipindi cha mwa mmoja uliopita na wapi wangependa kuwepo mwaka mmoja (au muda wowote ule mwingine) ujao.


Lengo
- Kupata picha ya misaada na vikwazo vya shughuli maalum
- Kutathmini maendelea kwa kuchora michoro ya H kwa vipindi tofauti
- Kuwasilisha upana wa maoni juu ya maendeleo, na misaada na vikwazo vyake
- Kutambua hatua za mbele zitakazokuwa fanisi zaidi kwa kufikia malengo yanayopendwa.
Wakati pa kutumia mchoro wa H
Mchoro wa H unaweza kurekebishwa kwa matumizi ya aina mbali mbali, k.m. kama zana ya kuwasaidia wenyeji kutathmini utendaji wa ushirikiano, programu, wakala na mipango; kama zana ya kutambua ishara za ienyeji kwa M&E, kama njia ya kutambua hatua zifwatazo na kipaumbele za kuchukulia hatua na kwenye kutathmini semina na mafunzo.
Jinsi ya kutumia mchoro wa H
Mchoro wa H una umbo la H pana ambayo inaweza kutumika kwa mazingira tofauti kupima kitu fulani kwenye kipimo kilicho kati ya sifuri na kumi (k.m. uaminifu wa kuitikia mabadiliko ya tabia nchi na tathmini ya kiwango cha mahudhurio ya mkulima kwenye mchakato wa kufanya maamuzi). Inatoa njia ya kuwakilisha kwa vielelezo iliyo rahisi kueleweka majibu ya wahudhuria yanayotathminiwa ili kuona kipi kinaenda sawa, nini inazuia maendeleo na vipi kuboresha hali hiyo.

Lengo
Kuelewa sababu zinazotaathiri hali fulani, ama kwa kuendesha muunganiko kuelekea lengo maalum (kikosi cha kutia moyo) au kuzuia muunganiko huu (kikosi cha kubana au vizuizi). Kikosi hiki kinaweza kuwa tofauti sana, zikibadilika kwa muda na kulingana na mazoea na ujuzi wa wale waliopewa kazi ya kuzitambua. Zinaweza kuunganisha pande kama vile kutia moyo, maadili, tabia za watu, malengo, hofu na dhana, pamoja na pande zakimaumbile zaidi kama vile maamuzi ya kishirika.
Wapi pa kutumia kikosi kazi (kk)
Kikosi kazi kinaweza kutumika kwenye hatua zote za upangaji wa mradi. Inaweza pia kutumika kutathmini sababu ya mchakato wa makabiliano kuendelea kama ilivyo na kupanga jinsi gani mradi unaeza kubadilika mbele. Kikosi kazi kinnasaidia kuelewa sababu nzuri zilizochangia maendeleo na pia vikwazo vilivyotatuliwa.
Jinsi ya kutumia kk
- Kwanza, amua ni swala gani ungependa kuchunguza kwa kutumia kk. Kwa mfano, “kutathmini nini imesaidia na nini imekwaza utekelezaji wa shughuli fuani ya makabiliano”.
- Kisha, watie moyo wahudhuria kuorodhesha vikosi vyote zilizosaidia utekelezaji wa shughuli za makabiliano, na kuziandika kwenye vipande vya karatasi iliyo na mishale upande mmoja wa karatasi.
- Orodhesha nguvu zote zilizozuia utekelezaji wa mpango wa shughuli na iweke upande wa pili wa karatasi hizo. Kila nguvu ya kuendesha au kukwamisha inaweza kuwekewa orodha ya ushindi kwa kuwekwa karibu au mbali na kitovu cha karatasi, ili kuwakilisha kiwango cha nguvu hiyo.
- Watie moyo wahudhuria kuchunguza jinsi gani ugeweza kuziongeza nguvu za kuendesha na kupunguza nguvu za vikwazo. Unaweza kutambua hatua zinazofwata za kutekeleza hayo. Kwa mfano, kwenye mchoro hapo chini,mojawapo ya vitu vinavyokwaza maendeleo imeorodheshwa kama “ taarifa juu ya mabadiliko ya tabia nchi inaelekea ktokuwa na uhakika”. Kwa sababu haitawezekana kuongeza uhakika wa taarifa hiyo, pengine unaweza kujadili jinsi gani maamuzi yafanyike ingawa hakuna uhakika, k.m. kwa kuchunguza maamuzi ya “kutojuta”, ambayo ina manufaa hata pale pasipokuwa na uhakika wa mabadiliko ya mbele ya tabia nchi.

Lengo
- Zoezi la Mto wa maisha linaweza kutumika kwa kufikiria juu ya maendeleo ya mchakato wa makabiliano hadi leo, kutambua nini kilichoenda vizuri na changamoto zilizojitokea.
- Kubadilishana mitazamio tofauti juu ya mradi huo huo na kutambua wapi panafanana.
Wapi pa kutumia mito ya maisha
Zana hii inaweza kutumika kuwasaidia watu kupata kufahamiana, kuzingatia uhusiano kati yao, kuchunguza matumaini na hofu juu ya ushirikiano wao, kufikiria viti vinavyoshangaza au vilivyo vigumu kwenye mradi ambao sasa umefikia mwisho wake.
Jinsi ya kutumia mito ya maisha
- kwa kutumia picha ya mto, waombe wahudhuria kuchora picha inayowakilisha mazoea yao ya kushirikia mchakato wa makabiliano. Wanaweza kuchora picha ya mtu mmoja mmoja au picha kwa kikundi kizima. Waombe wafikirie mazoea yao na kutambua pande nzuri zilizotekelezwa, mbinu muhimu (ikiwakilishwa na mito midogo) na changamoto au vikwazo walivyokumbana navyo (maji iliyovurugika, miamba, mamba). Picha nyingine (mitumbwi, samaki, madaraja, miamba, maeneo enye matope, maji mafupi n.k.) zinaweza kuwakilisha pande mbali mbali za safari.

Lengo
- Kuwakilisha maoni ya washiriki juu ya pande tofauti za hali, ikiwemo pia maswala,watu,matatizo, michakato, uhusiano, migogoro na uendeshaji.
- Kuwakilisha vitu vinavyoonekana kuwa muhimu kwa wahudhuria, sababu zao za kujiskia wamekwama nawapi wangeanza kutafuta mbinu za kuboresha hali.
Jinsi ya kutumia Picha zilizokuzwa
- Picha zilizostawi zinaweza kutumika kwenye hatua ya tathmini ili kuwakilisha maoni juu ya madhumuni ya kutathmini mchakato wa makabiliano
- Kulingana na maswali yanayoulizwa, picha zilizostawi zinaweza pia kutumika kulinganisha mazoea tofauti ya mchakato ule ule na sababu za kuwa na mazoea haya yanayotofautiana, au jinsi wahudhuria tofauti wanavyothamini pande tofauti.
Mara nyingi wahudhuria wanakuwa na mashaka juu ya ubora wa michoro yao, lakini wanazalisha picha zinazowakilisha mawazo yao na hofu zao vizuri sana, hata kushinda majibu ya moja kwa moja kwenye mahojiano. Hapo chini kuna mifano michache y á michoro ya picha zilizostawi inayowakilisha jinsi gani kikundi cha wahudhuria kilivyohisi mchakato wa makabiliano walioshirikia.
Wapi pa kutumia picha zilizokuzwa
- Anza na karatasi kubwa na peni nyingi za rangi tofauti na waombe washiriki kuchora kile wanachokiona kinatokea kwenye hali fulani, au kutokana na maombi fulani. Wanatakiwa watumie picha kuwakilisha hali yao kwa njia inayoweza kuwasilishwa kwa watu wengine. Kazi hii ichukue muda wa dakika 10 hadi 15.
- Wape maelekezo kama ifwatavyo:
- “Chora picha inayoeleza mazoea yako ya kushiriki kwenye mchakato huu”
- ”Chora picha inayoeleza hisia zako za sasa juu ya mwitoko shidi ya mabadiliko ya tabia nchi”
- Waombe waeleze picha zao kwa wahudhuria wenzao au kwa kikundi kizima (kama watakubali). Kubadilishana picha zilizostawi tofauti juu ya maoni ya watu juu ya mchakato wa makabiliano inakuruhusu kutambua viungo, tofauti, fursa, na upingamizi ambazo penine hazikujitokea wakati wa majadiliano ya moja kwa moja. Inawaruhusu wahudhuria kukosoa dhana zao juu ya kinachotokea, ambayo inaweza kusababisha wao kufikiria upya uelewa wao wa hali na hivyo kuathiri nini kinachotathminiwa. Mwezeshaji anaweza kutambua pale palipo na maada zinazofanana na pale mawazo tofauti yanapotokea.


Lengo
Ramani za mazungumzo zinawakilisha uelevu na maangalizi tofauti juu ya jambo ambayo yanajitokeza kutoka mazungumzo.
Wapi pa kutumia ramani ya mazungumzo
Zana hii inaweza kutumika kukamata maoni, hisia na majibu tofauti kwa jambo la 'kifyatuzi' fulani. Kwa kawaida hilo jambo la kifyatuzi linakuwa likiwekwa kama swali, k.m. “Yapi ni mazoea yako ya kuhudhuria kwenye utekelezaji wa mbinu za makabiliano dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi?” Au “Nini ulithamini zaidi kutokana na mahudhurio yako kwenye utekelezaji wa mbinu za makabiliano dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi?”

Jinsi ya kutumia ramani ya mazungumzo
- Andika jambo la kifyatuzi katikati mwa karatasikubwa na chora duara kuizunguka.
- Mwombe mojawapo wa wahudhuria kuitikia kifyatuzi hicho na kuanza mazungumzo ambayo yatakuwa yakinukuriwakwenye karatasi na kuunganishwa na kiyatuzi kilicho katikati.
- Waombe wengine waitikie mwitikio wa kwanza au kifyatuzi na nukuru mchango wao pia ili ramani ianze kutawanyika. Usijaribu kuipa ramani umbo lolote maalum, kwani zana hii ni kwa ajili ya kuelewa upana mzima wa maoni yaliyokuwepo bila kujaribu kuyakusanya na kuyachanganua kwa hatua hii.
- Ramani ikianza kuzidi ukubwa wa karatasi, ongezea karatasi nyingine kwa kubandika. Ni kawaida kwa ramani kuonekana kuwa vurugu na kujaa taarifa nyingi.
- Watu wakiridhika (au muda ukiisha), ni muda wa kufikiria juu ya ramani (na mchakato wa kuitengeneza). Waombe wahudhuria kujadili kinachoonyeshwa kwenye ramani na juu ya mitazamo yao au uelevu wa kifyatuzi. Chora maada kuu na chocote kilichobadilika kuhusu mitazamio ya watu kutokana na uchoraji wa ramani hii.
Zoezi la orodha ya ushindi
Aina nyingi ya mazoezi shirikishi ya orodha ya ushindi insaidia tathmini, hasa kwenye hatua za kukusanya na kuchanganua takwimu, kwa ajili ya kuweka kipaumbele kwa kutekeleza au kuangalia utendaji wa mbinu mbali mbali kulngana na vigezo vilivyokubalika, pamoja na taarifa nyingine. Kupanga umuhimu kwa ngazi ilikwishaelezwa kwenye “Kupanga mpango wa kukusanya ushahidi” ya Hatua ya 5.
Michoro ya Venn
Michoro ya Venn ni mbinu ya kuwakilisha uhusiano kati ya wadau na tofauti ya nguvu kati yao. Inaweza kutumika kwenye tathmini kufananisha jinsi gani uhusiano kati ya wadau wakuu ulifikiriwa mwanzo wa utekelezaji wa mbinu za makabiliano na jinsi uhusiano huu ulivyo mwishoni. Pia, zinaonyesha jinsi uhusiano unavyobadilika na sababu zake. Michoro ya Venn imeelezwa kwenye Sehemu ya 2, Hatua ya 2.
Mbinu nyingine bayana na za masimulizi
Kuna idadi kubwa ya zana nyingine shirikishi ambazo zinaweza kutumika kukusanya ushahidi wa ubora, ambao mara nyingi unahitajika kujib aina nyingine ya maswali ya tathmini, lakini inahitaji muda na rasilimali zaidi. Mbinu hizi hazitajadiliwa kwa kiina hapa, lakini zimetajwa ili kuonyesha upana wa zana zilizopo kwa wale watakaopenda kufanya tathmini inayochunguza mazoeay ya wahudhuria kwa kina zaidi. Kwa taarifa zaidi juu ya kila mbinu, tafhadhali fwata vitovuti vilivyoonyeshwa.
Maigizo shirikishi
Maigizo shirikishi ni mazungumzo ya wadau wengi inayotumia maigizo kama njia isiyo rasmi, iliyo bunifu lakini isiyotaka mzaha ya kuchingiza matazamio na mwitikio tofauti kwenye mlolongo wa thamani ya kahawa. Inaruhusu washiriki tofauti kubadilishana taarifa, kuunda na kuweka kipaumbele maswala na kutambua kwa pamoja masululisho kwa kuandika haithi fupu na kuiigiza.
Hii haihusu uandikaji na uchazaji rasmi wa maigizo. Neno 'maigizo' inarejea tu hali ya wahudhuria kuwa 'waigizaji', wanaoandika, wanaohadithia ,a kuigiza hadithi fupi, na pia wakiwa 'hadhira shiriki' wanaotazama maigizo mafupi. Wazo ni kuwa, baada ya kila hadhithi, ,ajadiliano yanafanyika kati ya waigizaji na watazamaji, kinyume na maigizo ya kawaida ambapo waigizaji wanawakilisha na hadhira wanatazama tu. Wajibu wa hadhira ni kuwasaidia wahudhuria wa kila kikundi kuchinguza kwa ukina zaidi tatizo na sululisho zilizowakilishwa.
Mfumo huu umetumika sana ulimwenguni kote (mara nyingine inaitwa 'maigizo kwa maendeleo') na imekuwa na mafanikio sana kwenye sekta ya kahawa nchini Uganda.
Video shirikishi ni zana ambayo inatumika na wahudhuria kusimuia hadithi juu ya yale yaliyobadilika kutokana na utekelezaji wa mbinu za makabiliano dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi kwenye eneo lao. Filamu inayokamilishwa inaweza kutmika kuwakilisha mawazo yao kwa wafadhili na mafanya maamuzi walio nje ya eneo hilo. Hivyo, mafunzo waliyoyapata yanaweza kuwakilishwa kwa watu wengi zaidi ili kuathiri michakato ya kufanya maamuzi nje ya sehemu ndogo ya mradi.
Hadithi za picha zinaweza kutumika kwa njia hiyo hiyo ili kuelezea jinsi gani maishilio, udhaifu na fursa zimebadilika tangu mchakato wa makabiliano uanze, na maoni ya mhudhuria maalum juu sababu zilizoathiri hii, km. mkulima wakahawa.
Hii ni zana rahisi. Kila mhudhuria wa kikundi anaazimwa kamera na anaombwa apige picha ya vitu ambavyo anahisi vinawakilisha sehemu mojawapo ya mazoea yake yanayotokana na mchakato wa makabiliano.Hii inweza ikawa pia vitu vilivyofanikiwa na vitu vilivyoshidikana, na chochote kingine ambacho pengine hakikuttarajiwa.
Maelekezo yako yanaweza pia yakawa ya kina zaidi, k.m. waombe wahudhuria wapige picha 10 za vitu wanavyoona vilifanikiwa, na picha 10 ya kuwakilisha chochote kile kinachohitaji maboresho. Kamera zikirudishwa na picha kuchapishwa, unaweza kuzitumia hizi kufananisha na kutofautisha, na pia kusisimua majadiliano. Tafuta pale picha zinapofanana.
Ramani ya matokeo iliundwa na Kituo cha Kimataifa cha Utafiti wa Maendeleo nchini Kanada (IDRC) kama njia ya kupanga, kuchuguza na kutathmini kwa kuwekea mkazo wa kutafuta sababu za matokeo ya miradi, badala ya kujaribu kupima moja kwa moja sababu za mabadiliko kutokana na miradi ya shirika maalum.
Ramani ya matokeo inasaidia sana kwenye tathmini ya mbinu za makabiliano, kwani inakubali kuwa michakato ya makabiliano ina utata na hubadilika; inatambua kuwa kuna matokeo mengi yasiyotarajiwa wala kupangwa kwa mbinu lolote. Pia inakubali kuwa matokeo yanatokana na sababu mbali mbali badala ya shughuli moja tu. Ramani ya matokeo inatoa njia ya kuvuta pamoja michango mingi tofauti ya matokeo, kitu ambacho ni muhimu ili kujifunza zaidi juu ya sababu zinazochangia makabiliano yanayofanikiwa.
Msingi wa mbinu hii ni kusilikiza ni nini watu (waliofikihwa mradi, wahudhuria, wadau, n.k. ) wanafikiria kuwa mabadiliko muhimu kutokana na mchakato wa makabiliano. Haihitaji utaalamu wowote kwa kuwezesha na ni rahisi kuwasilishwa kwa utamaduni mbali mbali, kwani watu wansikia rahisi kusimulia hadithi juu ya matukio wanayoyaona kuwa muhimu kwa.
Hakuna haja ya kueleza nini ni ishara na ni njia nzuri ya kupata maelezo juu ya mabadiliko yasiyoktarajiwa, na mabadiliko ambayo yanaweza kukosoa dhana juu ya yale yanayotokea. Mbinu hii inawatia moyo watu kujishughulishwa kwenye hatua za kukusanya takwimu, kwani wanahitaji kueleza sababu za badiliko moja kuwa muhimu zaidi kuliko badiliko lingine. Inaweza kutumika kuchunguza na kutathmini miradi inayoanzwa na ngazi za chini ambazo hazina matokeo ambayo yalishapangwa awali kwa ajili ya kutathmini.
Mbinu hii ya kujifunza historia inaelezwa kuwa 'hadithi inayosimuliwa kwa pamoja' kati ya watafiti kutoka nje na watekelezaji wa ndani wakijadili tokeo moja linaloshikika. Inalenga kuunganisha tathmini na hadithi kwa njia iliyo na thamani wa wale waliohudhuria kwenye kazi na wengine wanaolenga kujifunza kutokana nayo.
Maelezo ya kujifunza historia inajaribu kuingia ndani ya vipengele vya kibinadamu 'vilivyovurigika'' wakati wa utekelezaji. Inalenga kuwakilisha baadhi ya mitazamiao juu ya hali badala ya kufupisha mazimulizi mengi kuwa hadithi moja. Inwakilishwa kama masimulizi ya sauti nyingi na ya ngazi nyingi inayochora ramani ya yale yaliyotokea, na inatoa nukuu kutoka kwa wale walioshirikishwa na mawazo kutoka watafiti wakati wa .